Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,547
86,140
Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.

Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.
 
Taji mdogo wangu, za siku Kaka. Well, Hali ni mbaya tena Sana... Cha msingi ni kutotoka ndani na ubane matumizi hii itasaidia Sana.... Mungu akutendee mema katika kila jema Kaka. Njo inbox unipe number Kaka nilipoteza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.
Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.
Ameanzia mbali ila amekuja kuhitimisha kwa kuomba takwimu sahihi ili kujitathmini mahali tulipo.
 
Kwa sasa wewe hakikisha tu kwamba una mahitaji yale ya msingi kabisa, chakula na malazi. Usihangaike kuwa na kila kitu kama ilivyokuwa siku za kawaida.

Ukishaweza kuwa na chakula na familia yako basi, kaa kimya na kuchukua tahadhari kubwa mno dhidi ya ugonjwa. La sivyo utapata ugonjwa na ndani ya wiki 2 utakuwa umekufa.

Usiangalie eti biashara imeyumba, nakwambia bado hakijayumba kitu subiri utaona kuanzia mwezi wa 6 utatafuta ugali tu na ukipata utashukuru Mungu.

Hivyo usilalamike hili ni janga fanya ya msingi tu na kujilinda usipate ugonjwa manake ukipata ndio mbaya kuliko chochote kwa sasa.
 
Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.
Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.
Bila testing tusalimu amri tu kwa corona virus sioni mbadala.
 
Mkuu ombea corona ipite nakuhakikishia Huwezi kupata mshahara km hali itaendelea hivi

Nikustue ujipange usije ukawa unatapanya mali
Mkuu hata uendelee miaka miwili as long kwamba nafanya kazi na naingiza mapato nakosaje mshahara?? sio kwamba natamani ugonjwa uendelee, HAPANA! Ila Dharau zao kwetu watumishi wa Umma zikome kabisa, HESHIMA IFUATE MKONDO WAKE
 
Back
Top Bottom