Takukuru wanasa vyerehani 15 ofisi za CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru wanasa vyerehani 15 ofisi za CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 3, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  Takukuru wanasa vyerehani 15 ofisi za CCM Saturday, 03 July 2010 06:47

  Zulfa Mfinanga, Shinyanga
  Mwananchi


  VYEREHANI 15 vimekamatwa katika ofisi ya CCM wilayani Shinyanga vilivyotarajiwa kugawiwa wanawake wa chama hicho ikiwa ni wiki mbili baada ya mtangaza nia mmoja wilayani Maswa kukamatwa na Takukuru akigawa pikipiki tano kwa wakazi wa eneo la Malampaka.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Leonalda Ngaiza alisema vyerehani hivyo vimekamatwa kutokana na malalamiko ya kuwepo kwake ofisini humo suala lililoilazimu ofisi yake kufuatilia na hatimaye kuvikuta katika ofisi ya CCM wilaya vikiwa katika marekebisho ya kuviunganisha.

  Aidha, alisema kuwa tayari walishamhoji Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mwenyekii UWT na pia diwani wa kata ya Kitangiri, Moshi Kanji pamoja na katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Mwasiti Rajabu.

  “Katika hatua ya awali tayari tumeshamhoji mwenyekiti wa UWT pamoja na katibu wake….lakini bado tunaendelea na uchunguzi ili kujua vimetoka wapi, kwenda kwa akina nani na pia vilikujaje,” alisema Ngaiza.

  Aliongeza kuwa pia ofisi yake imepokea taarifa kutoka wilaya ya Bukombe kuwa kuna baadhi ya watu tayari wameshagawa vyerehani hivyo kuahidi kufuatilia kama waliofanya hivyo huko Bukombe kama ndiye huyo aliyetoa wilaya ya Shinyanga.

  “Pia huko wilayani tumepokea taarifa kuwa kuna watu wameshagawa vyerehani, ndio tunataka kujua kama ndio hawa hawa kwani huyu wa Shinyanga ni mmoja wa wawania ubunge wa viti maalum... lakini bado tutaendelea kuwahoji watu mbalimbali waliopo ndani ya mkoa na nje ya mkoa,” alisema.

  Kamanda Ngaiza alisema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kutokana na uzito wa ushahidi kwani ni mapema sana kuzungumzia adhabu ya jambo hili.


   
 2. S

  Subira Senior Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa kweli hao takukuru wa shinyanga ni bigup kwa saaana maana hawa wa arusha
  ni rushwa tupu mgombea fulani anapikisha pilau na kuwalisha wananchi kila mara with no respond na inajulikana, mwingine mgombea anakuja katikati ya mji na kugawa
  shs elfu mbilimbili hadharani, hakuna anaechukua hatua , na wanaarifiwa kwa kweli hapa arusha ni hatari tupu wagombea vingunge wanagawa pesa, wanatishia wananchi lakini takukuru imefumbia macho.

  je hawapo hapa arusha au wamenunuliwa?
   
 3. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Na bado, Takukuru wataendelea kugundua madudu mengine mengi tu mwaka huu!
   
Loading...