Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Naanza kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1) ambayo inasema hivi " Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia Uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na chombo chochote" mwisho wa kunukuu.
Nimeanza kwa kunukuu Ibara hiyo ya Katiba ya nchi yetu, ambayo ndiyo sheria mama nchini mwetu, ambayo pia Katiba hiyo viongozi wetu wakuu akiwemo Rais wetu wa nchi aliapa kuilinda na kuitii kabla ya kukabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu.
Kwa bahati mbaya sana Taifa letu linaloongozwa na serikali hii ya CCM ya awamu ya tano imeintroduce kitu cha hatari sana kwenye nchi yetu ambacho kama kisipokemewa na kila mwananchi mwenye kuitakia mema nchi hii, hakika nchi hii inaelekea kuangamia.
Kitu hicho si kingine Bali ni kuwa Taifa letu hivi sasa linatakiwa liimbe mwimbo mmoja tu wa kuisifu serikali yetu ya awamu ya 5 hususani Rais wetu kwa kila jambo wanalolifanya na kwa yeyote anayeikosoa serikali hii ametengenezewa msamiati mpya wa kuitwa mchochezi na mtetezi wa mafisadi wanaopora rasilimali zetu!
Kutokana na hali hiyo Taifa letu hivi sasa wananchi wake almost wote wamejazwa hofu kuanzia viongozi na wanachama wa CCM, viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, wanaharakati, viongozi wa dini, vyombo vya habari vya Umma pamoja na vya binafsi na wananchi wote kwa ujumla wake wametengenezewa mazingira ya kuzibwa midomo yao kwa yeyote anayetaka kuikosoa serikali ya awamu ya 5.
Lakini wakati huo huo metolewa RUKSA isiyo na mipaka kwa yeyote anayeimba wimbo wa kuisifia serikali ya awamu ya 5!
Tumeshuhudia wale wanaoandamana na kutoa maoni yao kuwa Katiba ya nchi ibadilishwe na kumfanya Rais wetu JPM awe Life President wetu ingawa ni maoni ya hatari sana yanayoweza kulitumbikiza Taifa letu kwenye machafuko, lakini watu hao wamekuwa wakiachwa huru bila kuguswa na chombo chochote cha dola.
Lakini wakati huo huo kwa yeyote mwenye kutoa maoni ya kuikosoa serikali hii ya awamu ya 5, ingawa ni haki yake ya kikatiba tumekuwa tukishuhudia watu wa aina hiyo wakishughulikiwa kikamilifu kwa kuwekwa ndani kwa kile kinachoitwa masaa 'yao' 48 ya wateule wa Rais!
Tunawaomba hao wateule wa Rais watufafanulie ni Ibara ipi ndani ya Katiba yetu inayotoa katazo kwa mwananchi yoyote kumkosoa Rais wetu?
Hebu tujiulize kitu kimoja iwapo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inatamka wazi kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi vya kisiasa na vyama hivyo vitatakiwa kuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake za kisiasa, sasa tunapaswa kumuuliza Rais wetu amepata wapi mamlaka ya kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akiruhusu chama chake cha CCM kiendelee kufanya shughuli zake za kisiasa bila kubughuziwa na vyombo vya usalama?
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake amewahi kutamka kuwa wananchi hatupaswi kukaa kimya tunapoona Rais wetu ana elements za kuendesha nchi yetu kidikteta na tunapaswa kupaza sauti zetu bila woga kumkenea Rais wa aina hiyo na Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kumuelezea Rais wa aina hiyo asiyetaka kuendesha nchi kwa misingi ya Katiba yetu kuwa HATUFAI.
Kwa hiyo hivi sasa siyo wajibu wa vyama vya siasa vya upinzani peke yao kukemea mfumo wa uendeshaji wa serikali ya awamu ya 5 wa kukandamiza waziwazi demokrasia yetu bali ni wajibu wa kila mwananchi, kila Kiongozi wa dini na kwa taasisi za haki za kibinadamu pamoha na vyombo vya habari vyote kukemea kwa nguvu zetu zote kuiambia serikali yetu ya awamu ya 5 kuwa ijirekebishe na kurudi kwenye mfumo wa utawala wa sheria wa Kuifuata Katiba ya nchi ambapo Rais wetu kabla hajaingia madarakani aliapa kuilinda na kuitii Katiba yetu.
Iwapo wananchi tutaamua kukaa kimya kwa hofu ya kiviogopa vyombo vya dola kutulaza ndani kwa zile saa 'zao' 48 za wateule wa Rais kwa kile walichokibatiza jina la uchochezi, hakika tutakuwa tumeamua kuliangamiza Taifa letu na historia haitatuacha salama kwa maana itatuhukumu.
Mungu libariki Taifa letu la Tanzania na uliepushe lisiangamie.