‘Taja jina la bibi mzaa mama wa Yesu Kristu!’

‘Taja jina la bibi mzaa mama wa Yesu Kristu!’

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Alhamisi, Septemba 26, 2013 06:22 Na Joe Beda

MIAKA zaidi ya 10 iliyopita nilisoma katuni moja kwenye gazeti la SANI ambayo huenda ndiyo katuni yangu bora niliyowahi kuiona kwani ilinifikirisha na kunichekesha kuliko nyingine nyingi. Kipindi hicho kulikuwa na vuguvugu kubwa la haki za mtoto na hasa mtoto wa kike, huku kukiwa na wimbi la walimu kadhaa wa kiume kushitakiwa mahakamani kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike.

Sijui kama suala hilo kwa sasa limekwisha, limepungua au limeacha kuripotiwa kwa sababu ya kupitwa na wakati, lakini inavyoonekana hali kwa sasa si sawa na kipindi kile.

Katuni ile ilimwonyesha mtoto wa kike akiwa amelala chini huku mwalimu wa kiume akimtandika bakora mfululizo na kumuuliza swali hili: “Nakuuliza, Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 9 Desemba mwaka 1961, ilikuwa juma ngapi?”

Mchoraji wa katuni ile aliiwekea maandishi ya utangulizi yaliyosemeka; ‘ukiona mwalimu anauliza swali hili, ujue ana lake jambo!’ Hakika lilikuwapo jambo kati ya binti huyo, mwalimu, na swali lile la ‘kizushi’.

Naam, nilicheka. Lakini nikajiuliza iwapo swali hilo ningeulizwa mimi ningekuwa na jibu? Tarehe ya Uhuru wa Tanganyika na hata Uhuru wa nchi nyingine kadhaa za Afrika tumekuwa tukikaririshwa miaka nenda rudi, lakini siku haswa ya tukio! Hapana.

Kumbukumbu za katuni hiyo zikanirudia majuzi baada ya watu wanaoaminika kuwa ni magaidi (wana mgambo) wa kundi la Al-Shaabab kuvamia mlolongo wa maduka ya Westgate Mall jijini Nairobi.

Mashuhuda walionusurika kuuawa kwenye tukio hilo, wameviambia vyombo mbalimbali vya habari kwamba magaidi hao walikuwa wakijitahidi kuwatenganisha ‘walengwa’ wao na ‘wenzao’ kwa kuwauliza jina la mama wa Mtume Mohammad (SAW)!

Sina uhakika na ugumu au wepesi wa swali hilo kwa ‘muumini’ mzuri, lakini nilicho na uhakika nacho ni kwamba, hata swali jepesi kama ‘jina lako nani’ unaweza kushindwa kulijibu kwa wakati ukiwa umeelekezewa mtutu wa bunduki na mtu asiye na masihara hata kidogo!

Mtu aliyeamua kwamba siku hiyo ndiyo siku yake ya kufa, labda itokee bahati mbaya, ni mtu hatari sana. Fikiria, tayari umeshuhudia watu wanne au watano wakipigwa risasi mbele yako baada ya kuulizwa swali, inafika zamu yako na kuulizwa ‘jina lako nani?’ hakika unaweza kushindwa kujibu!

Nikafikiria hivi kuna ‘waamini’ wenzangu wangapi wanaoweza kuulizwa ghafla na kutaja jina la bibi yake na Yesu mzaa mama? Tena hilo linaweza kuwa jepesi, lakini ni nani analijua jina la bibi yake Yesu mzaa baba mlezi?

Kwa kumbukumbu za haraka, nikakumbuka jina la Anna (Mtakatifu Anna) kuwa ndilo jina la mama yake Bikira Maria (bibi yake Yesu upande wa mama), lakini upande wa baba mlezi! Hatari.

Sasa hapo hakukuwa na shinikizo lolote, je ningekuwa nimeelekezewa bunduki? Hakika nikaikumbuka ile katuni kwamba ukiona mtu anauliza swali kwa mtindo huo, ujue ana lake jambo.

Nikawaza kuwa kama ingetokea bahati mbaya nikawa mmoja wa waathirika wa tukio la Nairobi, swali la haraka ambalo ningewajibu jamaa wale bila kusita ni kama wangeniuliza jina la mke (mkubwa) wa Mtume (SAW).

Haya mambo nikuomba Mungu yasikutokee. Ni mambo ya kusikitisha sana na hata kwa fikra za kawaida unashindwa kuelewa chuki hizi zinapandikizwa miongoni mwa binadamu kwa lengo gani?

Swali gumu zaidi ni jinsi gani ya kuzuia matukio ya kishenzi kama haya kutokea katika dunia hii ya utandawazi.

Jeshi la Polisi nchini limesema kwamba liko tayari, eti limejiandaa kuyakabili matukio kama haya; ni jambo la kushukuru kama kweli tuko tayari, lakini kikubwa ni kuyakinga yasitokee.

Ni hapo ndipo Watanzania wote tunapaswa kushirikiana. Ulinzi na usalama wetu unaanzia kwetu wenyewe, kwa kutoa taarifa kwa viongozi kuhusu mienendo ya kutia shaka ya kundi la watu au mtu yeyote unayemfahamu au usiyemfahamu.

Ipo tabia yetu ya kutowaamini watendaji kadhaa serikalini kwamba unaweza kutoa taarifa, kumbe unayemtaarifu anahusika au kuhusiana na kundi hilo matokeo yake usalama wako ukawa hatarini.

Sasa ushauri wangu katika jambo hilo ni kwamba, mtafute kiongozi unayemwamini hata wa chama cha upinzani, mtaarifu suala hilo na ninaamini yeye hataogopa kulipeleka serikalini; au basi mdokezee mwandishi wa habari unayemwamini kwani nao katika tasnia yao ni ‘risk takers’.

Lakini serikali nayo inapaswa kuwa makini. Iweke mtandao mpana wa kugundua uingizwaji nchini wa ‘fedha chafu’ au hata kama ni safi, lakini zinapoingizwa kwa wingi kwa kundi au mtu asiyeaminika, ni vyema zikazuiwa hadi itakapofahamika kazi ya fedha hizo nchini ni ipi hasa.

Ni wazi maandalizi ya shambulio kama hili la Nairobi yaligharimu fedha nyingi. Sasa. Fedha hizo ziliingizwaje nchini? Zilipitia benki gani? Zilikwenda kwa nani?

Tusiruhusu fedha chafu kufika mikononi mwa watu ambao mienendo yao inatia shaka.

Nimalizie kwa kuwakumbusha ‘wazee’ wenzangu muziki mmoja wa miaka ya 1970 uliokuwa na maneno ‘wanyama wabaya maana yake, sio simba wala si tembo, ni wanadamu wenye choyo…’

Nawasilisha
0684 419 506

Mwandishi kajitahidi sana, ila changamoto bado iko kwenye huu ushauri alioutoa. Nitatoa mfano:
Mwanzoni mwa mwaka huu, gazeti la mtanzania liliripoti uwepo wa chuo ambacho kinadhaniwa kutoa mafunzo ya kigaidi kisiwani Ukerewe. Mbunge wa huko Mh. Machemli (Chadema) alipotafanya mahojiano na mwandishi wa habari ile aliahidi kulifikisha swala la chuo hicho serikalini ikiwa na pamoja kutaka mitaala ya chuo hicho ikaguliwe. Haijulikani ni nini kilimtisha huyu mbunge wa upinzani (anayeaminiwa na mwandishi) kiasi kwamba ndani ya juma moja alikuwa ameyakana maneno yake licha ya kujua kuwa mwandishi alimrekodi. Wananchi wa Ukerewe bado wanahamu ya kujua mtaala wa hicho chuo, sifa za kujiunga na baada ya kozi wahitimu watafanya kazi gani. Mbunge alitishwa akatishika. Kwa hiyo kusema wabunge wa upinzani wanaweza wakawa msaada kwenye mambo ya usalama sidhani kama ni kweli.
 
Hata mi nakumbuka jina la Bibi wa Yesu kwa upande wa mama ni Anna, ila kwa upande wa baba sikumbuki kuwahi kusikia..
 
Alhamisi, Septemba 26, 2013 06:22 Na Joe Beda

MIAKA zaidi ya 10 iliyopita nilisoma katuni moja kwenye gazeti la SANI ambayo huenda ndiyo katuni yangu bora niliyowahi kuiona kwani ilinifikirisha na kunichekesha kuliko nyingine nyingi. Kipindi hicho kulikuwa na vuguvugu kubwa la haki za mtoto na hasa mtoto wa kike, huku kukiwa na wimbi la walimu kadhaa wa kiume kushitakiwa mahakamani kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike.

Sijui kama suala hilo kwa sasa limekwisha, limepungua au limeacha kuripotiwa kwa sababu ya kupitwa na wakati, lakini inavyoonekana hali kwa sasa si sawa na kipindi kile.

Katuni ile ilimwonyesha mtoto wa kike akiwa amelala chini huku mwalimu wa kiume akimtandika bakora mfululizo na kumuuliza swali hili: "Nakuuliza, Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 9 Desemba mwaka 1961, ilikuwa juma ngapi?"

Mchoraji wa katuni ile aliiwekea maandishi ya utangulizi yaliyosemeka; ‘ukiona mwalimu anauliza swali hili, ujue ana lake jambo!' Hakika lilikuwapo jambo kati ya binti huyo, mwalimu, na swali lile la ‘kizushi'.

Naam, nilicheka. Lakini nikajiuliza iwapo swali hilo ningeulizwa mimi ningekuwa na jibu? Tarehe ya Uhuru wa Tanganyika na hata Uhuru wa nchi nyingine kadhaa za Afrika tumekuwa tukikaririshwa miaka nenda rudi, lakini siku haswa ya tukio! Hapana.

Kumbukumbu za katuni hiyo zikanirudia majuzi baada ya watu wanaoaminika kuwa ni magaidi (wana mgambo) wa kundi la Al-Shaabab kuvamia mlolongo wa maduka ya Westgate Mall jijini Nairobi.

Mashuhuda walionusurika kuuawa kwenye tukio hilo, wameviambia vyombo mbalimbali vya habari kwamba magaidi hao walikuwa wakijitahidi kuwatenganisha ‘walengwa' wao na ‘wenzao' kwa kuwauliza jina la mama wa Mtume Mohammad (SAW)!

Sina uhakika na ugumu au wepesi wa swali hilo kwa ‘muumini' mzuri, lakini nilicho na uhakika nacho ni kwamba, hata swali jepesi kama ‘jina lako nani' unaweza kushindwa kulijibu kwa wakati ukiwa umeelekezewa mtutu wa bunduki na mtu asiye na masihara hata kidogo!

Mtu aliyeamua kwamba siku hiyo ndiyo siku yake ya kufa, labda itokee bahati mbaya, ni mtu hatari sana. Fikiria, tayari umeshuhudia watu wanne au watano wakipigwa risasi mbele yako baada ya kuulizwa swali, inafika zamu yako na kuulizwa ‘jina lako nani?' hakika unaweza kushindwa kujibu!

Nikafikiria hivi kuna ‘waamini' wenzangu wangapi wanaoweza kuulizwa ghafla na kutaja jina la bibi yake na Yesu mzaa mama? Tena hilo linaweza kuwa jepesi, lakini ni nani analijua jina la bibi yake Yesu mzaa baba mlezi?

Kwa kumbukumbu za haraka, nikakumbuka jina la Anna (Mtakatifu Anna) kuwa ndilo jina la mama yake Bikira Maria (bibi yake Yesu upande wa mama), lakini upande wa baba mlezi! Hatari.

Sasa hapo hakukuwa na shinikizo lolote, je ningekuwa nimeelekezewa bunduki? Hakika nikaikumbuka ile katuni kwamba ukiona mtu anauliza swali kwa mtindo huo, ujue ana lake jambo.

Nikawaza kuwa kama ingetokea bahati mbaya nikawa mmoja wa waathirika wa tukio la Nairobi, swali la haraka ambalo ningewajibu jamaa wale bila kusita ni kama wangeniuliza jina la mke (mkubwa) wa Mtume (SAW).

Haya mambo nikuomba Mungu yasikutokee. Ni mambo ya kusikitisha sana na hata kwa fikra za kawaida unashindwa kuelewa chuki hizi zinapandikizwa miongoni mwa binadamu kwa lengo gani?

Swali gumu zaidi ni jinsi gani ya kuzuia matukio ya kishenzi kama haya kutokea katika dunia hii ya utandawazi.

Jeshi la Polisi nchini limesema kwamba liko tayari, eti limejiandaa kuyakabili matukio kama haya; ni jambo la kushukuru kama kweli tuko tayari, lakini kikubwa ni kuyakinga yasitokee.

Ni hapo ndipo Watanzania wote tunapaswa kushirikiana. Ulinzi na usalama wetu unaanzia kwetu wenyewe, kwa kutoa taarifa kwa viongozi kuhusu mienendo ya kutia shaka ya kundi la watu au mtu yeyote unayemfahamu au usiyemfahamu.

Ipo tabia yetu ya kutowaamini watendaji kadhaa serikalini kwamba unaweza kutoa taarifa, kumbe unayemtaarifu anahusika au kuhusiana na kundi hilo matokeo yake usalama wako ukawa hatarini.

Sasa ushauri wangu katika jambo hilo ni kwamba, mtafute kiongozi unayemwamini hata wa chama cha upinzani, mtaarifu suala hilo na ninaamini yeye hataogopa kulipeleka serikalini; au basi mdokezee mwandishi wa habari unayemwamini kwani nao katika tasnia yao ni ‘risk takers'.

Lakini serikali nayo inapaswa kuwa makini. Iweke mtandao mpana wa kugundua uingizwaji nchini wa ‘fedha chafu' au hata kama ni safi, lakini zinapoingizwa kwa wingi kwa kundi au mtu asiyeaminika, ni vyema zikazuiwa hadi itakapofahamika kazi ya fedha hizo nchini ni ipi hasa.

Ni wazi maandalizi ya shambulio kama hili la Nairobi yaligharimu fedha nyingi. Sasa. Fedha hizo ziliingizwaje nchini? Zilipitia benki gani? Zilikwenda kwa nani?

Tusiruhusu fedha chafu kufika mikononi mwa watu ambao mienendo yao inatia shaka.

Nimalizie kwa kuwakumbusha ‘wazee' wenzangu muziki mmoja wa miaka ya 1970 uliokuwa na maneno ‘wanyama wabaya maana yake, sio simba wala si tembo, ni wanadamu wenye choyo…'

Nawasilisha
0684 419 506

Mkuu umeikopi mahali hii kitu? Mpe credit zake mwandishi, pia kama ni wewe pokea Pongezi zangu!
 
Mkuu nngu007, umejitahidi kuonyesha ulichokusudia na asante kwa kutimiza wajibu wako wa msingi.
Kweli sio utani hizi shughuli za kigaidi zinahitaji pesa nyingi kuzi-organize na sio rahisi mtu aliyefanya biashara halali ya kuuza viazi, kahawa, maharage nk akaweka pesa zake huko. Mara nyingi pesa chafu kama za madawa ya kulevya, ujangiri, uharamia na vitu kama hivyo ndio zinaunganishwa na hao maajenti wa nje then kuziingiza kwenye mfumo wa kawaida.
Ukweli mwingine unaweza kuwa hali halisi iliyopo Tanzania sasa hasa kwenye miji asilimia kubwa ya 'matajiri' wanamiliki pesa zisizo na maelezo sahihi na kibaya zaidi wanaozimiliki sio watu sahihi pia. Lakini kwa sababu kuwa na pesa ndio ujanja basi wengi tunaona sawa tu, tuombee Mungu hawa watu wasituelekeze hasira zao maana ni sawa na kichaa kuwa na panga kali au AK47.
 
Baada ya tukio la Westgate sisi watanzania tunazungumzia sana ulinzi na umakini. Lakini cha ajabu sijaona tangazo lolote lenye kuonesha namba ambazo tutapiga endapo tutaona/kugundua jambo lisilo la kawaida.
Nauliza: Nikiona kikundi cha watu wanne wamebebamifuko ya salfati iliyotunatuna wakiingia kwenye gesti ya mtaani kwetu nitaripotije kwa haraka kutumia mawasiliano ya simu?
 
Ukiwa katika hatari ni ngumu sana kutabiri utakachokifanya, ila nahisi ningeshikwa na hasira kuu na pengine ningejikuta namwambia niulize jina la mama yake Yesu ni si hilo unaloniuliza. Pale ningejua tu ni mwisho wangu umekaribia na singekuwa na haja ya kujifanya mpole kwao, bora niondoke kwa staili hiyo kwa sababu hata ningejua jibu la swali walilouliza nikalijibu, ningeishi nikijua mimi ni msaliti, nimeshindwa kutetea imani yangu. Mungu tusaidie tuwe imara katika majaribu na tusihofishwe na waovu tukakukana
 
Joachim and Anne were the parents of Mary and the grandparents of Jesus.
The name "Hannah" means grace. In Galilee, where she lived, Mary's mother was probably called "Hannah" even though we know her as Saint Anne. So, if you are named "Hannah" or "Anne" you are named after the mother of Our Blessed Mother.
It was in the womb of Saint Anne that Mary was immaculately conceived. From the first instant of her life, she was in a state of grace and free from all stain of Original Sin. It was her parents, Anne and Joachim that raised her to be faithful to God's word and remain free of sin.Anne is the patron of Christian mothers, and Joachim the patron of fathers. They were given the great honour and responsibility of raising Mary to be the Mother of God, and can help mothers and fathers today to raise their children to love and follow God too.

Joachim the husband of Saint Anne and the father of the Blessed Virgin Mary, belonged to the tribe of Judah and the house of David. Tradition tells us that he and his wife came from Galilee. They lived in Nazareth and there the Blessed Mother lived.
Anne and Joachim were childless for many years. At the time that they lived, this was considered to be a punishment of God among the Jews. They continued to pray and finally God answered their prayers when the Virgin Mary was born. This was their greatest honour, to be the parent's of Mary, the Mother of God and the Grandparents of Jesus.
The couple offered their little daughter to God in the Temple. As a young girl, she spent time in service to the Temple. working and learning with other girls. But it was problbly her parents who taught her to read, and certainly Joachim and Anne who taught her to love and follow God's word and to know and understand the Scriptures.
When the Angel Gabriel came to her at the Annunciation, Mary knew the prophecies of Jesus' life and death. She knew the full extent of the honour and pain she would experience when she gave her 'fiat.'Mary loved her mother and father. In this she is a beautiful example for children. Joachim and Anne loved their daughter and followed God's plan in raising her. In this, they are a shining example and intercessors for Christian parents.

Saints Joachim and Anne, both of the tribe of Judah of the royal house of David and venerated by the Church as the parents of the Blessed Virgin Mary, who was probably their only child.
There is another Mary mentioned in the Gospels as being the 'sister' of the Mother of God, but this was probably her cousin. Two Marys in one family stretches reason and this was a customary way of designating relatives in the East.
Saint Anne has been honored from early Christian times. Churches were dedicated in her honor, and the Fathers, expecially of the Eastern Churches, loved to speak both of her sanctity and her privileges of being chosen to raise the Mother of God.
Saint Joachim has also been honored from the beginning in the Churches of the East, and since the 6th century, public devotion to him has been observed in all countires. However, we know little about the lives of either Joachim or Anne, since the Gospels are silent on this account.
Some traditions grounded in very old testimonies, tells us that Saints Joachim and Anne in their old age came from Galilee to settle in Jerusalem. As a childless couple, they may have simply wished to spend their old age close to the Temple. But God, in his Wisdom and Mercy, granted them a child, and Mary was born and raised in Jerusalem.The sainted couple is often depicted with Mary and holding a book of Scriptures, teaching their daughter to read. A church was built in the 4th century, possibly by Saint Helena, on the reputed site of Saint Joachim and Anne's house in Jerusalem.
Wazazi wa Bikra Maria ni Anna na Joachim!
 
Bibi wa babake yesu ni mama Maria Nyerere.

Kashfa kwa imani za dini huwa na sura tofauti,
Kama unatak hata sisi tunajua kukufuru sema tu tumepata mafunzo sahii ya MUNGU MWENYE NGUVU
 
Ni kweli bibi yake yesu jina lake ni hannah na babu yake nadhani jina lake ni Joachim [ mtaniwia radhi kama nitakuwa nimekosea]
 
Mwandishi kajitahidi sana, ila changamoto bado iko kwenye huu ushauri alioutoa. Nitatoa mfano:
Mwanzoni mwa mwaka huu, gazeti la mtanzania liliripoti uwepo wa chuo ambacho kinadhaniwa kutoa mafunzo ya kigaidi kisiwani Ukerewe. Mbunge wa huko Mh. Machemli (Chadema) alipotafanya mahojiano na mwandishi wa habari ile aliahidi kulifikisha swala la chuo hicho serikalini ikiwa na pamoja kutaka mitaala ya chuo hicho ikaguliwe. Haijulikani ni nini kilimtisha huyu mbunge wa upinzani (anayeaminiwa na mwandishi) kiasi kwamba ndani ya juma moja alikuwa ameyakana maneno yake licha ya kujua kuwa mwandishi alimrekodi. Wananchi wa Ukerewe bado wanahamu ya kujua mtaala wa hicho chuo, sifa za kujiunga na baada ya kozi wahitimu watafanya kazi gani. Mbunge alitishwa akatishika. Kwa hiyo kusema wabunge wa upinzani wanaweza wakawa msaada kwenye mambo ya usalama sidhani kama ni kweli.

.
Kwa habari ya usalama wa mtoa habari kwa Tanzania yupo hatarini zaidi ya tunavyofikiri. Mfano ndio unataka kutoa siri ya walipua mabomu kwa polisi ambao ndio wenye dhamana ya usalama wa raia, utaanzia wapi wakati wao ndio walipuaji wa raia? Rejea bomu la Arusha. Ukisema labda utae taarifa kwa usalama taifa kuhusu watekaji wango'a kucha, kutoboa macho na kumwagia tindikali, wao ndio wahusika; flregea kisa cha Dr Ulimboka na Rama Igondu. Ukitaka kuripoti kwa watawala kuhusu pesa chafu utaishia hewani kwani wao ndio wawindaji wa hizo fursa za upatikanaji wa pesa chafu na watoaji ulinzi wakubwa wa wahusika; regea Kina Rostam na richmondi/epa yao na kina wabunge mazungu ya unga. Kama ni kufa acha watuue tu! Hakuna namna ila kama kuna uwezekano wa personal defence tumia hiyo.

Natamnai mwandishi wa makala hiyo angekuwa member wa JF aweze kusoma michango hii apatekujua jinsi ushauri wake usivyofanya kazi katika mazingira ya sasa ya Tanzania. Pia akiweza ajikumbushe kisa cha kufungiwa 'maisha' gazeti la mwanahalisi.
 
Back
Top Bottom