Taja mapungufu ya Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taja mapungufu ya Katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Zhu, Dec 18, 2010.

 1. Z

  Zhu Senior Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jf hebu tuanze kuijadili katiba iliyopo kama kweli tunaijua. Maana wengi wanasema tu katiba mpya wakati hata iliyopo hawajui. Katiba ya marekani imetungwa 1786 na zimefanyika amendment 26 tu ya mwisho ilikuwa 1992. Je katiba yetu inamapungufu yapi mpaka tuifanyie overwhole. Katiba ikibadishwa yote na sheria lazima zibadilike so sio jambo just over night. Let us see if we really know our katiba.
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni 'overhaul' siyo 'overwhole'. Rekebisha ili thread yako ipate heshima na kuchangiwa.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Rais apunguziwe madaraka ili baadhi anaowateua wathibitidhwe na Bunge!
  2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe huru, ie cmposition ya wajumbe wa tume ijumuishe pia wapinzani.
  3. Tanzania sio tena nchi ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuwa njia kuu za uchumi zote haziko mikononi mwa Serikali. Kwahiyo Katiba ifanyiwe marekebisho kuondoa kipengele hicho!
  4. Katiba ifanyiwe marekebisho iendane na Katiba ya Zanzibar, km kuondoa cheo cha uwaziri kiongozi!
  5. Viti maalum vya ubunge na udiwani viondolewe, havina kazi yoyote.
  6. Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Wabunge, kwa kuwa hao wabunge hawawakilishi chochote.
  7. Matokeo ya urais yawe challenged mahakamani, kwa hiyo kile kipengele kwamba Tume ikishatangaza matokeo basi hakuna mahakama yoyote yenye uwezo wa kuyachunguza kiondolewe!
  8. Rais asiwe na uwezo wa kubadili Wizara mara kwa mara, idadi ya wizara ziwekwe kwenye Katiba na kama ataona kuna haja ya kuziongeza Bunge liridhie. Hii itapunguza Rais kubadili Wizara kila mara, kwa kutaka kuwapatia maswahiba wake vyeo! Pia Wizara ziwe chache ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.
  9. Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana kazi waondolewe na badala yake wabaki Wakurufenzi watendaji wa Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya!
  10. Muundo wa Muungano uwe wa Serikali tatu!
  11. Kuwe na equal distribution ya resources badala ya kuconcetrate tu kujenga Dar es Salaam na baadhi ya mikoa. Kwa hiyo iwekwe mechanism kwenye Katiba, eg Swrikali za Majimbo zenye baadhi ya mamlaka juu ya resouces zilizopo maeneo yao.
  13. Mgombea binafsi aruhusiwe Kikatiba!
  14...
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sio lazima kuijua katiba, maana imeandikwa kisheriasheria hivi na inatuboa most of us..cha msingi ni kwa vitu ambavyo tunataka vifanyike ambavyo havipo sasa kwa sasa viwe vested kisheria kwene katiba. Thats all.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kwa kuanzia mi ningesema vyeo vyote vya kuteuana vifutwe, pengine except Ministers au 'Secretaries', vyovyote vile mtavyowaita. Vyeo na kazi serikalini watu wapewe based on merits baada ya kuwa wameomba. Huko kwene vyama vyenu uchwara teuaneni tani yenu, lakini pale ninapotumbukiza kodi yangu, HAPANA.
   
 6. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,582
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Kwa ufupi tunataka katiba ya wananchi, inayosimamia na kutoa mamlaka makubwa kwa wananchi na siyo katiba tuliyo nayo sasa ambayo ni ya serikali na Rais. Serikali na Rais wana nafasi kubwa sana ya kuamua chochote wanachotaka. Ndiyo maana inastahili kuandikwa upya siyo kuirekebisha kwa sababu tatizo siyo content bali msingi wa hiyo katiba kuwa ipo kwaajili ya kuwapa uhuru watawala kuamua chochote wananchotaka kufanya kwaajili ya wananchi badala ya kuwa katiba ya wananchi inayowaelekeza viongozi na serikali nini cha kufanya kwaajili ya ustawi wa wananchi.
   
 7. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya niyatakayo yawemo ndani ya katiba mpya 1-Katiba iainishe wazi wazi uwepo wa TANGANYIKA kama TAIFA; Na MAMLAKA zake kama taifa ziwepo! 2- Mikoa ipunguzwe iwe Majimbo na Wakuu wa majimbo wasiteuliwe bali wachaguliwe ili wawajibike kwa Majimbo husika 3-Tume ya uchaguzi ishirikishe wadau wote na mwenyekiti wa tume akubalike na wadau wote.4-Iwepo sera ya taifa inayo bainisha TANGANYIKA TUITAKAYO! Na wanasiasa Wanadi jinsi ya kufikia huko.......5-Mipaka ya Dini/imani iwekwe bayana kuwadhihirishia wazi wazi Kwamba hiki ni mwiko kwao na hiki ruksa ili wasivuke mipaka!..............
   
 8. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  14.Isiwe lazima kwa waziri kua mbunge.
  15. Isiwe lazima kua waziri lazima atoke chama kinachokua madarakani manake hii inawanyima wanbunge wa upinzani fursa ya uwaziri hata kama wangekua wanauwezo wa kutoa huduma kwa ufanisi sana na kuwapa wale wa chama tawala hata kama hawana uwezo wakiutendaji. Ndo sababu tunasema wathibitishwe na bunge.
  16. Katiba iweke mandate ya kuweza kuwa evaluate wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya periodically.Sio jitu linakaatu madarakani miaka ishirini na halijafanya chochote na hakuna wakuliuliza.
  17.Iweke wazi kikomo cha ubunge na ipaunguze muda wa ku staaf kisheria (62) ya sasa ni ming inasababisha ukosef wa ajira.
  18......
   
 9. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kwanza katiba kama katiba ni sheria (ndo sheria mama) sas we unategemeaje sheria mama ibadilike halaf ndogondogo zibakie kama zilivyo??
   
 10. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #10
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asiyejua sio jambo la overnight ni nani lakini? Utambue mabadiliko yote lazima yaanzie na katiba ambayo ni ndio sheria mama. Nyingine(statutes) zitafanyiwa mabadiliko na Bunge kuendana na katiba mpya. Na hiyo sio big deal hata kidogo! Kenya ndio wanachofanya kwa wakati huu. Mbona watanzania waoga hivi? Tatizo hapo ni nini? Nina wasiwasi hata katiba yenyewe huijui ndio maana unailinganisha na ya Marekani.
  Hakuna sifa kuibadili au kuifanyia marekebisho mara ngapi. Wako kimya kwa sababu iko poa kwa upeo wao. Issue hapa ni je inafaa kulingana na mahitaji ya wakati tulionao? Kwa mfumo wa chama kimoja iko poa sana! Natumaini umeona mapungufu yake machache tu kwenye uchaguzi uliopita. Tusiache mpaka wakina Ocampo waje baada ya moto kuwaka ndo tuzinduke! Amka sasa na uanze kuisoma katiba yako!
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ???????
   
 12. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  18. Ikija kwenye suala la kulipa kodi wote tuwe sawa, sio kwamba kodi inalipwa na sisi watu wa chini (pangu pakavu) ila mawaziri, wabunge, makamu na rais mwenyewe hawalipi kodi yoyote ktk mapato yao ya mshahara na allowance. Me nazan sbb hawalipi kodi ndo maana wanatoa sana misamaha ya kodi kijinga jinga

  19....
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  19. abolish death penalty.....
  20. legalize marijuana
  21. .....
   
 14. T

  Taso JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  ni kodi gani ambayo wewe unalipa waziri halipi?

  news flash, in Tanzania the brunt of the tax burden befalls the higher earners.

  wakulima na wamachinga na wavuvi na mama ntilie na waponda kokoto na walinzi wa kimasai na wapika pombe na waganga wa kienyeji hawalipi kodi!
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  je sheria inawaruhusu kutokulipa kodi? au ni inefficiency na mapungufu ya system ya Taxpayer Identification..... hawa uliowataja wana adress...? business licenses.... secured identity...... au serikali ina record zao?.... mkuu.. basi afadhali hawa wanatumia loophole ya informal earners kuliko licensed and registered business taycoons whom intentionally evade tax ..... uliowataja wanahitaji elimu kidogo tu na serikali kuwa makini
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Dec 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye 20 nafikiri umepitiwa ndugu!
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu.... nimekupata... lakini haya mateja yataendelea tusumbua tuu... yawekewe kiwango cha dozi na sehemu muhimu and public private za kuvutia bangi zao.... huu moshi watu wengi muhimu wanatumia hata ma prof. wengi wanakula hii mihadharati ikiwasaidia kutoa lecture
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Dec 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tukiacha hiyo kitu iendelee itaharibu mno watoto, esp wanafunzi, wanakuwa kama mazezeta na shule zinakuwa hazipandi!
   
 19. L

  LAT JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ninakiri kwa hilo kwani mfumo wa nchi yetu isiyo hata na vitambulisho vya uraia hauwezi ku control hii situation ninayozungumzia... hivyo haitekelezeki....

  21. empowerment ya natives especially on natural resources..... iwekwe wazi na katiba kma sheria mama ya resources zetu na uwezeshwaji na siyo visheria vinavyotungwa tungwa tu na kina ngeleja na kubadilishwa pale kina barrick and anglo wakilalamika
  22. sheria zinazounda state organs zibadilishwe na polisi isiwe jeshi bali iwe ni taasisi ya kutoa huduma za usalama na ulinzi wa raia... mfano badala ya kuwa Tanzania Police Force iwe Tanzania Police Service... South Africa wana SAPS na its one of the best policing organs in the world...policing does not mean using force... using force will be the last resort like ...if the pain persist see a medical doctor
   
 20. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Pay as you earn na income tax,kifupi mshahara wao upo full haukatwi kitu
   
Loading...