magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,201
- 3,322
Wanabodi, Salaam;
Jana kuna taarifa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kukamatwa kwa mwenyekiti wa Simba FC na baadae kuthibitishwa na maafisa wa TAKUKURU kwa kile walichoeleza kuwa Aveva alichepusha fedha za usajili wa Emmanuel Okwi. Yaani makosa ya Aveva ni kupitisha fedha za simba kwenye akaunti yake binafsi.
Sakata la Aveva halina tofauti na sakata la fedha za Escrow alizogawa James Lugemalira kwa baadhi ya taasisi lkn fedha hizo zikaingizwa kwenye akaunti binafsi. Mfano, askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilaini pesa za kanisa ziliingizwa kwenye akaunti yake binafsi, halikadhalika Anna Tibaijuka aliwekewa pesa za shule katika akaunti yake.
TAKUKUU huenda wakati ule haikuwa na makali kama haya iliyonayo kwa sasa. Nawakumbusha hilo deal. Pia ikibidi na wale waliotajwa kubeba fedha kwenye viroba katika benki ya Stanbic. Isiwe nongwa kwa Aveva tu.
Nawasilisha!