Taikon wa Fasihi awards 2020

Taikon wa Fasihi awards 2020

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,197
Reaction score
79,692
TUZO ZA TAIKON WA FASIHI 2020

Mwaka umeisha, kama ilivyo ada ifikapo mwisho wa mwaka, tarehe kama za leo, nimekuwa na kawaida kutoa Tuzo kwa Watanzania ambao nimewaona wamefanya vizuri katika fani zao, au Nyanja mbalimbali. Tuzo hizi ni sehemu tuu ya kutambua, kuheshimu, kuzikubali, kutoa moyo kwa Watanzania wenzetu waendelee kufanya kazi nzuri zaidi. Nafahamu wapo Watanzania wengi wanaofanya kazi nzuri zaidi lakini hawa watawawakilisha.

Haya Mabibi na Mabwana, ule wakati wa Kutoa Tuzo umewadia, Nitawaomba pale nitakapo taja mshindi wa Tuzo mshangilie kwa furaha na bashasha.

A. TUZO ZA WANASIASA

1. Kiongozi Bora wa kisiasa wa kiume kwa Mwaka 2020
Mhe.ANTHONY JOHN MTAKA CHIGANGA, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

2. Kiongozi Bora wa Kisiasa wa Kike kwa Mwaka 2020
Mhe. Jokate Mwegelo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani

3. Kiongozi Bora wa vyama vya Upinzani kwa mwaka 2020
Mhe. Tundu Antipas Lisu, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA

4. Kiongozi Bora wa chama tawala CCM kwa mwaka 2020
Mhe. Humphrey Polepole, Aliyekuwa Katibu wa itikadi na uenezi taifa, CCM

5. Mwana CCM Bora aliyeitangaza CCM Mtandaoni bila kulipwa chochote na chama chake kwa mwaka 2020
Mwl. Dhadei Ole Mushi, Member wa JF, na Facebook

6. Mpinzani bora aliyetangaza CHADEMA Mtandaoni bila kulipwa chochote kwa Mwaka 2020
Bw, Malisa Godlisten, Member wa Jf na Facebook

7. Mwanapropaganda bora kwa mwaka 2020
BW/ Bi. Kigogo 2014, member wa Twitter

8. Chama cha Bora cha kisiasa kwa mwaka 2020
Chama cha Mapinduzi - CCM

9. Mwanasiasa aliyeongoza kwa kusemwa iwe kwa zuri au kwa Baya kwa mwaka 2020
Mhe. Rais, John Pombe Magufuli


B. TUZO ZA SANAA, MICHEZO NA BURUDANI

1. Mwana muziki Bora kwa mwaka 2020
Diamond Platnum, CEO wa WCB

2. Mwana Muziki Bora wa Kike kwa mwaka 2020
Nandy, Nandera.

3. Mchoraji Bora kwa mwaka 2020
Bw, Vensa Temu

4. Muigizaji bora wa kiume kwa mwaka 2020
Bw, Madebe Lidai

5. Mwigizaji Bora wa Kike kwa mwaka 2020
Pipi, Jina lake halisi ni MAGDALENA MUNISI, kacheza tamthilia ya Danga iliyoandikwa na kuongozwa na Idris Sultan

6. Mchekeshaji Bora wa Stand up comedy kwa Mwaka 2020
Maxwell the Great, wa Cheka Tuu

7. Kwaya bora kwa mwaka 2020
Zabron singers kahama

8. Mwandishi bora wa Fasihi(Riwaya) kwa Mwaka 2020
Ndg, Mtalaze Dickson, wa Kitabu cha Kijiji kisicho na Makaburi

9. Mchezaji Mpira bora kwa mwaka 2020
Aishi Manula, Golikipa wa Simba

10. Mkalimani Bora wa filamu kwa mwaka 2020
DJ MARK, Hamad Abdallah wa Acheche Production

11. Producer na Dj bora wa muziki kwa mwaka 2020

12. Mchekeshaji bora kwa mwaka 2020
Abdalah Nzunda, MKOJANI

13. Bondia Bora wa Masumbwi kwa mwaka 2020
Bw, Hassan Mwakinyo

C. TUZO ZA KIJAMII, UTAMADUNI NA MEDIA

1. Kungwi Bora kwa mwaka 2020
Irene Mbowe, wa Unga wa Bembeleza.

2. Mhamasishaji bora wa Mtandaoni kuchangia wahitaji kwa mwaka 2020
Bw, Malisa Godlisten, Member wa Jf na Facebook

3. Mtandao Bora wa Kijamii katika Nchi yetu kwa mwaka 2020
JAMII FORUM, ya Bw, Maxence Melo

4. Mchangiaji Bora wa mitandao ya Kijamii kwa mwaka 2020
> Infantry Soldier wa jamii Forum

5. Kampuni ya Mabasi inayotoa huduma Bora kwa mwaka 2020
Shabiby Luxuary Bus

6. Kiongozi wa Dini aliyetoa huduma bora kwa mwaka 2020
PASTOR DANIEL MGOGO

7. Msomaji bora wa simulizi kwa sauti kwa mwaka 2020
Ananias Edgar, msomaji wa Makala za Denis Mpagaze, wa ANANIA EDGAR TV

8. Shule bora kwa mwaka 2020
Kemebos Secondary School

9. Mganga bora wa masuala ya Miti, uganga, ulozi na uchawi kwa mwaka 2020
Mshana Jr, wa Jamii Forum, jina lake halisi kapuni

D. TUZO ZA UCHUMI NA BIASHARA

1. Mfanyabiashara bora kwa mwaka 2020
Bw, Fred wa Vunjabei

2. Mtangazaji bora mbunifu kwa mwaka 2020
Millard Ayo

3. Kijana mwenye kuhamasisha zaidi vijana kujiletea maendeleo kwa vitendo 2020
Millard Ayo

4. Mhamasishaji bora (Motivational speaker) kwa nadharia 2020
Bw, Anthony Luvanda, AKA MC luvanda.

5. Mkulima bora mdogo na mhamasishaji wa kilimo 2020
Mr. Papaya. Bado natafuta jina lake halisi

6. Dalali bora kwa mwaka 2020
Jacklini wa Ujenzi zone

7. Mkoa bora wenye fursa nyingi Tanzania kwa mwaka 2020
Mkoa wa Dar es salaam

Niwapongeze wale wote waliopata bahati ya kupata Tuzo hizi. Ni katika jitihada za kutambua kazi za wale waliofanya vizuri.

Muandaaji wa Tuzo,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Hizo tuzo bhana mbona sijamuona Sir Jeff Dennis
 
Daah🤔,hongera mkuu naamini umefanya kazi ya ziada sanaa.Ni kazi kubwa kuweza ku fit watu wote hao.
Kingine nashukuru kumuona bro wangu akitambuliwa na watu Mbalimbali .
Any way,kahama wew ni mwenyeji sehem gani??🤔

#jr
 
Daah🤔,hongera mkuu naamini umefanya kazi ya ziada sanaa.Ni kazi kubwa kuweza ku fit watu wote hao.
Kingine nashukuru kumuona bro wangu akitambuliwa na watu Mbalimbali .
Any way,kahama wew ni mwenyeji sehem gani??🤔

#jr

Mkuu, jiandae kuingia kwenye Tuzo zangu mwakani kwa kulifanyia taifa hili maajabu yenye manufaa
 
kwa kipi nilichokifanya cja ziada mkuu🤔🤔?
Any way ,niwakati wa kuchapa kazi na kudumisha amani kwa taifa letu
#jr

Ni kweli Mkuu, wakati wa kufanya maajabu katika kazi zetu ni huu.

Jitahidi mwakani Mungu akijalia mwezi kama huu nikuweke kwenye List ya Tuzo kama mtu aliyetisha kwenye fani yake
 
Ni kweli Mkuu, wakati wa kufanya maajabu katika kazi zetu ni huu.

Jitahidi mwakani Mungu akijalia mwezi kama huu nikuweke kwenye List ya Tuzo kama mtu aliyetisha kwenye fani yake
Ahsante nitafanya hivyo mkuu.Ni fahari na furaha kwa any body kutambuliwa kwa kile anachokifanya.


But mkuu nimekuuliza swali hujajibu,kahama wew ni mwenyeji maeneo gani??🤔
 
Mkuu hizo tuzo zimekaa palipo, hapo hakuna upendeleo hapo
Upendeleo upo maana chanzo xha taarifa zako ni media na social media.

Kwahiyo umetumia sana watu ambao kutwa kucha wanajitanfaza mitandaoni.

Mfano ni Huyo Mgogo na Jokate. Hawana maajabu ila ni mabingwa wa social media. Hata Vunja Bei katumia pesa na nguvu sana kujitangaza kwa mwaka huu.
 
Upendeleo upo maana chanzo xha taarifa zako ni media na social media.

Kwahiyo umetumia sana watu ambao kutwa kucha wanajitanfaza mitandaoni.

Mfano ni Huyo Mgogo na Jokate. Hawana maajabu ila ni mabingwa wa social media. Hata Vunja Bei katumia pesa na nguvu sana kujitangaza kwa mwaka huu.

Mkuu biashara ni matangazo
Kabla hujatangazwa, jitangaze. Hiyo ni kanuni Mzee Baba.

Bila mitandao unafikiri huduma zingekuwaje?
 
Back
Top Bottom