MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 15,739
- 39,770
Turudishe nyumba zote za msajili (NHC) tulizodhulumu (tulizotaifisha) kutoka kwa wageni na watu wetu . Turudishe mabenki, mashamba, viwanda, shule na taasisi zote tulizo dhulumu (taifisha) kutoka kwa wageni na wananchi wetu. Tuwaombe radhi na kuwalipa fidia watu wote waliodhulumiwa na mali zao kuharibiwa wakati wa Azimio la Arusha na operation vijiji.
Tufanye sala kuu ya toba, taifa limrudie Mungu, bila hivyo maendeleo tutayasikia redioni na kwenye television. Kwani, tulidhulumu watu na vilio vya watu hao waliodhulumiwa vinalitesa taifa letu. Taifa letu limebarikiwa na kila lililo jema lakini bahati mbaya, kwa sababu ya dhuluma hiyo, hakuna kinachotokea.
Muheshimiwa Raisi, hatujalogwa, ila tulidhulumu, sasa laana ya dhuluma hiyo ndiyo inayotutafuna. Turudishe mali zisizo zetu ili tuweze kufungua milango ya bahati kwa manufaa ya taifa letu.
Nawasilisha kwaajili ya mapovu baridi na moto.