October 9, 2018
Dar-es-Salaam, Tanzania
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars kitaondoka usiku wa leo kuelekea mjini Praia, Cape Verde kwa ndege ya kukodi kuifuata timu ya taifa ya huko kwa ajili ya michuano ya kufuzu kwa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kambi ya timu hiyo Waziri Mwakyembe amesema, mabadiliko ya safari hiyo kutoka Dream Liner na kuamua kukodi ndege yanatokana na ufinyu wa uwanja wa ndege wa Mjini Praia ambao hauwezi kutua ndege kubwa.
Aidha Waziri Mwakyembe amewataka wachezaji wa Taifa stars wakacheze kwa kujituma ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo huku akiwasihi watanzania kuiombea timu hiyo.
Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia na Nahodha Msaidi wa Taifa Stars Himidi Mao wameelezea maandalizi ya mchezo huo.
Habari & Video kwa hisani kubwa ya:
Source: Global TV Online