TAKUKURU chunguzeni Vodacom Premier League

fastum

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
337
220
Nimekua nafuatilia sana hizi mechi za vodacom premier leaque ,
Nianze na Simba na Yanga, hizi ndo timu hapa Tanzania zinadumaza mpira kwanza wao ndo wanaongoza kutoa rushwa kwa hizi timu ndogo zinazochipukia kwa hiyo hata mpira wanaocheza hauhitaji umakini sana ili mradi tu wameonga ili wapate ushindi na hili ujue hao ndo wanaodumaza mpira hapa angalia wanavyocheza mpira na timu za nje timu inapata nafasi 16 goli moja jamani hapo kuna striker kweli au mbwebwe tu mwisho wasiku hatufiki mbali tunatolewa kwenye mashindano.pia kuna mechi ambazo nimeshuhudia kwenye kahawa matokeo ya mpira kabla haujachezwa yanajulikana tena viongozi kabisa wanasema wamekaa na timu pinzani wameelewana bei so wanashinda au wanashindwa kutokana na walioelewana.
Pili hizi timu zetu za mkoani zinazopanda daraja na hata ambazo zipo kwenye leaque kwa muda mrefu ,hizi timu kwa sababu ya hali zao za uchumi timu inakubali kuongwa hela ili iweze kusafiri,kulipa pa kulala kula na hata kulipa mishahara kwa wachezaji mwisho wa siku hizi timu hali yao huwa sio nzuri huishia kushuka na hata wachezaji wao ushindwa kuonesha kiwango chao uwanjani kwa sababu wamezoea kuongwa na kukubali kupoteza michichezo kwa hiyo kiwango chao uishia hapo au kwa vile pia wao ni mashabiki wa Simba na Yanga ununuliwa na hao hao na hali ya mpira huwa hiohivo miaka nenda miaka rudi.
Mwisho haya yote yakibadilika ndipo tutasonga mbele.nawakilisha.
 
Tuthibitishie kuwa yanga na simba wanatoa rushwa....yanga na simba kutawala mpila Wa bongo isiwa ndo sababu ya rushwa,hata Spain Barcelona na real Madrid hufanya hivyohivyo,acha wivu
 
Tuthibitishie kuwa yanga na simba wanatoa rushwa....yanga na simba kutawala mpila Wa bongo isiwa ndo sababu ya rushwa,hata Spain Barcelona na real Madrid hufanya hivyohivyo,acha wivu
Ni ushahidi tu unakosekana.

Ukipatakina ushahidi kama ule JUVENTUS akashushwa daraja itakuwa poa.

Juzi PIQUE alikuwa analalamika namna waamuzi wanavyoibeba RMA. Issue ni ushahidi tu, Yanga na Simba ni tabia zao hizi.
 
Ni ushahidi tu unakosekana.

Ukipatakina ushahidi kama ule JUVENTUS akashushwa daraja itakuwa poa.

Juzi PIQUE alikuwa analalamika namna waamuzi wanavyoibeba RMA. Issue ni ushahidi tu, Yanga na Simba ni tabia zao hizi.
So,ka huna ushahidi basi huna haki ya kusema
 
Jamani ushahidi unawezekana tu kupatikana tena very simple kama TAKUKURU itaacha pia ushabiki wa simba na yanga
 
Kisa Yanga kachukua Ubingwa sio?lengo lako uliilenga Yanga ili kuzuga ukaona uwaingize na Wamatopeni a.k.a Mezani Fc.
 
Back
Top Bottom