Taifa linahitaji uponyaji je nani wa kuliponya?

Taifa linahitaji uponyaji je nani wa kuliponya?

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
265
Taifa letu limeingia katika kiza kizito ambacho hatukuwahi kufikiria ,wakati tunaomboleza vifo vya wenzetu 500+ walipoteza Maisha wakati wa uchaguzi bado mioyo ya watu wengi haina faraja na matumaini.

Tunapitia kipindi kigumu kama taifa kila mmoja najiuliza tumefikaje?Mwaka 2021 Raisi aliingia madarakani alionekana taa inayoangaza akiwa amekuja kuwafuta machozi wa Tanzania lakini mpaka leo hii 2026 mambo yamebadilika ghafla nchi imeingia katika kiza kinene Taifa limejaa majeraha makubwa

Je nani wa kuliponya Taifa? Nani wa kuleta maridhiano ya kweli ndani ya mioyo ya watanzania ,hatutaki kutengeneza usugu kwa unafiki tunahitaji namna nzuri ya kurejesha Taifa kwenye misingi iliyokuepo.
 
Back
Top Bottom