Taja wamiliki wa CCM na CHADEMA

ccm ni chama cha wakulima na wafanyakazi wa tanzania,hao ndio wamiliki halali wa ccm.
 
Si halali kisheria na kiitikadi kuwa na mawazo kwamba mtu au watu fulani wanamiliki chama fulani cha Siasa.
Neno mwafaka ni nani mweny ukulitimba wa madaraka au mamlaka katika chama cha siasa.
CDM ilianzishwa na Mzee Mtei kwa pesa yake ya Mfukoni. Mazee huyu hakupitisha Bakuli la Matonya kuchangisha fedha, michango imekuja baadaye sana. hata hivyo Mzee Mtei bad si mmiliki wa CDM:tape2:

CCM imetokana na TANU na ASP vyama vyote viwili vina hitsoria ndefu sana yenye kuwaunganisha wazalendo wengi wa nchi hii kama si wananchi wote. Hata hivyo CCM sasa hivi si chama cha Wazalendo wa Tanzania tena, ni chama cha Mafisi wachache wenye kila hila ya kudhurumu Utu wa Mtanzania.
Kuna kundi la watu ndnai ya CCM wanahodhi madaraka na kujiweka juu ya sheria, kimtazamo wanaonekana ndiyo wamiliki wa CCM lakini ukweli ni kwamba si wamiliki wa CCM hawajawahi na hawatakuwa. Watu hawa wachache siku zao za mamlaka ndani ya CCM zinahesabika. Ndiyo maana kila uchaguzi wa ndani wa CCM ufanyikapo kuna rushwa za kukata na Nyengo ili kutwa kura sababu ni kwamba Fedha nidyo inayomili CCM siyo mtu au kundi la watu wachache.

Malecela ni mmoja wa watu waliokuwa na nguvu sana ndani ya CCM, yuko wapi sasa?
Fikiria kaangushwa na Kipimo cha Matusi Lusinde kule Mtera.

Vyma vya siasa vina watu wenye nguvu sana ndani yake lakini si wamiliki.

Wamiliki wa vyama ni wanachama wa vyama hivyo.
Nimetafakari muda mrefu sana juu ya wamiliki wa vyama hivi. Kati ya vyama hivyo kuna hatari ya kuwa wakiondoka baadhi ya viongozi chama kinafutika.
 
Back
Top Bottom