Takukuru wadaiwa kusababisha hasara Vodacom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru wadaiwa kusababisha hasara Vodacom

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by PayGod, Jan 18, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Takukuru wadaiwa kusababisha hasara Vodacom Send to a friend

  Phinias Bashaya, Bukoba
  MAOFISA wawili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) Mkoa wa Kagera wanahusishwa na upotevu wa zaidi ya Sh 9 milioni ,uharibifu wa samani na simu katika ofisi za kampuni ya simu za mkononi Vodacom baada ya kuwa chanzo cha vurugu katika ofisi hizo mjini hapa.
  Katika tukio hilo la Januari 10,maofisa hao walifika katika ofisi za kampuni hiyo wakimshikiza kwa kumpa kichapo Meneja wa ofisi hiyo Michael Bigambo ili awape baadhi ya vielelezo walivyohitaji kwa ajili ya kazi za taasisi hiyo.

  Akisimulia mkasa huo meneja huyo alisema alikuwa na makubaliano na maofisa hao ya kupewa vielelezo walivyohitaji,ingawa aliwaambia wawe wavumilivu kwani alihitaji ruhusa kutoka makao makuu ya kampuni hiyo baada ya kufanya mawasiliano.

  Pia alisema kabla ya kupewa kichapo kwa madai ya kuwadharau maofisa hao, Desemba 31 mwaka jana alifika ofisa aliyejitambulisha (jina linahifadhiwa) akitaka vielelezo hivyo na kuahidi kuwa angevitoa baada ya kuwasiliana na makao makuu ya kampuni.

  Hata hivyo Meneja huyo ambaye alijeruhiwa sehemu ya goti na kudai anaendelea kusikia maumivu alikutana na ofisa huyo nje ya ofisi Januari 7 na kumjulisha kuwa alikuwa amejibiwa tangu Januari 5 na wanaweza kufika kwa ajili ya kuchukua taarifa hizo.

  ''Alifika ofisa wa Takukuru Desemba 31,akiwa na barua ya kuomba kupatiwa nyaraka za siri kwa ajili ya uchunguzi,nilisema ombi hilo nalituma makao makuu kwani sina mamlaka ya kutoa taarifa walizohitaji''alisema Bigambo

  Hata hivyo alidai siku ya tukio walifika wakitaka nyaraka hizo na kwa vile alikuwa anatoa nyaraka nyingine kwa Ofisa upelelezi wa Mkoa wa Kagera Peter Matete aliwaomba wavumilie ili aweze kuwapatia taarifa hiyo.

  Kwa mujibu wa Michael Bigambo mmoja wa maofisa hao alimkwida shati kwa madai ya kuwadharau na kusababisha vurugu kubwa zilizoleta taharuki kwa wateja ambao walikuwa wakisubiri huduma ya M-Pesa na kumshushia kipigo kilichokuwa chanzo cha upotevu wa pesa na uharibifu wa mali mbalimbali.

  Alipoulizwa kuhusu tukio hilo Ofisa upelelezi wa Mkoa wa Kagera, Peter Matage alikiri kuwa katika chumba cha faragha ndani ya ofisi hizo wakati vurugu zikitokea na kuwa anachofahamu yeye ni kuwa alishiriki kutuliza hali hiyo kwa kuwasuluhisha.

  Lakini hakuwa tayari kuzungumza kama malalamiko ya tukio hilo yamefika ofisini kwake.
  Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Takukuru, Exevery Mhyela alikiri maofisa wake kuwa katika ofisi za kampuni hiyo siku ya tukio na kudai hawezi kutoa maelezo zaidi kuhusiana na kazi ya uchunguzi.
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kunahitajika uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli.
   
 3. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh!!
   
 4. m

  mams JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sasa Takukuru wamepata wapi mamlaka ya kupiga, uchunguzi zaidi unatakiwa!
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inaelekea kufuatia usajiri wa simu "privacy" ya watumiaji wa simu iko mashakani; kulingana na maelezo haya inaelekea vyombo vya upelelezi vinapigana vikumbo katika makampuni ya simu kwaajili ya kupata habari ya mawasiliano binafsi. Kuna umuhimu wa kutafuta uwezekano wa kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya simu katika ngazi ya taifa ili kuwaondolea maafisa wa ngazi za mkoa hadha ya kupambana na hivi vyombo vya dola.
   
Loading...