Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 989
Taifa langu Tanzania lilianza kuonyesha mgawanyiko awamu ya tatu ya utawala chini ya rais Mkapa. Kikwete ndiye aliruhusu tukaona dhahiri mgawanyiko huu. Huku wazalendo wakihamasisha haki na uwajibikaji, maadili na utawala bora. Kule kikundi kidogo kikaanza kukiuka maadili, kupenda rushwa na ufisadi. Makundi haya yakashamiri. Kufikia 2010 kundi lenye ubinafsi wa kujilimbikizia Mali bila huruma ya jamii ya watanzania maskini walio wengi. Tukaona ni suala la fursa tu, ukiipata unaiba na kujilimbikizia na ukiwekwa kando unalalamikia kundi hilo. Hatimaye tukaanza kuamka tukiona jinsi tulivyogawanyika. Kundi kubwa likaanza kushambulia mafisadi na hawa waliokosa maadili. Katiba ikaandaliwa na Warioba tukaisifia. Kundi dogo likaendelea kutugawa. Katiba ikatupwa na tukavurugwa zaidi. Mungu akaleta neema kundi dogo likagawanyika. Wachache madarakani na wachache wakaja kundi la maadili na kuanza kutuaminisha wameongoka. Wakatukanwa walioko madarakani hadi tukaliamini kundi dogo lililomegeka. Tukahangaika kulisafisha na kumbe ikawa funzo. Waliobaki kule wakaanza kujisahihisha hadi wakampata Magufuli kama ajali. Sasa tuliovurugwa huku tukaanza kuona kundi dogo linajirekebisha. Je tuliamini tena? Tuungane nalo? Kundi letu nalo likiwa na hawa waliotoroka linazidi kubeza na kutokuamini mabadiliko ya kundi dogo madarakani. Akitumbuliwa tuliyekuwa tunamuona mwizi tunalalamika, tunamtetea kama mazuzu. Tukiona pesa imepatikana kwa makusanyo ya kodi tunabeza. Akiitwa Wema tunasema kidagaa, lakini akiitwa Gwajima tunadai kavunjiwa heshima. Tumegawanyika. Tukiona jema limetendwa na hawa waliojirekebisha tunakasirika. Tulipokuwa pamoja Lowasa akaitwa fisadi tukashangilia. Baadaye tukamsafisha lakini akakosa uraisi tukashangaa. Hata wenzetu kama Slaa nao tukawafurisha lakini sasa tukiambiwa bombadia zimekuja tunanuna. Nyumba zikijengwa kwa bilioni 10 UDSM hatuamini tunasema maigizo. Tumegawanyika. Hatupendi watende jema.
Baada ya hayo Neema inakuja. Kundi la waliojirekebisha linatuvuta. Hata likiamua kurudi na katiba ya Warioba hatutawaelewa. Lakini kidogokidogo tunaanza kuelewana. Tunataka maendeleo. Hatuwataki wavuta bangi/madawa hata wanaouza hata kama walitukopesha. Watanzania tubadilike. Tukiunga mkono juhudi za huyu aliyeanza kutafuta haki na uadilifu hata kama anakosea....tumuunge mkono na kumkosoa ili tusonge mbele. Wenzetu katika hili hawako nasi bali wanataka tuipige teke Neema.
Naipenda Tanzania. Simpendi fisadi hata kama alininunulia ubwabwa. Simpendi muuza madawa hata kama anaongoza taasisi yetu. Tushikamane tuliache kundi dogo liaibike