Takukuru Iringa, Fuatilieni kesi hii ya ndoa iliyokuwa Mahakama ya Mwanzo Bomani kwa Hakimu Rajabu muone aliyoyafanya

MTAKA HABARI

Senior Member
Jan 17, 2019
123
149
Naomba kwa dhati vyombo vyetu vya ulinzi na usalama fanyeni uchunguzi juu ya kesi hii,Mh Rajabu maamuzi uliyo yafanya katika shauri ulilolifanyia maamuzi tarehe 20/04/2022 linalo mhusu mtu anayefahamika kwa jina la Agatha kuhaga na Mumewe anayefahamika kwa jina moja la Nyenza ni kuinajisi sheria na kutokuwa na hofu na Mungu.

Mgawanyo wa mali ulioufanya una walakini.
  1. Kati ya viwanja 3 mwanamke mke 1
  2. Gari 3 mwanamke bila bila
  3. Pikipiki 4 mwanamke bilabila
  4. Bajaji 2 mwanamke bilabila
Kumbuka huyu mama ameachwa na watoto 2 wadogo. Na unajua pia mwanaume kamuacha mkewe kwa kuwa kapata Kimada mungine.

Halafu unasema apewe laki 1 ya matunzo kwa mwezi mhh.

Naomba kwa dhati kabisa serikali ifatilieni hukumu hii kuna mengi mtajifunza kwenye mahakama zetu.

Nafanya jitihada za kumpta huyu mama na namba zake ili nimuunganishe na watu wanaoweza kumsaidia.

Ila kwa taarifa zilizopo ni kwamba mkuu wa wilaya Iringa ameamua kuliingilia Jambo hili.
 
sasa mtu anapewa lak 1,kila mwez ,unataka apewe gar,au pkpk ,apeleke wapi !?, Akahonge wanaume!!! shutup kabisa.
 
Mleta mada ni mp....bavu kila mwezi laki moja ni kubwa mno tena sana je? umeuliza kuwa hizo mali walichuma wote au huyo mama alikuwa mama wa nyumbani tu.
 
Mleta mada ni mp....bavu kila mwezi laki moja ni kubwa mno tena sana je? umeuliza kuwa hizo mali walichuma wote au huyo mama alikuwa mama wa nyumbani tu.
Siamini kama hukuzaliwa kwa bahati mbaya.kwa mujibu wa taarifa zilizopo mali walichuma wote,na hata baadhi ya mali aliandika majina ya huyo dada
 
Kwa mujibu wa taarifa ni mwanamke,sababu ni kwa kuwa jamaaa kaitelekeza familia na kuhamia kwa mwanamke mwingine
 
Siamini kama hukuzaliwa kwa bahati mbaya.kwa mujibu wa taarifa zilizopo mali walichuma wote,na hata baadhi ya mali aliandika majina ya huyo dada
nyuma ya pazia huwezi kujua usimhukumu huyo jamaa bila kujua huyo mwanamke pengine ndiyo chanzo cha talaka au kama unaona wivu wa mali olewa wewe
 
Kama Haujatidhika na maamuzi ya Uyo Hakimu Kata rufaa sio kupiga kelelee Hata uyo DC awezi batilisha iyo Hukum ispokua Mahakama ya Juu.

Sasa kama mama alikua Mama wa Nyumbani ulitaka apewe nini? Nyie ndio mnao tupa wanaume shida na Mahaki yenu hayo. Sasa endeleeni Kupiga keleee JF badala ya kukata rufaa afu muda upite ndo Mtajua ignorance of Law has no excuse
 
Back
Top Bottom