Yaani Mkuu huwezi amini huyo JRM yaani namjua Kindakindaki hadi naona hata aibu kumzungumzia / kumsema / kumchambua humu Jamvini. Narudia tena kusema yaani ninamjua hadi huwa kila nikimwona anahangaika na masuala ya Siasa huwa namshangaa na namuonea tu huruma. Naomba niishie hapa tafadhali na nimtunzie tu heshima yake kwani najua njaa ndiyo inamsumbua japo alikuwa na nafasi kubwa mno ya Kujiendeleza Kimaisha tena nje ya Siasa kwakuwa ni Kijana ambaye 90% ya maisha yake ameishi na Viongozi wote wakubwa wa nchi hii ukianzia kwa Rais Mstaafu Mzee Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Lowassa, Spika Mstaafu Hayati Mzee Samuel Sitta, Waziri wa Mambo ya Ndani sasa Mwigulu Nchemba, Mzee Stephen Wassira, Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, Wakurugenzi Wakuu wa TISS wa awamu iliyopita ya JK na Watendaji wake Waandamizi kabisa, CDF Mstaafu Mzee Mwamnyange. Kama angewatumia hapo Watajwa wote hapo kujiendeleza Kielimu na Kimaisha tokea zamani leo hii JRM angekuwa mbali na si Mtu wa kutaka kusumbuka na Siasa za Tanzania ambazo Mimi naziona hazina tija zaidi tu ya Mtu kujishushia hadhi yako katika Jamii na kuonekana wa hovyo hovyo. Hakuna maisha mazuri kama kuishi nje ya masuala ya Siasa.
Mkuu yangu ni hayo tu.