Taifa Stars kichwa cha mwendawazimu???..........mpaka lini??!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa Stars kichwa cha mwendawazimu???..........mpaka lini??!!

Discussion in 'Sports' started by Sajenti, Oct 18, 2011.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mshabiki mkubwa wa soka ya hapa Tanzania hali kadharika kutokana na utandawazi uliopo sasa na napenda pia soka ya nje ya Tanzania. Lakini kubwa nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu mwenendo wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Kwa maoni yangu sielewi hasa kile wenzetu walipopewa dhamana ya kuendesha michezo nchini ikiwemo soka kama wanajua wanachokifanya. Tumekuwa wepesi wa kutamani mafanikio bila kuyatokea jasho. maneno mengi yanazungumzwa na viongozi wa vyama vya soka kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa kuwa eti soka ya Tanzania imekuwa, mimi nasema hapana imeshuka tena kwa kasi kubwa ni kama gari iliyoshindwa kupanda mlima ikarudi nyuma.

  Kwa maoni yangu hebu watanzania tuamke na tuwe serious na kile tunachotamani kufanikiwa nacho. Katika soka msingi wa mafanikio ni mipango ya kuandaa timu za watoto na vijana ambao mwishowe ndio hao huingia timu ya taifa. Siamini katika kubadirisha makocha kama nguo kuwa ndio suluhu. Hapa hata tungeletewa Sir Alex Furgeson, Jose Morinho au Carlo Ancelloti hakuna kipya kwani tatizo ni msingi mbovu. Karibu 80% ya wachezaji waliopo sasa katika timu a taifa ni wachezaji wasio na uwezo na kasi ya kucheza mpira wa sasa. Bila kubadirisha mitazamo yetu ili kujenga msingi imara na endelevu taifa stars itaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu kama alivyowahi kusea raisi mstaafu wa awamu ya pili alhaji Ali HAsani Mwinyi kila mtu anajifunzia kunyoa kwetu. Naongea hili kama mtanzania ninayekerwa na hali ya timu yetu ya taifa. Viongozi wabadirike na kuwa na mtazamo chanya. Sasa hivi dunia imekuwa kama kijiji habari na mamb mbali mbali tunayapata kwa urahisi. Inashamgaza sana licha ya sasa hivi taifa stars kuwa na wafadhili wengi na wanaotoa fedha nyingi timu inadorora kila uchao. Miaka ya 80 ambapo suala la timu ya taifa walitupiwa FAT bado mpira ulionekana kiasi cha timu kukata tiketi kucheza mashindano ya Afrika.

  Tusipoamka wenyewe hakuna atakayekuja kutuamsha tutabaki kubadirisha makocha tukidhani wao ndio wanaocheza mpira na kuleta mafanikio......naishi hapa kwa leo hebu tujadili wapenda soka.
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Yeah ni kichwa cha mwendawazimu hii timu
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  sajenti umeongea mengi na kwa uchungu sana. Ndiyo maana ukitazama utaona thread yangu,''tatizo la Taifa Stars ni kocha?''nami nakukaribisha kuchangia. Mimi nafikiri kwa jinsi tunavyoendesha soka letu na michezo yote kwa ujtmla,ni kama uwe Ulaya halafu usiku umeme ukatike ghafla.Kibiriti hujui uanzie kukitafutia wapi! Pamoja na udhamini mkubwa,makocha wa kigeni,wachezaji tulio nao,hatufiki mbali kimichezo,hususan soka,achilia mbali kuchukua vikombe. Huwa naangalia mataifa kama Chezc Republic,Uholanzi na Ugiriki. Kwa muda mrefu hawakuwa wamechukua vikombe lakini WAMO KWENYE RAMANI YA SOKA! Kuwa kwenye ramani ya soka kunaleta matarajio ya kuchukua vikombe hapo mbeleni.. Tufanyeje? Tafakari.. Pitia thread yangu uangalie.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ishu ni kuandaa timu kuanzia watoto na sio kufanya maandalizi ya zima moto kama tunavyofanya.
  hata aje Morinho kwa timu tuliyo ayo hawana jipya.
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,036
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Na kocha ni tatizo,anachagua shikamoo jazz sana.
   
 6. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  anakuwa hana mbadala ukizingatia ndio ana mechi ya mashindano wiki moja mbele ulitegemea atapata wapi wengine wapya kuwajenga na kuingia mashindanoni?
   
Loading...