Taifa lipo njiapanda, wananchi ndiyo tutakaoliokoa au kuliangamiza

mimi nadhani unataka huruma ya kisiasa tu! unachokitaka wewe ni kile unachokiita uhuru wa habari na mawasiliano kwa kuitumia katiba vibaya, ili upate fursa ya kuupotosha umma.
Unasema kwamba taifa lipo njia panda, wewe mwenyewe unafahamu kwamba hii si sahihi, bali chama chako chadema ndiyo kipo njia panda.
Jitahidi kuleta threads ambazo zitawarudisha ktk mstari, vinginevyo tutawamisi sana chadema.
Jibu hoja na wala usilete porojo za kilumumba Lumumba......

Hebu niambie huyo Mwenyekiti wako wa Chama kwa kutumia ile kofia yake nyingine ya dola hajapiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020?

Sasa nikuulize wewe kada mwenzake, huyu Rais ametumia Ibara ipi ya Katiba ya nchi yetu kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani na kuruhusu chama chake cha CCM kiendelee kufanya mikutano ya kisiasa bila kubughuziwa na vyombo vya usalama?

Nyinyi wanaccm endelezeni tu unafiki wenu.....

Lakini jaribuni kujiuliza imekuwaje mtu kama Nape aliyeamua 'kujipendekeza' kwa Mkulu kwa kuondoa Bunge Live, lakini hatimaye amekuja kutolewa bastola pale Protea!

Unaweza kujiona leo uko salama, lakini kwa utawala huu wa Magu, hakuna mwenye uhakika ya kesho yake, whether you are a CCM leader or from opposition......

Solution ni moja tu ya kuiepusha nchi hii isiangamie, ni wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, kupaza sauti zao kwa nguvu zao zote kumwambia Magu na serikali yake warejeshe utawala wa sheria nchini utakaoheshimu Katiba ya nchi yetu ambayo ndiyo sheria mama, ambayo Rais wetu aliapa kuilinda na kuitii kabla hajakabidhiwa jukumu la kuongoza nchi yetu.
 
Hakuna uhuru usio na mipaka! Taifa liko njia panda labda kwenye mitandao ya kijamii..kila mtu anaendelea na shughuli zake na wahalaifu kama Lissu wanaendelea kushughulikiwa kama kawaida..

Hahahahaha taifa liko njia pandwa kwakuwa Mhalifu kashikwa? Kwanza sio watu wote wanajua kama huyo muhalifu kakamatwa..tatizo lako unafikiri kila mtanzania anapita jf...acha mhalifu akabiliwe vilivyo
 
Wewe jidanganye na hako kaposho kako unakokapata kwa ajili ya kueneza propaganda humu JF......

Lakini hakika under Sizonje's rule, hakuna mtu atayejiaminisha kuwa yuko salama by 100%

Naendelea kurudia nchi iko njiapanda na wananchi wanapaswa waitikie wosia aliotuachia Mwalimu Nyerere ambaye alisema tusiogope kukemea, tunapoona dalili za udikteta unaingia nchini.

Na hali hiyo ndiyo inayojitokeza kwenye awamu hii ya huyo Bwana mkubwa.
 
Ni kweli kabisa Mkuu BAK.

Kwa bahati mbaya sana nchi yetu kwenye awamu hii ya 5 tumepata Mkuu wa nchi ambaye anaamini kila kitu anachoongea yeye ni 100% perfect na kwa yeyote anayeamua kumkosoa, ingawa ni haki yake ya kikatiba, anamwita analeta chokochoko na anaviagiza vyombo 'vyake' vya dola vimshughulikie!

Kama Taifa hakika safari hii tumeuingia mkenge.....
Huyu wetu anajifanya hasikii kitu, mungu mtu
 
Nina hakika kwamba wanaosifia leo ndio hao hao watakaokosoa kesho utawala ukiondoka! Nina Hakika pia kwamba ndani ya ccm kuna wengi tu wanalalamikia gizani wakiwa wamejifungia. Hii ndo ule unafiki uliokubuhu! Hivi haimpasi mtu kupimwa akili anapopendekeza jambo ambalo katiba inalikataa?
hivi tunaipenda tanzania au mtu? maana watu watapita lakini tanzania haitapita kamwe! Basi natuambiwe tu kuwa kaja masihi au mtume msaidizi!
 
mimi nadhani unataka huruma ya kisiasa tu! unachokitaka wewe ni kile unachokiita uhuru wa habari na mawasiliano kwa kuitumia katiba vibaya, ili upate fursa ya kuupotosha umma.
Unasema kwamba taifa lipo njia panda, wewe mwenyewe unafahamu kwamba hii si sahihi, bali chama chako chadema ndiyo kipo njia panda.
Jitahidi kuleta threads ambazo zitawarudisha ktk mstari, vinginevyo tutawamisi sana chadema.

Wale wale UKUKU,endelea kupiga makofi.
Nitamuomba mleta mada aweke Clip ya JKN aliyokemea watu kama JPM.

In short hatufai kuwa kiongozi wa Taifa letu,aende kwao akafige Ng'ombe
 
It is true.

Yaani watu wanashangilia hao wanaoitwa waandamanaji wanaopendekeza JPM awe Life President wetu.....

Wakati Katiba yetu ya nchi inatoa ukomo wa miaka 10 kwa Rais yeyote hapa nchini kuwa hapaswi kuongoza nchi yetu kwa zaidi ya miaka 10

Kwenye Uzi wako ukiweka na ile Clip ya JKN ya kumpinga Rais kama.JPM itawasaidia Lumumba FC
 
Kwenye Uzi wako ukiweka na ile Clip ya JKN ya kumpinga Rais kama.JPM itawasaidia Lumumba FC
Hebu nimwombe Mkuu BAK atuwekee ile clip ya Mwalimu Nyerere aliyotuasa waTZ tusikae kimya wakati tunaona tunatawaliwa na mtu anayeiendesha nchi kidikteta.
cc : BAK
 
Hebu nimwombe Mkuu BAK atuwekee ile clip ya Mwalimu Nyerere aliyotuasa waTZ tusikae kimya wakati tunaona tunatawaliwa na mtu anayeiendesha nchi kidikteta.
cc : BAK

Utafanya la maana na lile la ubaguzi
 
Naanza kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1) ambayo inasema hivi " Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia Uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na chombo chochote" mwisho wa kunukuu.

Nimeanza kwa kunukuu Ibara hiyo ya Katiba ya nchi yetu, ambayo ndiyo sheria mama nchini mwetu, ambayo pia Katiba hiyo viongozi wetu wakuu akiwemo Rais wetu wa nchi aliapa kuilinda na kuitii kabla ya kukabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu.

Kwa bahati mbaya sana Taifa letu linaloongozwa na serikali hii ya CCM ya awamu ya tano imeintroduce kitu cha hatari sana kwenye nchi yetu ambacho kama kisipokemewa na kila mwananchi mwenye kuitakia mema nchi hii, hakika nchi hii inaelekea kuangamia.

Kitu hicho si kingine Bali ni kuwa Taifa letu hivi sasa linatakiwa liimbe mwimbo mmoja tu wa kuisifu serikali yetu ya awamu ya 5 hususani Rais wetu kwa kila jambo wanalolifanya na kwa yeyote anayeikosoa serikali hii ametengenezewa msamiati mpya wa kuitwa mchochezi na mtetezi wa mafisadi wanaopora rasilimali zetu!

Kutokana na hali hiyo Taifa letu hivi sasa wananchi wake almost wote wamejazwa hofu kuanzia viongozi na wanachama wa CCM, viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, wanaharakati, viongozi wa dini, vyombo vya habari vya Umma pamoja na vya binafsi na wananchi wote kwa ujumla wake wametengenezewa mazingira ya kuzibwa midomo yao kwa yeyote anayetaka kuikosoa serikali ya awamu ya 5.

Lakini wakati huo huo metolewa RUKSA isiyo na mipaka kwa yeyote anayeimba wimbo wa kuisifia serikali ya awamu ya 5!

Tumeshuhudia wale wanaoandamana na kutoa maoni yao kuwa Katiba ya nchi ibadilishwe na kumfanya Rais wetu JPM awe Life President wetu ingawa ni maoni ya hatari sana yanayoweza kulitumbikiza Taifa letu kwenye machafuko, lakini watu hao wamekuwa wakiachwa huru bila kuguswa na chombo chochote cha dola.

Lakini wakati huo huo kwa yeyote mwenye kutoa maoni ya kuikosoa serikali hii ya awamu ya 5, ingawa ni haki yake ya kikatiba tumekuwa tukishuhudia watu wa aina hiyo wakishughulikiwa kikamilifu kwa kuwekwa ndani kwa kile kinachoitwa masaa 'yao' 48 ya wateule wa Rais!

Tunawaomba hao wateule wa Rais watufafanulie ni Ibara ipi ndani ya Katiba yetu inayotoa katazo kwa mwananchi yoyote kumkosoa Rais wetu?

Hebu tujiulize kitu kimoja iwapo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inatamka wazi kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi vya kisiasa na vyama hivyo vitatakiwa kuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake za kisiasa, sasa tunapaswa kumuuliza Rais wetu amepata wapi mamlaka ya kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akiruhusu chama chake cha CCM kiendelee kufanya shughuli zake za kisiasa bila kubughuziwa na vyombo vya usalama?

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake amewahi kutamka kuwa wananchi hatupaswi kukaa kimya tunapoona Rais wetu ana elements za kuendesha nchi yetu kidikteta na tunapaswa kupaza sauti zetu bila woga kumkenea Rais wa aina hiyo na Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kumuelezea Rais wa aina hiyo asiyetaka kuendesha nchi kwa misingi ya Katiba yetu kuwa HATUFAI.

Kwa hiyo hivi sasa siyo wajibu wa vyama vya siasa vya upinzani peke yao kukemea mfumo wa uendeshaji wa serikali ya awamu ya 5 wa kukandamiza waziwazi demokrasia yetu bali ni wajibu wa kila mwananchi, kila Kiongozi wa dini na kwa taasisi za haki za kibinadamu pamoha na vyombo vya habari vyote kukemea kwa nguvu zetu zote kuiambia serikali yetu ya awamu ya 5 kuwa ijirekebishe na kurudi kwenye mfumo wa utawala wa sheria wa Kuifuata Katiba ya nchi ambapo Rais wetu kabla hajaingia madarakani aliapa kuilinda na kuitii Katiba yetu.

Iwapo wananchi tutaamua kukaa kimya kwa hofu ya kiviogopa vyombo vya dola kutulaza ndani kwa zile saa 'zao' 48 za wateule wa Rais kwa kile walichokibatiza jina la uchochezi, hakika tutakuwa tumeamua kuliangamiza Taifa letu na historia haitatuacha salama kwa maana itatuhukumu.

Mungu libariki Taifa letu la Tanzania na uliepushe lisiangamie.
Mku hili ni la ukweli kwani mwogope mtu ambaye malalamiko yake anayatolea ktk blangeti ni mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi cha kampeni niliandika Mara kadhaa kuhusu tatizo la akili la mgombea flani lakini Jf moderators wakawa wanafuta
Iko haja kwa sasa waTz kutafakari kwa makini kama kweli huyo jamaa yupo sawa huko upstairs?
 
Iliyopo njia panda ni chadema mkuu, taifa linasonga mbele kwa maendeleo kila mahali. Awamu ya tano ni awamu bora kabisa. Wananchi wanaikubali.
 
Ni bahati mbaya sana CCM imetengeneza taifa la wajinga ambao katika awamu hii ya tano wanaamini raisi tuliyenaye ni masihi amabye amekuja kuukomboa ulimwengu hivyo kazi yao ni kumuimbia mapambio ya kumsifu na kumuabudu kiasi kwamba na yeye ameshajiiunia na kujiweka katika nafasi sawa na Mungu kimatendo na matamshi yake!
 
mimi nadhani unataka huruma ya kisiasa tu! unachokitaka wewe ni kile unachokiita uhuru wa habari na mawasiliano kwa kuitumia katiba vibaya, ili upate fursa ya kuupotosha umma.
Unasema kwamba taifa lipo njia panda, wewe mwenyewe unafahamu kwamba hii si sahihi, bali chama chako chadema ndiyo kipo njia panda.
Jitahidi kuleta threads ambazo zitawarudisha ktk mstari, vinginevyo tutawamisi sana chadema.
Unamsifu bondia wako kuwa ni mashuhuri kwakati wapinzani wake unawafunga mkono wakati wa mpambano.
Aibu kubwa sana nyie mliokuwa brainwashed
 
I
Ni bahati mbaya sana CCM imetengeneza taifa la wajinga ambao katika awamu hii ya tano wanaamini raisi tuliyenaye ni masihi amabye amekuja kuukomboa ulimwengu hivyo kazi yao ni kumuimbia mapambio ya kumsifu na kumuabudu kiasi kwamba na yeye ameshajiiunia na kujiweka katika nafasi sawa na Mungu kimatendo na matamshi yake!
It is very true
 
Viongozi wetu wa dini ndiyo wanao tukwamisha kama wao wangeli kuwa mstari wa mbele kutoa matamko ya misimamo sahihi nina imani huu UKOLONI ungeli ondoka bahati mbaya wanaogopa JELA kuliko MUNGU
Viongozi wa dini mkuu? Dini ipi? Hawa hawa wachumia tumbo?
 
Back
Top Bottom