Wana jf hebu tuanze kuijadili katiba iliyopo kama kweli tunaijua. Maana wengi wanasema tu katiba mpya wakati hata iliyopo hawajui. Katiba ya marekani imetungwa 1786 na zimefanyika amendment 26 tu ya mwisho ilikuwa 1992. Je katiba yetu inamapungufu yapi mpaka tuifanyie overwhole. Katiba ikibadishwa yote na sheria lazima zibadilike so sio jambo just over night. Let us see if we really know our katiba.
1. Rais apunguziwe madaraka ili baadhi anaowateua wathibitidhwe na Bunge!
2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe huru, ie cmposition ya wajumbe wa tume ijumuishe pia wapinzani.
3. Tanzania sio tena nchi ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuwa njia kuu za uchumi zote haziko mikononi mwa Serikali. Kwahiyo Katiba ifanyiwe marekebisho kuondoa kipengele hicho!
4. Katiba ifanyiwe marekebisho iendane na Katiba ya Zanzibar, km kuondoa cheo cha uwaziri kiongozi!
5. Viti maalum vya ubunge na udiwani viondolewe, havina kazi yoyote.
6. Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Wabunge, kwa kuwa hao wabunge hawawakilishi chochote.
7. Matokeo ya urais yawe challenged mahakamani, kwa hiyo kile kipengele kwamba Tume ikishatangaza matokeo basi hakuna mahakama yoyote yenye uwezo wa kuyachunguza kiondolewe!
8. Rais asiwe na uwezo wa kubadili Wizara mara kwa mara, idadi ya wizara ziwekwe kwenye Katiba na kama ataona kuna haja ya kuziongeza Bunge liridhie. Hii itapunguza Rais kubadili Wizara kila mara, kwa kutaka kuwapatia maswahiba wake vyeo! Pia Wizara ziwe chache ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.
9. Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana kazi waondolewe na badala yake wabaki Wakurufenzi watendaji wa Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya!
10. Muundo wa Muungano uwe wa Serikali tatu!
11. Kuwe na equal distribution ya resources badala ya kuconcetrate tu kujenga Dar es Salaam na baadhi ya mikoa. Kwa hiyo iwekwe mechanism kwenye Katiba, eg Swrikali za Majimbo zenye baadhi ya mamlaka juu ya resouces zilizopo maeneo yao.
13. Mgombea binafsi aruhusiwe Kikatiba!
14......
Sio lazima kuijua katiba, maana imeandikwa kisheriasheria hivi na inatuboa most of us..cha msingi ni kwa vitu ambavyo tunataka vifanyike ambavyo havipo sasa kwa sasa viwe vested kisheria kwene katiba. Thats all.
???????kwanza katiba kama katiba ni sheria (ndo sheria mama) sas we unategemeaje sheria mama ibadilike halaf ndogondogo zibakie kama zilivyo??
14.Isiwe lazima kwa waziri kua mbunge.
15. Isiwe lazima kua waziri lazima atoke chama kinachokua madarakani manake hii inawanyima wanbunge wa upinzani fursa ya uwaziri hata kama wangekua wanauwezo wa kutoa huduma kwa ufanisi sana na kuwapa wale wa chama tawala hata kama hawana uwezo wakiutendaji. Ndo sababu tunasema wathibitishwe na bunge.
16. Katiba iweke mandate ya kuweza kuwa evaluate wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya periodically.Sio jitu linakaatu madarakani miaka ishirini na halijafanya chochote na hakuna wakuliuliza.
17.Iweke wazi kikomo cha ubunge na ipaunguze muda wa ku staaf kisheria (62) ya sasa ni ming inasababisha ukosef wa ajira.
18......
ni kodi gani ambayo wewe unalipa waziri halipi?18. Ikija kwenye suala la kulipa kodi wote tuwe sawa, sio kwamba kodi inalipwa na sisi watu wa chini (pangu pakavu) ila mawaziri, wabunge, makamu na rais mwenyewe hawalipi kodi yoyote ktk mapato yao
wakulima na wamachinga na wavuvi na mama ntilie na waponda kokoto na walinzi wa kimasai na wapika pombe na waganga wa kienyeji hawalipi kodi!
19. abolish death penalty.....
20. legalize marijuana
21. .....
mkuu.... nimekupata... lakini haya mateja yataendelea tusumbua tuu... yawekewe kiwango cha dozi na sehemu muhimu and public private za kuvutia bangi zao.... huu moshi watu wengi muhimu wanatumia hata ma prof. wengi wanakula hii mihadharati ikiwasaidia kutoa lecture
Tukiacha hiyo kitu iendelee itaharibu mno watoto, esp wanafunzi, wanakuwa kama mazezeta na shule zinakuwa hazipandi!
ni kodi gani ambayo wewe unalipa waziri halipi?
news flash, in Tanzania the brunt of the tax burden befalls the higher earners.
wakulima na wamachinga na wavuvi na mama ntilie na waponda kokoto na walinzi wa kimasai na wapika pombe na waganga wa kienyeji hawalipi kodi!