Taifa ambalo punda wa masikini ni punda wa kweli na wanatumika kubeba mahitaji muhimu ya binadamu wakati huo huo punda wa mafisadi ni binadamu wenzao na wanatumika kubeba madawa ya kulevya.
Taifa ambalo linaendeshwa Kwa matukio hili kuwapumbaza raia wake.
Taifa la wananchi wavumilivu duniani mpaka majirani zetu wanatushangaa.
Taifa la watu wanafiki kuwahi kutokea,kwani kabla ya uchaguzi wananchi wanaonekana kuwa na ari ya kuleta Mabadiliko lakini wakati wa uchaguzi wanachagua chama kilekile wanachokilalamikia Kwa umaskini na shida zao
Taifa ambalo wananchi elfu ishirini wanaporwa ardhi na serikali na kupewa mzungu bureeeeee. Taifa ambalo wachimbaji wadogo wanaporwa machimbo yanapewa wazungu. Hakika haya mawili yanaweza kuleta machafuko.
Taifa lenye watu wengi wanaojua vyanzo vya matatizo ya nchi ila wanaishia kunyoshea kidole kwa viongozi wakati mabadiliko yanaanza kwa mtu mmoja tena bila kujali wa pembeni yako atabadilika au laa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.