Wanabodi nawaamkua
Muda mrefu nimekuwa msomaji humu kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Lakini kwa uwezo wa Mungu Muumba nimeona nichukue wasaa kuandika huu uzi mfupi.
Tanzania (Tanganyika) ilipofikia sasa ni njiapanda ngumu with narrow escape. Sababu za kusema hayo ni kwamba
- Viongozi wamejigeuza watawala huku wakidhibiti maoni chanya na ukosoaji wowote
- Vyombo vya dola vimewageuza raia sisi kama adui namba moja wa nchi
- Wengi wanaosimama na wananchi, wanaonekana ni mongers wa madaraka. Ambapo wakipewa madaraka baada ya kuhamia CCM wanageuka more vampires kuliko wenyejj CCM.
- Srrikali imejitenga na wananchi. Katiba hususan Ibara ya 8 inapuuzwa na kusiginwa kupitia matendo ya Serikali
- Kutekwa na kuuawa wakosoaji na ili mkosoaji apone chupuchupu ni pale atakapobambikizwa kesi na kushtakiwa
- Mhimili wa Mahakama umegoma na kukwepa kusimamia HAKI. Mahakama kwa umoja wake imesimama upande wa watawala bila kujali athari za muda mrefu
- Wapunzani wamefunguliwa kesi za kubumba, mfano kesi ya uhaini dhidi ya Lisu n.k.
- Sababu ni nyingi, unaweza kuongezea za kwako pia...
Nchi inakuhitaji kwa sababu;
- Uzalendo ni kuipigania nchi hususan ustawi chanya wa demokrasia, uchumi, kisekta, kiutamaduni na kadhalika kwa gharama yeyote.
- Mungu anaifuta CCM, hivyo ni jukumu lako na langu kutumia akili na hekima alizotupa Mungu kutengeneza mbadala wake
- Mfumo wa nchi umejengwa katika kuisaidia CCM kuliko nchi. Mauaji na matukio hasi ya kisiasa dhidi ya raia yanaonekana dhahiri kutendwa ama kuratibiwa na vyombo vya dola. Hivyo kama mimi na wewe hatutosimama kuhesabiwa kila mtu atafikiwa kwa wakati wake na kutendwa kiuovu, yowe la mtu mmoja liamshe MAYOWE ya kupambanja haki
No Reforms
No Election