Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
- Thread starter
- #21
Jibu hoja na wala usilete porojo za kilumumba Lumumba......mimi nadhani unataka huruma ya kisiasa tu! unachokitaka wewe ni kile unachokiita uhuru wa habari na mawasiliano kwa kuitumia katiba vibaya, ili upate fursa ya kuupotosha umma.
Unasema kwamba taifa lipo njia panda, wewe mwenyewe unafahamu kwamba hii si sahihi, bali chama chako chadema ndiyo kipo njia panda.
Jitahidi kuleta threads ambazo zitawarudisha ktk mstari, vinginevyo tutawamisi sana chadema.
Hebu niambie huyo Mwenyekiti wako wa Chama kwa kutumia ile kofia yake nyingine ya dola hajapiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020?
Sasa nikuulize wewe kada mwenzake, huyu Rais ametumia Ibara ipi ya Katiba ya nchi yetu kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani na kuruhusu chama chake cha CCM kiendelee kufanya mikutano ya kisiasa bila kubughuziwa na vyombo vya usalama?
Nyinyi wanaccm endelezeni tu unafiki wenu.....
Lakini jaribuni kujiuliza imekuwaje mtu kama Nape aliyeamua 'kujipendekeza' kwa Mkulu kwa kuondoa Bunge Live, lakini hatimaye amekuja kutolewa bastola pale Protea!
Unaweza kujiona leo uko salama, lakini kwa utawala huu wa Magu, hakuna mwenye uhakika ya kesho yake, whether you are a CCM leader or from opposition......
Solution ni moja tu ya kuiepusha nchi hii isiangamie, ni wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, kupaza sauti zao kwa nguvu zao zote kumwambia Magu na serikali yake warejeshe utawala wa sheria nchini utakaoheshimu Katiba ya nchi yetu ambayo ndiyo sheria mama, ambayo Rais wetu aliapa kuilinda na kuitii kabla hajakabidhiwa jukumu la kuongoza nchi yetu.