Taifa Limenza kugawanyika

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,012
2,179
Mbali na matatizo ya Kisiasa nchini na mgawanyiko wa mawazo ya muundo wa Katiba pamoja na mchakato wake.

Tofauti za Kidini zimeanza kuongezeka na zinakuwa kwa kasi kubwa sana. Sasa hivi tuna Sekondari ambazo dini mbili hazichanganyiki, tuna chuo kikuu cha kiislamu ambacho wakristu hawaingii kusoma hapo. Kuna shule ya sekondari pale Iringa ya mwarabu wa ASAS ambayo sasa dini tu haitoshi, bila kuwa Mhindi au mwarabu huingii kusoma.

Shule hizi siyo seminari. Ni shule za kawaida na hakuna sababu ya kubagua dini au rangi ya mtu.

Wasiwasi wangu ni kwamba hali hiyo inawaonyesha vijana wetu kwamba hawastahili kuchangayika. Wanasoma ktk mazingira hayo na hata itakapofika ktk ajira hawataweza kuchanganyika.

Wapi tunakokwenda? Tunaowaita viongozi wanaiona hali hii au ni faraja kwao?
 
wewe ndo umegawanyika......ujinga tu...we hao waliogawanyika unawaona wapi mbon sisi mitaani tuko poa tu...au unaishi msikitin au kanisani nini..?
 
Leo ndio akili yako imefanya kazi!!!!

Mgawanyo ulikuwepo, upo ,utakuwepo mpaka wewe na mimi tutapoiacha dunia hii mbona huhoji kwa nini wewe ni muislamu au mkristo????!!!!

Wangapi wamefika chuo kikuu na mikopo inawasumbua kupata ili waendelee na masomo???!!!!!

Percent ngapi ya Watanzania wanapata maji ya bomba na umeme???!!!

Kina mama wanajifungulia chini wakati kuna watu hawataki kutibiwa nchini!!!!

Ubaguzi upo tu ila siku mtu akiumia kama wewe leo hii yamekukuta ndio unaanza kupiga kelele na mayowe!!!!!!

A common enemy is still engulfing us
 
Yeah, Wanasema AMANi na Upendo Nchini uliletwa na MABABU zetu na sio Kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Kwanza baada ya UHURU

Wakaona ni BORA kulivunja AZIMIO LA ARUSHA ambalo lilikuwa linasheria za kuzuia hayo Matabaka...

Wewe Ukenda NAIROBI kuna sehemu ya WASOMALIA; WALUO; Wakikuyu ni MJI WAO...

Ukitembelea Miji yooote Tanzania hakuna hata Mmoja wenye ENEO ambalo ni KABILA MOJA au DINI MOJA tu Wanaishi...

Lakini Subiri kidogo; Na Viongozi wetu hawaongelei HAYA kwasababu HAWANA HEKIMA; Hawana ile Convincing Power ya Kusikilizwa kama NYERERE alivyo; Au kama BILL CLINTON alivyo USA
 
I have been reading a book about the Biafra War by Chimamanda Ngozi Adichie called 'Half of a Yellow Sun'. It has really opened up my eyes and what is happening now in Tanzania bears similarities to the beginning of the revolution in Nigeria. The revolution failed in Nigeria and many, many people lost there lives in the cause of the BIAFRA WAR.

The Biafra war was fought between 1967-70. Millions of people died and if you read the book you will have to take a break now and again to walk out and get a breath of fresh air to dry your tears and keep pinching yourself so as to bring yourself back to reality....(I experienced many sleepiness nights too).Be prepared by the graphic pictures that get imprinted in your mind!!. Forewarned is forearmed.

Many people starved to death, children died of kwashakor and malnutrition, young men were conscripted, they were very inhumane and raped young women to dull the pain that they themselves felt(I guess to numb their senses) for being part of the ugly war that they were forcefully asked to fight.

The Ibo tribe were targeted by the Hausa and Yoruba (mainly) for dominating the country's economy, civil service and business. It is really scary reading the book as I have seen too many similarities in what is happening in Tanzania today. The irony of it all is that the western countries fuelled the war in Nigeria for their own benefits...the questions to us Tanzanian should ask ourselves is..... What is the west after in our beloved country??. We don't have oil do we??.

The west send out the Red Cross to feed the displaced people with, cornmeal, egg York powder and powdered milk. However the really good stuff....goodies, where used to lure victims by relief staff, "Big men" and even shockingly some priests to have sex with women and young girls for exchange for treats such as crayfish, corned beef, salt and sugar which had become a luxury.

Please lets stop fuelling hatred amongst our own as it will get us absolutely NO WHERE!!.This is a war between the rich and poor and equality. Lets all address why this has happened and stop blaming each other. Lets try and progress towards a common goal...and embrace the Umoja spirit once again that built Tanzania. Lets pass a mabati, a brick a stone, an olive branch.. to each other regardless of Udini, rangi, tribe( or gender)and lets start building Tanzania again. The Biafrans were so engrossed in the plight of their own that they would say...IF THE SUN REFUSES TO RISE, WE WILL MAKE IT RISE. Does this ring a bell with some of the slogans we are seeing at the moment in Tanzania???.

Last but not least, the revolution of the Biafrans failed and their state failed and they had to be part of Nigeria again in order to survive!!. The Revolution failed the people. THOSE WHO DON'T LEARN FROM HISTORY ARE DOOMED TO REPEAT IT.
 
mkuu labda familia yako imegawanyika, unawajaza watu ,madudu hapa..
 
Mmbona mnakua waoga kiasi hicho na kuacha kujibu hoja? eti mtu unasema mbona hatujagawanyika wakati umeambiwa kuna shule na vyuo vya dini flan tu je huko sio kugawanyika? mtoa maada amesema kuna shule wanayo soma wahindi tu je huko siko kugawanyika? acheni unafki nyinyi hii nchi imegawanyika vipande viwili
 
mgawanyiko huo ulikuwepo tokea enzi za mkoloni na ukaendelea mpaka awamu ya nne hongera kwa kufunga leo na kuona hilo.
 
wewe ndo umegawanyika......ujinga tu...we hao waliogawanyika unawaona wapi mbon sisi mitaani tuko poa tu...au unaishi msikitin au kanisani nini..?

Unakoelekea unaweza ukataja unavyolawitiwa tofauti na wengine. Kama unakataa kwamba ubaguzi wa Kidini haupo, sema. Kama unasema hakuna ubaguzi wa rangi kwenye shule ya ASAS, sema. Au umeguswa kwenye tabia yako nini? Pole!

Leo ndio akili yako imefanya kazi!!!!

Mgawanyo ulikuwepo, upo ,utakuwepo mpaka wewe na mimi tutapoiacha dunia hii mbona huhoji kwa nini wewe ni muislamu au mkristo????!!!!

Wangapi wamefika chuo kikuu na mikopo inawasumbua kupata ili waendelee na masomo???!!!!!

Percent ngapi ya Watanzania wanapata maji ya bomba na umeme???!!!

Kina mama wanajifungulia chini wakati kuna watu hawataki kutibiwa nchini!!!!

Ubaguzi upo tu ila siku mtu akiumia kama wewe leo hii yamekukuta ndio unaanza kupiga kelele na mayowe!!!!!!

A common enemy is still engulfing us

Unakoelekea yaonekana utaniambia maisha yako ya ndani ya nyumba yanavyotofautiana na wengine ukidhani yanalingana na hayo niliyoandika. Upuuzi nisiyoutaka na ninao uzungumzia ni hayo niliyoyataja.

Kama huwezi kujadili au kuona ubaya wa ubaguzi wa kidini na rangi yako mwaka huu wa 2013, unathibitisha yaliyoandikwa na Aristotle hapo chini.
 
kugawanyika? kwa rangi, kabira,elimu, au dini? mgawanyiko huko pale pale tumeurithi kutoka kwa mababu zetu kwa hiyo hauwezi kuisha kwa hoja nyepesi au kwa maneno rahisi kama hivi. Mgawanyiko unaanzia kutofautiana katika ubora wa elimu,umasikini, na utajiri hii inatokana na pengo la kipato, mgawanyiko wa kiimani hiyo ni njaa tu inasumbua, uwezi kuwa tajiri sana ukaangaika na udini ukijua tu hali ikichafuka hata ulichonacho kitapotea.
 
Unakoelekea unaweza ukataja unavyolawitiwa tofauti na wengine. Kama unakataa kwamba ubaguzi wa Kidini haupo, sema. Kama unasema hakuna ubaguzi wa rangi kwenye shule ya ASAS, sema. Au umeguswa kwenye tabia yako nini? Pole!

Uoga wako wa kukabiliana na hali halisi hauwezi kubadili ukweli kuwa mpasuko upo siku nyingi ila mayowe huja kwa wingi pindi watu wa daraja la kati la kimaisha wanapobanwa wao!!!!!!

Watu wa daraja ya chini haya ni maisha yao ya kila siku na wala hajawahi kupiga kelele kama zako,wakati sisi tunalalamikia kodi ya simu kuna watu wanakula mlo mmoja!!!!!Hili halikuumi au sio mpasuko huu wakati wewe umejaza fridge????!!!! Selfish minded are blind

Wewe uko hapo unabofya tu kwa kuwa una uhakika wa maisha yako wakati kuna thread humu wanafunzi wanahaha kwa mikopo ya vyuo,umechangia hizo thread hata moja????!!!!!Usiogope ukweli mgawanyiko upo tayari!!!!!!

Petrol ikipanda bei sisi ni wa kwanza kulalama ilhali kuna watu hawajawahi kuona umeme,baiskeli ya kumtoa nyumbani mpaka shamba hana!!!!!Huo sio mgawanyiko umewahi kusikia wanalalamika kama wewe???!!!! ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA

We na umri wako hujui tatizo la madawati nchini??!!!Limekugusaje hili,watoto wako kama unao wanasoma shule hizi????!!Unashtuka mgawanyiko leo? Are you serious or hypocricy of the first order???!!!!

Mgawanyiko sio dini na rangi tu amka na utafakari kikomavu acha kulialia kwa sababu mgawanyiko wa safari hii unaathiri maisha yako!!!!!
 
Mleta mada ameleta jambo la maana sana,ingawa kuna watu hawataki kujua huo ukweli,lakini huko ndiko tulikofikia.Mbegu imeishapandwa,tusubiri mavuno yake.
 
Sasa tunatengeneza kambi za Al-shabab

Economic deprival and deeply rooted poverty is the root cause of militancy. Case in point militancy in Delta region and Boko Haram in Northern Nigeria. Rising inequality and poverty in Tanzania will surely sooner or later destroy social cohesion.
 
Inabagua serikali iliyojifungia na watu wa dini moja na kuwakatia mabilioni ya fedha kila mwaka ije iwe taasisi au raia wa kawaida?!
 
wewe ndo umegawanyika......ujinga tu...we hao waliogawanyika unawaona wapi mbon sisi mitaani tuko poa tu...au unaishi msikitin au kanisani nini..?

Unapaswa kuitwa siafu jike,kwani sjaona haja ya kumdhihaki mleta hoja.hiki kitendo cha ubaguzi wa kidi kipo na kinazidi kukomaa kwenye mashule kama unaakili timamu jiulize inakuwa vipi we ni mkiristo unalazimishwa kuingia mskitini kusali ilihali we sio mwislam?na vivyo hivyo kwa shule za kikatoriki mwanafunzi mwislamu analazimishwa kwenda kanisani na kusoma mafundisho ya biblia je hapo kuna haki ya kuabuda?serikali ipo inaimba kidumu chama cha mapinduz kila sku,imeshindwa kuilinda katiba na kuitetea kuhusu uhuru wa kuabudu,kwa mantiki hiyo kukiwa na watoto watano wa kislamu watatu wakristo wawili wanahtaji nafasi kwenye shule ya kikristo kipao mbele unadhani kitakuwa kwa nani?imefka sasa mtoto wa kislamu aogope kuvalia mavaz ya kidini pindi anapoenda kutafta nafasi kwenye shule za kikristo kwani ataambiwa nafasi haipo kabla hata ya kupewa kiti,ilinitokea mwenyewe sintasahau.
 
Huu uchambuzi wako ni wakizushi, uchochezi na Unafiki mkubwa sana. Na hizi ndo dalili za fikra jangwa na mawazo kame.
Hebu angalia majina yaliyotolewa na TCU kwaajili ya wanafunzi takaojiunga na MUM mwaka huu kama hakuna watu wa dini nyingine.
Halafu mbona unaonekana kuushambulia upande mmoja? Inamaana wewe unaziona taasisi za Kiislam tu!!? Hizo nyingine huna taarifa nazo au umetumwa.
Hata ufanyeje, amani tulonayo haitavujika kirahic!!?
MAMLUKI MKUBWA
 
Back
Top Bottom