Tabia hizi zipo kila Kona... Jamani tubadilikeHabari za sikukuu!
Biashara ya miwa imeshika kasi sana maeneo ya Mbagala hasa toka kizuiani mpaka Mbagala rangi tatu, ukipita njia ya Mbagala maeneo hayo utakuta vijana wengi sana wanajipatia ridhiki yao kwa kufanya biashara hiyo ambayo kiukweli inafanya vizuri kutokana na muonekano wa maeneo biashara hiyo inapofanyika.
Wateja wengi wa biashara hiyo ni watu walio kwenye vyombo vya usafiri haswa mida ya foleni kipindi cha jioni. Tatizo lililopo ni kwamba walaji wengi wa hiyo miwa pamoja na wauzajj hawazingatii swala la usafi wa mazingira wa maeneo biashara hiyo ilipo kwani utupaji hovyo wa makapi ya miwa baada ya kutafunwa unafanyika maeneo hayo kiasi kwamba kuanzia makapi ya miwa yaliyozagaa barabarani, pamoja na kwenye mitaro.
Nawasihi wahusika ambao wauzaji wazingatie swala la usafi wa mazingira kwa kuzikusanya taka hizo ili zikatupwe kwenye dampo lililo rasmi na wateja walio kwenye magari wasitupe hovyo makapi ya miwa waliotafuna bali watupe kwanye ndoo za taka zilizopo kwenye mabasi ya abiria.
Well said... onyo linatuhusu site....mtu na akili zake kabisa(Sijui kama ni TIMAMU) anatupa uchafu sehemu ya public bila hata kujali(Sijui anahisi kuna watu wa kufanya usafi)
halafu taka zikijaa mtu huyo huyo anaanza kulalamika "Haya maeneo machafu kweli"
Mi nashangaa sana
kuja kufikia civilization ya first world countries SIO LEO
Usafi ni tabia wala sio issue ya kushurutishwa na mtu,ni jambo la kimalezi toka utotoni,tuanze kuwafundisha watoto toka utotoni issue ya usafi na kuweka mazingira katika hali safi,mtu mzima na midevu yake ukimwambia kwanini unatupa taka hapa? mnaweza hata kupigana badala ya yeye kuelewa kua lile ni kosa na sio ustaarabu!Hivi kwani ile sheria ya utupaji taka ovyo unatoa faini haipo tena?
Kuna watu pasipo shurti hawaendiUsafi ni tabia wala sio issue ya kushurutishwa na mtu,ni jambo la kimalezi toka utotoni,tuanze kuwafundisha watoto toka utotoni issue ya usafi na kuweka mazingira katika hali safi,mtu mzima na midevu yake ukimwambia kwanini unatupa taka hapa? mnaweza hata kupigana badala ya yeye kuelewa kua lile ni kosa na sio ustaarabu!
Hebu pandikizeni Inzi wa kipindupindu hapo, watu wata- surrender wenyewe! Maana mtu msafi kamwe hapati kipindupindu, never!Inzi wanapenda sana taga mayai kwenye hizo taka taka za miwaa... na kipindi cha mvua ndo inzi wanaongezekaaa
Siku Inzi akiwa serious kama nyuki, basi mambo yatabadilika sana
Chungu kaona kivunoGanda la muwa la jana....