TAHLISO nimeona kauli yenu ila napenda kujibu hivi

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
TAHLISO nimeona kauli yenu ila napenda kujibu hivi.

TSNP ni non-profit organization, ni Civil society .sio tawi la serikali,wala sio tawi la chama cha siasa .kazi yetu kubwa ni kutetea haki na wajibu wa wanafunzi nchi nzima.Tupo registered kihalali.tunatetea wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu na kusisitiza watimize wajibu wao.

Hatulipwi hata cent na wanafunzi ila tumekuwa mstari wa mbele kuwapigania kuanzia maswala ya udahili hadi mikopo ,nyinyi mnaojiita viongozi wa wanafunzi vyuo vikuu mlisimama lini kuwasemea ? .

Kazi yetu kubwa ni Ku advocate,Ku shauri,kusemea na Ku lobby ili haki za wanafunzi ziheshimiwe.Tofauti kubwa TSNP na TAHLISO.

TSNP ni non-governmental organization TAHLISO ni governmental organization. (TSNP sio tawi la serikali ,TAHLISO ni tawi la serikali).

TSNP hailipwi na wanafunzi wala serikali ,TAHLISO inalipwa na uongozi wa serikali za wanafunzi kila mwaka,pia hulipwa na serikali.

TSNP huwatetea ,hushauri,hukosoa na kupendekeza ili haki za wanafunzi ziheshimiwe ,TAHLISO huishia kusifia tuu serikali na kukinzana na matakwa ya wanafunzi.

TSNP hujihusisha na wanafunzi kuanzia Shule ya msingi hadi chuo kutetea haki zao,TAHLISO ni vyuo vikuu tuu kwa njia ya makongamano ,seminars na kugawana posho.

Mfano,halisi leo mmejitokeza kupinga kauli ya TSNP juu ya kifo cha Aquilin kupigwa Risasi ,kuwa nyinyi ndio mnakibali cha kusemea shida na maswala ya wanafunzi,kwani TAHLISO ni lini mmeanza kusemea matatizo ya wanafunzi hadi leo mjinasibu hivyo?

Wanafunzi walipata shida Udahili mlikuwa wapi?

Wanafunzi walipata shida mikopo mlikuwa wapi?

Wanafunzi walipata shida AVN mlikuwa wapi?

TAHLISO hata siku moja hamtaweza kusemea shida za wanafunzi,ikiwa bado ktk bawa na kwapa la serikali!

TAHLISO aliondoka nayo Paul Makonda,ile ndio ilikuwa TAHLISO ,TSNP haiwezwi kusita kutekeleza majukumu yake ,TSNP haina maslahi ,TAHLISO ina Maslahi na TSNP haiwezi shindana na TAHLISO timizeni wajibu wenu tusiingiliane sababu TSNP haijafunja wala kukeuka sheria.

Abdul Nondo.
 
Tahliso aliondoka nayo makonda tena!? Kivp mufti!? Makonda naye ana historia ipi ikiyotukuka tahliso!? Naomba ufafanuzi wa hoja, haja na mifano kaka!?
Vingnevyo ntatoa shilingi yangu
 
Ningependa kushauri uongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu usiwe wa kada kabisa. Maana ukada huu sijui utaishia wapi maana wengine hatuna ushawishi wa kuwa wanasiasa hivyo tukiona wanachuo wanamitazamo ya kisiasa naona kama wanajichulia kupotea.
 
Term hii TLS ndo imebaki kusikika wengine wapo njombe wamefunikwa blankets wapate joto
 
Nikiwa mmoja wa wahasisi wa TAHLISO pale UCLAS wakati wa mgomo wa bodi ya mikopo wizara ikiwa chini ya Pius Ng'wandu nillioona ikipoteza dira siku Ile ile. Nikaondoa kabisa imani yangu. Vyote vivunjwe tu Nadhani.
 
Back
Top Bottom