Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Kaimu Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola ameanika mikakati yake ya “kutumbua majipu”
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola, akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis
Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola ameanika mikakati yake ya “kutumbua majipu” akisema kwa sasa taasisi yake inashughulikia kesi 36 kubwa, zikiwamo zinazosubiri uchunguzi baada ya kuibuliwa na Rais John Magufuli.
Miongoni mwa kesi hizo ni ya kampuni ya Lake Oil, inayotuhumiwa kuingiza kwenye soko la ndani mafuta yaliyotakiwa kwenda Congo na hivyo kukwepa kodi ya Sh8.5 bilioni, ya upatikanaji wa wazabuni kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa inayomkabili mkurugenzi wa zamani wa Rahco.
Pia, imo kesi ya ununuzi wa mabehewa 25 mitumba uliokiuka Sheria ya Ununuzi, na ya hati fungani iliyohusu malipo ya dola 6 milioni za Marekani kwa kampuni ya Enterprise Groth Market Advisors (EGMA) zilizotokana na mkopo wa Serikali wa dola 600 milioni za Marekani.
“Waliokuwa wanadhani kwamba kuna uholela serikalini, the game is over (mchezo umekwisha). Wajipange upya,” alisema kaimu mkurugenzi huyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mlowola alisema kati ya kesi hizo, zipo zilizokamilika na kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kuombewa kibali cha kuwafikisha mahakamani waliobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Mlowola alisema taasisi yake itafanya kazi ili kufikia azma ya Rais Magufuli ya kupambana na rushwa na ufisadi ili kuliletea Taifa maendeleo.
“Rais anapozungumzia kwamba amejipa kazi ya kutumbua majipu, tambueni kwamba Takukuru ndiyo vidole vya Rais katika kutumbua majipu hayo. Kasi ya kufanya shughuli hiyo ni yetu na mwenye vidole akishaamua kutumbua jipu, kazi ya vidole ni utekelezaji tu,” alisema Mlowola na kusisitiza kwamba hakutakuwa na mchezo katika suala la maadili.
Mlowola alitaja baadhi ya kesi ambazo uchunguzi wake unaendelea kuwa ni pamoja na tuhuma mbalimbali zinazomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (Rahco), Benhadard Tito baada ya kubaini kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za kuwapata wazabuni kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa.
Mkurugenzi huyo alitaja kesi nyingine kuwa ni ile ya ununuzi wa mabehewa ya kokoto ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Alisema ununuzi wa mabehewa 25 ya kokoto kutoka kampuni ya Hindustan Engineering and Industries ulikiuka Sheria ya Namba 21 ya Ununuzi ya Umma ya Mwaka 2004.
“Tupo katika hatua za mwisho kukamilisha uchunguzi wa kesi hii na tutawafikisha mahakamani wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa bila kujali hadhi zao wala nyadhifa walizonazo,” alisema Mlowola ambaye anakaimu nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Dk Edward Hoseah aliyeondolewa kwa kutoshughulikia kikamilifu sakata la utoroshaji makontena bandarini.
“Tayari baadhi ya watuhumiwa kwenye kesi hii tumeshawakamata na kuwahoji, akiwamo raia wa Kenya aliyekuwa mtu muhimu katika mchakato huo wa kumpata mzabuni.”
Kuhusu Lake Oil, Mlowola alisema kampuni hiyo ilifanya udanganyifu kwa kuuza kwenye soko la ndani lita 17,461,111 za mafuta ya petroli ambayo ilidanganya kwamba imeyasafirisha kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mlowola alisema kuwa ametoa muda wa miezi miwili kwa Lake Oil kulipa Sh8.5 bilioni kwa kulisababishia Taifa hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kukwepa kodi na watafikishwa mahakamani endapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.
Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba taasisi yake iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha uchunguzi wa kesi ya hati fungani, shauri linalohusu malipo ya dola 6 milioni za Marekani kwa kampuni ya EGMA ili kuisaidia Tanzania kupata mkopo wa dola 600 milioni za Marekani.
“Takukuru imebaini kwamba fedha hizo zilitakatishwa na watumishi wa umma wasio waaminifu wakishirikiana na baadhi kutoka sekta binafsi wakifahamu kuwa wamezipata kwa njia haramu,” alisema Mlowola.
Atoa angalizo
Mlowola ametoa angalizo kwa makundi mbalimbali ya watu kujihadhari na vitendo vya rushwa na kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria. Aliyataja makundi hayo kuwa ni maofisa wa umma wanaohusika na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Alitaja kundi jingine kuwa ni wale wanaohusika na matumizi ya Serikali, kwa mfano wakurugenzi wa halmashauri na maofisa ugavi wa taasisi mbalimbali. Alisema matumizi yote ya Serikali yanaongozwa na sheria ya ununuzi, kwa hiyo wazingatie sheria hiyo.
Makundi mengine ni watoa huduma kwenye ofisi za umma pamoja na wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla. Alisema watoa huduma kwenye taasisi za umma wamekuwa wakiomba rushwa kwa wananchi bila kutimiza wajibu wao. Aliwataka kujihadhari na tabia hiyo kwa kuwa nyakati zimebadilika.
Tutajitahidi kupambana na rushwa kubwa kwa sababu ndiyo zinasababisha rushwa ndogo kutokana Serikali kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi na kuwafanya watafute mbinu nyingine za kuongeza kipato chao,” alisema.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuwatumikia wananchi wake kwa kulitokomeza tatizo la rushwa na ufisadi nchini na wataendelea kuzuia na kupambana na rushwa nchi nzima.