Tajiri nambari moja duniani atua Arusha................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tajiri nambari moja duniani atua Arusha...................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 31, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Tajiri nambari moja duniani atua Arusha


  *Awasili uwanjani KIA na ndege nne binafsi
  *Yuko na wafanyabiashara wakubwa hamsini
  *Pesa yake ni bajeti ya Tanzania mara nane


  Na Said Njuki, Arusha
  [​IMG]
  TAJIRI namba moja duniani, Bw. Mukesh Ambani (53) (pichani) raia wa India amewasili nchini jana alfajiri kimyakimya kwa safari ya
  kitalii.
  Tajiri huyo aliwasili jana saa 10.15 alifajiri Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na ndege nne binafsi akifuatana na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 50.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa waratibu wa safari hiyo hapa nchini, Bw. Godfrey Famandes zimeeleza kuwa lengo la safari yake ni kutembelea hifadhi za taifa, hususan Hifadhi ya Serengeti.

  Bw. Ambani kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kimataifa ndiye tajiri namba moja akimiliki dola za Marekani bilioni 63.2 (zaidi ya sh. trilioni 90), akifuatiwa na Carlos Slim Helu kutoka Mexico mwenye dola za Kimarekani bilioni 62.2993 na Mmarekani William Bill Gates akifuatia kwa karibu akimiliki dola za Marekani bilioni 62.29.

  Katika kundi hilo dogo la matajiri watano duniani nafasi ya nne inashikiliwa na Warren Buffett kutoka Mexico ambaye anamiliki dola 55.9 na kufuatiwa na Lakshmi Mittal wa India mwenye kitita cha dola bilioni 50.9.Akizungumza na njia ya simu jana, Bw. Famendes ambaye ni Mkuu wa Oparesheni wa Kampuni ya Gapco Tanzania ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo na mwenyeji wa
  tajiri huyo, alikiri kuwasili kwa tajiri huyo na kusita kuzungumzia safari hiyo zaidi.
  Safari yenyewe ni ya binafsi zaidi, hivyo sina cha kukueleza zaidi ya kukuthibitishia kuwa ni kweli amewasili…sina uhakika na idadi ya wafanyabiashara aliofuatana nao,� alisema Bw. Famendes kwa njia ya simu.

  Habari zaidi kuhusiana na safari hiyo zimeeleza kuwa tajiri huyo pamoja na wenzake wamewasili Hifadhi ya Serengeti, ambayo ina hadhi ya urithi wa dunia, na tayari jana walifanya mzunguko wa kwanza wa kutembelea hifadhi hiyo na kujionea maajabu ya dunia ya hifadhi hiyo.
  Kuja kwa mfanyabiashara huyo na wenzake na fahari kubwa kwa Tanzania, kwani ni kielelezo kuwa tayari dunia imeanza kujua vivutio tulivyo navyo, nchini na umuhimu wake duniani, alisema mmoja wa wakurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) huku akisizitiza kuwa hana habari lakini akiahidi kufuatilia ujio huo.

  Bw. Ambani alizaliwa Aprili 19 mwaka 1957, huko Aden (Colony of Eden) sasa Yemen akiwa na uraia wa India. Kwa sasa anaishi Antilia, Mumbai Maharashtra na mke wake Nita Ambani, wakiwa na watoto watatu, Akash, Anant na Isha

  Alisoma Chuo Kikuu cha Mumbai na baadaye Stanford, Uingereza. Kwa sasa ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reliance Industries chini ya Ambani Group of Campanies.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Sahihisho dogo tu Warren Buffet siyo kutoka Mexico yeye ni Mmarekani.............

   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Tusibweteke, kwenye utalii tunahujumiwa na mitandao mbalimbali ya habari nasi hatukanushi: mfano, kunahabari kwenye mtandao inayowaonya watu kuacha kupanda ml. Kili kwa kuwa waliopanda wanawezapata matatizo makubwa ya kiafya kutokana na high altitude, lakini pia wanatahadharishwa kuwa eneo hili malaria ni endemic. Ni vema mamlaka husika zikatafuta namna ya kuosha la sivyo hatufiki mbali.
   
 4. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mukesh Dhirubhai Ambani (born on 19 April 1957) is an Indian business magnate and the chairman and managing director of Reliance Industries,[4] the largest private sector enterprise in India, a Fortune 500 company,[5] and one of the largest private sector conglomerates in the world. His personal stake in Reliance Industries is 48%.[6]
  As of July 2010, he is the richest man in Asia[7] and the fourth richest man in the world with a personal wealth of US$29.0 billion. On 29 October 2007, a strong rally in the Indian stock market and the appreciation of the Indian rupee boosted the market capitalisation of all Reliance group companies, making him for a while the world's richest man,[8] with net worth climbing to US$63.2 billion leaving Bill Gates behind at around $56 billion.[9][10] According to Forbes Magazine forecasts, he is expected to regain the title of the richest man in the world in 2014.[11][12]
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Waandishi wetu!
  Mimi sion faraja yoyote.
   
 6. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkataba wa kampuni ya India iitwayo TATA, inayoua ndugu zetu kule Arusha, nani atakua na nakala yake atuwekee hapa kabla kilio kipya hakijaanza. Maana Lowassa alionekana kuishugulikia sana na yule mwenzetu sote tunamfahamu kwenye kitu pesa.

  Nchi masikini unapotembelewa na 'TAJIRI NAMBA MOJA DUNIANI' tazama kila kona ya nyumba yako na ukajiulize kuna kitu gani cha kuweza kukwapuliwa ukaiifadhi vizuri.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu si ndiye pia mmiliki wa bharti airtel
   
 8. l

  limited JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndio mmiliki wa gapco tanzania na alitaka kununua bt tanzania sijui imefikia wap nafikiri atakwenda hadi magogon maanake pale ni kama soko la ferry au jamaa atamfuata huko
   
 9. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Amboni plastic Tanga na baba yake upo hapo? Unafunga mlango wakati jamaa anafahamu mpaka chumbani kwako!
   
 10. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,771
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  Hapana sie,mmiliki wa bharti airtel ni mtu mwingine kabisa
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kaka umepiga Ikulu... Duh...
   
 12. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  utajiri wake unamsaidia nini na unawasaidia nini watu wengine, unaweza kuwa tajiri wa dunia hii kumbe jehanum inakungoja...mwaminini Yesu, utajiri udumuo, Naam, utajiri wa kweli ni ule unaotoka kwa Bwana, Jiwekeeni hazina zenu mbinguni...hazina yako ilipo ndipo utakapokuwapo na moyo wako. mwenye sikio na asikie.
   
Loading...