Napenda kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kurudisha discipline serekalini. Kwa yeye mwenyewe kuona uozo na ufisadi kwenye idara zote za serekali ni ngumu inabidi asaidiwe.
Inasikitisha sana kuona mashirika na taasisi ya serekali ambayo yangeweza yakaendeshwa kwa faida kubwa yanaendeshwa kwa hasara kutokana na uongozi dhaifu. Mfano mkubwa ni wakala wa majengo ya serekali (TBA). Dhumuni kubwa la TBA ni kuwasaidia watumishi wa serekali wapate makazi bora.
TBA imekuwa ikikabiliwa na tuhuma zifuatazo:
1. Ubadhirifu wa fedha za mauzo na ujenzi wa nyumba za serekali. Hili suala limekuwa likifumbiwa macho na wakaguzi wa serekali (NAO) na kamati husika ya bunge.
2. Uongozi mbovu usiokuwa na ubunifu. Viongozi wa TBA na ndugu zao waliowapa ajira za muda wameifanya TBA kama ni mtandao wao wa kujinufaisha binafsi. Kuna ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu za serekali.
3. Wengi wanaofaidika kuuziwa nyumba mpya na zamani za serekali ni maafisa na vigogo wa serekali. Watumishi wa kawaida kupata nyumba ya TBA ni ndoto.
4. Mfumo mbovu katika usimamizi wa rasilimali za taasisi mfano rasilimali watu na fedha. Kitengo cha ukaguzi wa ndani ni kama hakipo.
Waziri mwenye dhamana anaonekana kulifumbia macho suala hilo. Nawaomba TAKUKURU, CAG, WABUNGE NA MAGAZETI wazifanyie kazi tuhuma hizo ili kumsaidia Rais wetu kusafisha ufisadi na uozo wa TBA na mashirika yetu ya serekali.