TAKUKURU Tanzania mpo wapi?

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
Wasalam wakuu.

Moja kati ya hotuba za Baba wa Taifa Mwalimu Jk Nyerere mwaka1995.
Alisikika akisema "anayetoa rushwa na anaepokea rushwa wote wana makosa adhabu ni viboko 12 akiingia jela akitoka 12 akumuonyeshe mkewe.
Anaendelea kusema Rushwa ni adui mkubwa wa haki japo kwa kipindi cha utawala wake ilikuwepo lakini walikiwa wakali sana kupambana na rushwa."

Anamalizia hotuba yake kwa kufananisha Rushwa na Kansa kwamba rushwa ni ugonjwa mbaya sana.


Kadiri siku zinavyozidi kwenda nchi yetu imekuwa ikikithiri kwa Rushwa, tumekuwa tukishuhudia upendeleo katika nafasi za ajira tenda na hata nafasi ndogo kabisa.

Maandiko matakatifu yanafananisha kwa kiasi kikubwa sana Rushwa na upofu.

Taifa linaelekea kwenye upofu kutokana na Viongozi kushadadia Rushwa . Viongozi wapo mstari wa mbele kuibadilisha jina Rushwa kila kitu mfano.
Takrima.
Hongo.
Kitu kdgo
Mzigo nk.

Taifa linaangamia kwa RUSHWA.
Tumeshuhudia katika kura za maoni ndani ya chama cha Mapinduzi kukiwa na rushwa nje nje.

1.Rushwa ya kofia.
2.Rushwa ya Tshirt.
3.ugawaji wa kanga.
4.ugawaji wa vitambaa.
5.Ugawaji mkubwa wa vilemba na skafu.
6.Rushwa ya Fedha ikiwa imetamalaki.

Chama cha mapinduzi kimeona zote hizo hazitoshi sasa rasmi Chama kimeamua kuwa na aina nyingine ya rushwa kama.
1. Kugawa ajira kipindi cha kampeni.
2.kuwapakiza wananchi kwenye Maroli.
3.kununua viongozi wa upinzani kwa madai ya kupita bila kupingwa.
4.Matamasha makubwa wa sanii katika kamlenk za Chama cha mapinduzi nk.

Katika tafakari yangu nashindwa kuelewa viongozi wa taasisi husika na mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi.
Je ni kweli wanamuenzi walimu nyerere kwa vitendo????
Je ni kweli wanamuenzi Baba wa taifa kwa Vitendo?????

Je hiki chama kinachosifika kwa Rushwa kweli hakijapoteza uhalali wa kuendelea kushika Dola???

TUJITAFAKARI.
MJUKUU WA MWALIMU.
 
Back
Top Bottom