Taifa linaumwa lipo ICU, nani mkombozi wake?

Taifa linaumwa lipo ICU, nani mkombozi wake?

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,745
Reaction score
1,171
Upo msemo wa wahenga unasema asiyejua kufa achungulie kaburi. Msemo huu umebeba dhima nzito juu ya uumbaji wa Dunia na mwanadamu.

Quran tukufu nayo imesema kila nafsi itaonja mauti,Kwa msingi huo kifo ni sehemu ya uumbaji katika kumkutanisha Mja na Muumbaji.

Kama kifo ni wajibu kwanini tunahangaikia watu wetu kuishi Kwa gharama kubwa wanapoumwa ili kunusuru uhai wao,uliwahi kujiuliza hili swali!

Tunahangaika Kwa kuwa udhaifu wa binadamu ndipo unapoanzia na kutengeneza maandiko ya ziada kuwa jisaidie kwanza nami nikusaidie,na kwa umuhimu wa jambo lenyewe serikali inaamua kufanya biashara ya afya na wananchi wake,Kwa mantiki ya nipe fedha nikupe afya.

Kipaumbele cha kwanza Cha serikali za kidunia ni afya ya Wananchi wake,ndiyo maana Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ustawi wa Wananchi umetajwa kama ndiyo msingi mkuu wa serikali, hivyo serikali inawajibika kulinda na kustawisha afya za Wananchi wake kiafya, kijamii, kiuchumi n.k.

Kwa kulitambua Hilo,serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanzisha Kwa makusudi mazima biashara ya afya Kwa Wananchi kama msingi wa ustawi wa Wananchi bila kujali hawa ndiyo walipaji Kodi wakubwa, na fedha zao ndizo zinatumika kununua dawa za hospitalini, vifaa tiba n.k. wakistahili grace period ya ulipaji Kodi wao Kwa njia ya Matibabu kama msamaha unavyotolewa Kwa wawekezaji.

Leo hii hakuna mwananchi asiyefanya biashara na serikali ya kununua huduma mbalimbali ambazo ni kinyume na takwa la katiba kuwa msingi mkuu wa serikali ni ustawi Kwa Wananchi.

Maanake ni kwamba mbali na Kodi za Bure serikali inayokusanya toka Kwa Wananchi Bado inatumia fedha hizo hizo kuwauzia huduma za ustawi Wananchi.

Leo nitazungumzia Afya ya Taifa iliyoko ICU ambayo serikali imewekeza fedha za walipa Kodi waaminifu wa nchi hii kwenye biashara ya afya ya wananchi hao.

Tumeona serikali ikijinadi na kujinasibu kupitia Rais aliyeko madarakani aliyehodhi mamlaka ya serikali kuwa chini yake Kwa jina la fedha za mama kuwekeza kwenye majengo na vifaa tiba Kwa hospitali mbalimbali za umma kote nchini.

Katika kuupiga kwake mwingi, wananchi wameendelea kutaabika kwenye suala Zima la afya ya kila mmoja.

Watanzania hawatibiwi bila kuwa na fedha bila hata kujali ni wachangiaji waaminifu wa Kodi inayokusanywa Kwa mabavu na serikali hii, bila ushirikishwaji wa wananchi zaidi ya watunga sera.

Ukilazwa kwenye hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili kama huna fedha maanake umechagua kufia kwenye majengo ya serikali badala ya kufia Nyumbani.

Hii ni Kwa sababu kama huna fedha huwezi pata dawa, imesababisha mamia ya wagonjwa kufariki Dunia wakiwa wodini Kwa kukosa fedha za dawa, huku wakiendelea kulipia kitanda na gharama zingine mbalimbali zinazoendelea Kwa njia ya bill.

Mfumo huu wa biashara umeathiri Sana maisha ya wananchi wanaolazwa kwenye hospitali mbalimbali huku aliyeupiga mwingi akijinasibu amejenga hospitali Kila Wilaya.

Nimekaa Muhimbili nikimuhudumia Mgonjwa wangu Kwa siku 40, nimeshuhudia zaidi ya wagonjwa waliofariki 100 Kwa siku hizo, wengi wakikosa huduma sahihi kutokana na kukosa matibabu sahihi Kwa ukosefu wa fedha, lakini Nchi ikiendelea kupalilia Deni la Taifa zaidi ya T 107/-

Unajiuliza ikiwa Taifa halina kipaumbele cha afya Kwa Wananchi wake,kulinganisha na deni la Taifa sanjari na ukuaji uchumi wa Mama,hizo fedha zinawekezwa kwenye nini!

Hiyo ni Moja, lakini hata maiti ya aliyefariki Kwa kukosa huduma sahihi akiwa Mgonjwa anadaiwa, na huwezi kumzika bila kulipia gharama za Matibabu za Mtu mfu aliyekufa Kwa kukosa huduma ila akidaiwa fedha za pango la hospitali.

Kuna haja gani Sasa kuwa na hospital ya Taifa ikiwa serikali imeacha msingi mkuu wa ustawi wa wananchi wake kupata ustawi wa afya ya mwili na akili!

Ni wakati sasa Kwa watunga sera kuziheshimisha fedha zetu za Kodi Kwa kuweka msingi mzuri wa matumizi ya Kodi katika kuokoa nguvu kazi ya Taifa inayopotea Kila kukicha.

Yanayoendelea kwenye hospitali za umma hakuna tofauti na hospital za watu binafsi.

Tunaposemea mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi wenye kusimika viongozi wasio na tija Kwa Taifa ni pamoja na kugatua utekelezaji yakinifu wa sera ya afya Kwa Taifa Kwa kuzifanyia reforms angalau ule ustawi wa wananchi uonekane Kwa kiwango fulani.

Ni wakati sasa wa kujienga Tanzania Kwa kuruhusu wenye moyo safi kutuonyesha njia, kuendelea kuwatumia watengeneza matatizo Kwa ustawi wa Kodi za wanyonge ni kulinajisi Taifa na nchi Kwa umoja wake.

#NRNE ikawe Chachu ya kuiondoa afya ya Taifa ICU.

Mungu ibariki Tanganyika Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom