Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Jamani hiyo lockdown imetangazwa lini? Au Magufuli amehamia Chadema?maana nilisikia kuwa Chadema ndo wanataka lockdown ili watu wafanye fujo wampindue magufuli
Unajua maana ya partial?
 
The legal fraternity has lost five of it's very own in 24 hours
Augustino Ramadhani CJ RTD
Ali Haji Pandu CJ Zanzibar RTD
Alhaji Musa Kwikima AG J RTD
Evod Herman Mmanda
Gaudiosius Ishengoma
 
Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.

Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.
Kwa sasa ni kiza kinene, tena kibaya cha kutisha, wengi wetu bado hatuamini au kupima ukubwa wa tatizo na madhara yanayokuja. endapo hali hii itaendelea kwa niezi mitatu ijayo. Hivi itakuwaje pale ambapo hakiba iliyopo imeisha na hakuna mbadala? Tutajipanga sokoni kugombania vyakula kama nchi za wenzatu waliowahi kupata majanga? Mungu tuepushie mbali hili tatizo.
 
Mkuu hata uendelee miaka miwili as long kwamba nafanya kazi na naingiza mapato nakosaje mshahara?? sio kwamba natamani ugonjwa uendelee, HAPANA! Ila Dharau zao kwetu watumishi wa Umma zikome kabisa
Hujaona mbali mkuu, mambo yanaweza kuwa mabaya hadi watumishi wa umma wakazitishiwa mishahara yao. Hivi ikienda hivi miezi sita hiyo serikali yako itapata wapi pesa za kuwalipeni?

Think big mkuu!!!
 
Hapa nakumbuka kile kibao alichoimba Marjani Rajab 'Shida'.
Shida haina ngoja ngoja, Oohooo Shida
Haina Tajiri masikin, Oohoo shida
Shida eheee ehee, Oohoo shida
 
Anaandika Taji Liundi
Hadi caterers wakubw
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.
Mungu wangu niliwahi waza kuwa dar itajifunga yenyewe ingawa mukulu alisema never!!
From this dar tayari lockdown
 
wewe jamaa bado hujielewi tena una mawazo ya kitoto kabisa,hauna utofauti na mtu anayeombea vita.
Kama serikali inashindwa hata kununua barakoa kwa wananchi watapata wapi hizo milioni 40 za kumpa kila mtumishi.
tumia akili kujiongeza
Mkuu we tulia hali ikifika huko we utakuwa ushakufa kabisa! Saivi Serikali inatoa Mikopo hadi 40M bila riba kwa watumishi so najiandaa kisaikolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaona mbali mkuu, mambo yanaweza kuwa mabaya hadi watumishi wa umma wakazitishiwa mishahara yao. Hivi ikienda hivi miezi sita hiyo serikali yako itapata wapi pesa za kuwalipeni?

Think big mkuu!!!
Asante kwa maoni yako
 
wewe jamaa bado hujielewi tena una mawazo ya kitoto kabisa,hauna utofauti na mtu anayeombea vita.
Kama serikali inashindwa hata kununua barakoa kwa wananchi watapata wapi hizo milioni 40 za kumpa kila mtumishi.
tumia akili kujiongeza

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla hujakurupuka kureply soma vizuri utajiaibisha "GREAT THINKER" wapi nimesema serikali itakopesha 40M kwa kila mwananchi kama imeshindwa kutoa 50M kwa kila kijiji?
 
Kabla hujakurupuka kureply soma vizuri utajiaibisha "GREAT THINKER" wapi nimesema serikali itakopesha 40M kwa kila mwananchi kama imeshindwa kutoa 50M kwa kila kijiji?
Aiseeee isaidie hiki kilimo
 
Attachments

  • IMG-20200428-WA0057.jpg
    IMG-20200428-WA0057.jpg
    46 KB · Views: 17
Back
Top Bottom