TAKUKURU Mkoa wa Tabora imemfikisha Mahakamani, aliyekuwa Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mhandisi Mwita B. Joram

Jul 14, 2019
7
1
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Tabora imemfikisha Mahakamani, aliyekuwa Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mhandisi Mwita B. Joram kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa Mkandarasi wa ujenzi wa barabara. Mhandisi Mwita B. Joram kwa sasa ni mhandisi wa barabara huko TARURA, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

Mhandisi Mwita B. Joram alifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega Mheshimiwa Gradness Badha mnamo tarehe 12/07/2019 kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa Mkandarasi wakati wa utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. Mtuhumiwa akiwa Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, anatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa Mkandarasi mwezi Julai na Agosti mwaka 2018.

Kesi inayomkabili Mhandisi Mwita B. Joram ya tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa imeahirishwa hadi tarehe 14/08/2019 itakapotajwa tena kwa mara ya pili. Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
Serikali hii inaongoza kwa kufungulia kesi watu za UHUJUMU UCHUMI,NA UTAKATISHWAJI PESA WATU WANAOZEA MAHABUSU HUKU KUNA MTU ANAMISS USE PUBLIC FUND BILA KUGUSWA.
 
Back
Top Bottom