Mkuu kama tunajua hali ni hiyo,jee tukae tukilumbana na kusubiri hicho kipigo?
Vita ya ufisadi itaishaje wakati viongozi muhimu kama Waziri anayeshughulikia usalama wa Taifa Anasimama kibwebwe kutoa mipasho na ngebe kutetea ufisadi huko Dodoma? Hujamsikia Sophia? Usalama wa nchi hii uko mashakani. Hilo tulijue kabisaNikikumbuka ile vita ya Idi Amini..
Mola inusuru Tanzania na vita. Tuache kwanza mmalize hiyo vita ya UFISADI
Nimejiuliza sana swali hili bila majibu. Nisaidieni.
Mwaka 1978 tuliingia vitani na Uganda chini ya Idd Amin, lakini tulipambana kama Taifa vita ile kwa pamoja yaani viongozi wetu, makamanda, askari, Taasisi mbalimbali na Raia wote hadi tukashinda.
Sasa hivi hatuna tena maelewano ya aina ile. Tunachokiona ni uhasama kati Bunge na Serikali, Serikali na Raia wake, Taasisi na Taasisi na hata Askari na Raia. Ufisadi umeshika kasi ndani ya Taasisi muhimu za Umma kiasi kufikia kununua vifaa vya kijeshi vinavyodhaniwa kuwa viko chini ya kiwango (fake) hasa tukikumbuka vitu kama Helicopter zinazoanguka hovyo na mabomu yanayolipuka hovyo.
Jee kwa hali kama hiyo, ikitokea nchi jirani kushambulia mipaka yetu tunao uwezo wa kuhimili mapigo kama ule wa mwaka 1978 kama Taifa? Ama tutaita wawekezaji wa kijeshi kutulindia mipaka yetu huku sisi tukiendelea kupiga soga la malumbano?
Swali linazidi kuchukua nafasi hasa baada ya kusikia chokochoko za Malawi kwa mipaka yetu. Maana tukilemaa kesho tutasikia Rwanda anaitaka Ngara,Burundi anataka Kibondo na Kenya anautaka mlima Kilimanjaro.Bado swali hili najiuliza hadi leo na jibu sijapata.
nyie si mnasema Tanzania ni nchi ya Amani
amani yenyewe haipo zaidi ya viini macho
siombei vita mungu aepushe mbali cause tutakaoumia ni sisi wananchi wenye hali ya chini