Takukuru yabaini mapungufu katika miradi Rukwa

Takukuru yabaini mapungufu katika miradi Rukwa

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Rukwa imetekeleza ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 6.7 katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU, kiasi cha Shilingi 422,280,519 kilichotolewa kama mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kilifuatiliwa. Vilevile, ufuatiliaji umefanyika katika makadirio na makusanyo ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mwaka wa fedha 2023/24 yenye jumla ya Shilingi 4,200,335,330.12.

TAKUKURU pia ilifuatilia utekelezaji wa miradi mitano yenye thamani ya Shilingi 2,155,077,028, kwa lengo la kubaini ubora na thamani halisi ya fedha zilizotumika. Katika ukaguzi huo, miradi kadhaa ilibainika kuwa na mapungufu na ushauri ulitolewa ili kufanya marekebisho.

Miongoni mwa mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na:

1. Upungufu wa mafundi na vibarua katika baadhi ya miradi, hali iliyopelekea ucheleweshaji,

2. Kuchelewa kufikishwa kwa vifaa vya ujenzi katika maeneo ya miradi,

3. Changamoto ya mfumo wa manunuzi (NEST) iliyosababisha kuchelewa kupatikana kwa fundi mkuu,

4. Kutojengwa kwa baadhi ya miundombinu iliyoainishwa kwenye mikataba, mfano, katika ujenzi wa Kituo cha Afya Sumbawanga, incinerator ya kuteketeza taka haikujengwa.

Soma Pia: Mtendaji wa kata Sumbawanga ahukumiwa miaka 60 jela kwa uhujumu uchumi
1757592107180.png

Chanzo: Vosfmtz
 
Back
Top Bottom