TAHARIRI: Miili Iliyopatikana Ruvu Ifukuliwe; Ben Saanane apatikane - Ni Utu Huu!

Tahariri hii imetoka gazeti la Zama Mpya

BEN-SAANANE-e1481561687834.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya ahadi za TANU ilikuwa ni ile iliyosema “Binadamu wote ni sawa” na pia “kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”. Ahadi hizi baadaye ziliingizwa pia kwenye Katiba yetu kama sehemu ya Haki za Msingi (Bill of Rights).

Kimsingi, kanuni hizi zinatuambia kuwa tunaweza kuwa na tofauti nyingi sana baina yetu, kuanzia zile za kidini, kisiasa, rangi, lugha, asili ya kitaifa n.k. Lakini mwisho wa yote sisi sote kama binadamu ni “sawa”. Usawa huu hauko katika masuala ya kisheria, hali, hadhi, ujiko, ukwasi n.k bali ni usawa unaotokana na ubinadamu wetu. Kwamba sisi sote kama binadamu tumeumbwa sawa na utu wetu wote ni sawa. Hakuna mwenye utu zaidi ya mwingine!

Taarifa za kupatikana miili ya watu saba ambao inadaiwa walikuwa wamefungwa kwenye viroba wakiwa na dalili za kuwa wameteswa au kuumizwa ni taarifa ambazo zinapasa kumshtua kila mtu anayejiona yeye ni binadamu. Katika usawa wetu wa kibinadamu tunajikuta tunaitwa siyo tu kuhoji lakini pia kupaza sauti kwa niaba ya binadamu wenzetu hao ili kutaka haki juu yao itendeke.

Bahati mbaya taarifa hizi pia zimehusishwa na kutoweka kwa miongoni mwa vijana wanaharakati Bw. Ben Saanane ambaye hajaonekana kwa muda sasa. Ninasema ni bahati mbaya kwa sababu Ben Saanane amekuwa akijihusisha na masuala ya kisiasa na hata ukosoaji wa viongozi walioko madarakani. Kutoonekana kwake katika kipindi kile kile ambacho miili hii imepatikana na kuzikwa kwa kile ambacho watu wanaona kama ni ‘haraka haraka’ kunawafanya watu wahisi labda kijana huyu ni miongoni mwa watu hao.

Binafsi naamini kwanza kabisa hata kama Ben Saanane angekuwa hajakosekana kama hivi na kama angekuwa anaendelea na shughuli zake bado kupatikana kwa miili hiyo kungetusukuma kutaka kujua ni nini kinaendelea, kwanini na na ni nani anahusika.

Kuna mambo kadhaa ambayo ni kweli. Kwamba, hao watu hawakujifunga wenyewe kwenye viroba lakini pia ni vigumu kuamini kama walijitumbukiza wenyewe wakiwa kwenye viroba kwenye mto Ruvu. Hili kimantiki haliwezekani. Ni wazi kuna binadamu wengine walihusika katika kufanya hili – la kuwafunga kwenye viroba na kuwatumbukiza mtoni. Na kama ni kweli watu hao walikuwa wameuawa kabla ya kufungwa au kutupwa mtoni basi ni wazi pia kuwa kuna watu walihusika na mauaji hayo.

Ni kwa sababu hiyo naweza kusema kuwa ni ukosefu mkubwa wa hekima na weledi kwa chombo chochote cha umma kutokufuata taratibu za msingi za kiutu za kushughulikia watu hao. Baada ya miili kukutwa ikielea jambo kubwa na la msingi kufanyika – kwa taratibu za kisheria na kawaida kabisa – ni kutaka kujua kwanza hao ni kina nani, walikufa vipi, na kwanini wapatikane eneo moja, na ni nani anahusika.

Maelezo ambayo yametolewa yenye kuashiria kuwa hawa ni “wahamiaji haramu” yanazua maswali mengi zaidi kuliko yanayojibu. Kama Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Mwigulu Nchemba anajua kuwa hawa ni wahamaiji haramu basi ni muhimu kwenda mbele zaidi na kujibu maswali zaidi badala ya kuyaacha yaning’inie hewani kama mzoga uliooza. Yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani bila ya shaka atakuwa na majibu ya maswali yote haya. Hawa ni wahamiaji kutoka nchi gani na walijuaje? Je, ni kwanini waliuawa? Je, majina yao ni kina nani? Je, ni nani walihusika na ama mauaji yao au kuwatumbukiza mtoni?

Kama nilivyosema awali hawa ni binadamu; utu wao haujadiliki kwani binadamu wote ni ‘sawa’ na wote wana utu sawa. Hata adui bado ni binadamu. Hata mtu unayemchukia bado ni binadamu. Kanuni hii ya msingi iliyoliunda taifa letu haipaswi kupotezwa au kudharauliwa na yeyote.

Lakini swali la msingi na muhimu ni je Serikali iko tayari kuacha vyombo huru kufanya uchunguzi wa miili hiyo ili kujiridhisha kuwa hawa siyo Watanzania na raia wa Tanzania ambao wanalindwa na sheria mbalimbali za nchi yetu?

Binafsi naamini ili kuondoa hisia kuwa serikali ama inahusika – moja kwa moja au kwa namna moja – na tukio hili ni vizuri kwanza kabisa miili yote ifukuliwe, ifanyiwe uchunguzi wenye kushirikisha watu huru, na hatimaye taarifa itolewe (post mortem) ili kutoa wasiwasi wowote ambao unaweza kuonekana umeingia kwa wananchi.

Lakini pia, ni jukumu la vyombo vyote vya serikali ikiwemo TISS, Polisi na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha kijana Ben Saanane anapatikana kwani kutokupatikana kwake kunaleta ubaridi katika harakati za kisiasa nchini. Hii ni kwa sababu kama miili ya watu hao ni kazi ya kundi la kihalifu nchini na kutokujulikana au kupatikana kwa kundi hilo kunaweza kutumiwa kisiasa kuonesha kuwa serikali inaanza au taasisi zake zinaanza kufanya kile ambacho kimeshuhudiwa huko Burundi na Rwanda na kwenye baadhi ya nchi ambazo siasa zake hazijali sana haki za raia au zile haki za kibinadamu. Ni kwa maslahi ya serikali kumpata Ben Saanane.

Ni matumaini yangu, kuwa serikali yetu itafanya yote yanayopaswa ili kuondoa wingu la hofu ambalo linaweza kufanya watu wahofie serikali yao. Kupatikana kwa Ben Saanane na kufanyiwa uchunguzi kwa miili iliyopatikana Ruvu ndio njia pekee ya kuzidi kuonesha kuwa serikali ya Awamu ya Tano inajali wanyonge na wale wasio na watetezi hata kama watu hao ni wahamiaji au wanasiasa wa upinzani au wale ambao wanawakera au wanaoweza kuwaona kuwa ni maadui wao.

Nje ya hapo maswali yanayoulizwa sasa hayatakoma na yatapaswa kuulizwa na kutakiwa kujibiwa siku moja. Hata kama siku hiyo itachelewa. Na majibu yake yatakapopatikana wahusika wote bila kujali vyeo vyao vya sasa, hadhi zao za sasa, au kile wanachoweza kuamini kuwa ni kinga za sasa siku moja wataitwa kujibu mbele ya Watanzania, na mbele ya Mungu.
Tuache na maumivu yetu.

Kebehi sio kitu chema
 
M
Inasemekana hatua zote muhimu ili kupatiwa ripoti ya mawasiliano yake ya simu hiyo siku ametoweka zimefuatwa lakini cha kustaajabisha kampuni husika ya simu inachelewesha hiyo ripoti bila sababu zozote.

Who is behind all that?mimi na wewe watazamaji tu.
Mkuu you are trying to feed into the conspiracy theory.
Kwa vyombo vya dola kupata transcripts za communications za mtu yeyote ni swala dogo kabisa.
Kampuni ya simu yoyote haina ubavu wa kukataa kutoa hizo transcripts kwa vile polisi wanazifuatilia baada ya kupata court order.
 
mtoa mada ni kundi lilelile tu,katumwa na anatumika,amekuwa akiunga mkono hizi sera kwa maandishi,na maandishi yake yamezaa haya,eti sasa naye kaja analia,kweli si kila anayelia msibani analia kwa uchungu,wengine wanatoa machozi msibani kwa kufurahishwa na tukio
Hii dhana kwamba ukiunga mkono mtu/chama/serikali huna tena haki ya kukosoa imetengeneza majuha wengi sana nchini.
Majuha yamejaa kwenye vyama,yamejaa mitaani na yamejaa serikalini yakiwa na kazi moja tu ya kuunga mkono.Majuha ya watu katu hayakosoi watu wao.Majuha ya vyama katu hayakosoi vyama vyao.Na majuha ya serikali katu hayakosoi serikali yao.
Wewe upo kwenye hayo makundi.
 
Kutaka serikari ichunguze sio tatizo, lakini kuanza kuishutumu ndio tatizo.

Kapotea so far that is known, how? lichunguzwe.

Lakini sio kuhitimisha na vitu ambavyo havina ata historical logic or behaviour za serikari towards politicians.
Naomba isiwe ni viongozi wa kisiasa ama wa upinzani au tawala kutafuta stori mpya ya kuichafua serikali,

Nimekaa na haya mawazo yangu nikajukuta kama nakabwa koo vile
Kwa hili embu ngoja niyatoe yakinikost potelea mbali,

Naanza hivi:-
Inawezekana kama kweli saa nane kapotea ni pande mbili ndio zitahusika ambazo ni wahasimu kisiasa.
1. Uongozi kwa maana ya serikali
Vigezo vyangu
a) haiwezekani watu saba wapatikane halafu haraka haraka wazikwe kama wanyama kana kwamba ni wagonjwa wa ebora au ugonjwa wowote hatari,
b) tamko la mh. Waziri kuwa walozikwa ni wahamiaji haramu kwa maana ya wakimbizi, hiii haiharalishi kuwaondoa uhai wao hasa kwa kitendo cha kinyama, na sidhani kama kuna tamko lolote la kutafutwa kwa waliofanya hilo tukio
c) kuwanyima haki malehem hata kwa kutangazwa sura zao au hata kusubiri matangazo kutoka kwa barozi zilizoko nchini naamini wapewa taarifa picha zikawekwa wazi tukawatambua au wakatambulika na ndugu zao kokote waliko duniani

Mf:- hivi karibuni kuna mtanzania aliokolewa kutoka uarabuni kupitia video iliyozunguka kutafuta ndugu zake, hatimaye taarifa zikavuka mipaka mpaka tz akaokolewa kutoka kwenye mateso makali, kwa nini sisi tukute bin adam mwenzetu kafa hafu tunachukulia kirahisi hivi??
Mawazo ya wengi tunaweza sema hata saa nane yaweza akawa alikua miongoni mwao,

Ni kwa nini tuituhumu serikali??

Huyu ndie mtu alieweza kukosoa popote na wakati wowote pasipo na kupepesa macho, iwe kweli au si kweli yeye alisimamia kile anachokijua
Ikaonekana akipotea wengi watazima midomo walokuwa wanamfuata saa nane kwa mienendo yake.

2. VYAMA VYA UPINZANI ( UKAWA)
Vigezo vyangu
a)kutafuta tukio la kuwarudisha juu
Ikumbukwe kuwa toka uongozi huu uingie madarakani ni dhahili ukawa umepoteza dira hasa kwa kukosa pakuongelea,
Tumekua tukisikia hoja zao sio zile za kujisimamia wamebaki ni kusubiri matukio kama waandishi wa habari ili wasikike katika vyombo vya habari na pengine wasisahaurike kama wapo
Cha ajabu watu wamekua wakijipa moyo kuwa serikali itayamaliza, mf; bila kupepesa macho kwenye sakata la kiwanda cha dangote cha theruji tuliona walivolishangilia baada ya kiwanda kufungwa, kwenye tetemeko la kagera tuliona walivoyatafuta madhaifu ya serikali dhidi ya majanga.
Kwa hili inaonekana wazi kuwa wapinzani wamekuwa wakiliombea taifa majanga na pengine kuyatengeneza ili kuikosoa serikali.

b) kafara
Kutokana na hali mbaya kisiasa hasa za upinzani kwa mwendo kasi wa mh. Raisi inaonekana wazi uponzani unayumba hivyo inaweza kuamuliwa mtu atolewe kafara ili kupata pakuongelea kama waote tunavyoshuhudia japo ni kitendo cha kinyama na katika haya mambo yaweza kuwa kweli au si kweli.

c) kujitengenezea historia ya kishujaa, vyama pinzani vinatabia ya kutafuta historia ya kweli na ambayo kila anaeisoma imguse kweli kweli, mtu kama huyu akitolewa kama mfano katika chama hukuza jina na historia yake na ya chama pia, japo hua inapendeza ikitokea pale napofanya kwa masirahi ya taifa na watu wake kwa nia njema,
d) kuchafua serikali
Baada ya kugundua kua viongozi walioko madarakani kwa sasa na hata mawaziri waliowengi kujenga hoja ni kazi hasa za kwenye tuhuma kama hizi wengi hupendelea vitendo zaidi ili vilete tija kwa taifa zima, wao wanaitumia hii nafasi kuwamulika kwa wanainchi tuliojikuta tunawekeza mawazo yetu na fikra zetu kwa wanasiasa.

Baada ya kuongea yote hayo sasa najihisi huru na nimawazo yangu tu hakuna chanzo chocho wala mtu yeyote nyuma yangu nazungumza kulingana na mtazamo wangu katika hili swala gumu na zito katika taifa letu

Kama nikokinyume na matakwa ya watu natumia neno samahani
 
Haaaah bado kabisa haijaniingia kama Ben kafa.............

I will never accept that situation until this will be confirmed.....

Kama hii itakuwa imetokea kweli Tanzania tutakuwa tumeingia kwenye historia ya hovyohovyo tokea Uhuru.......

Mkuu hivi kwani umesahau ya kamanda Mawazo aliuliwa vipi na na kina nani?
 
Hivi Maiti iliyoibuliwa kwenye Maji ikiwa imeoza inaweza kuwekwa Juani au Kwenye Jokofu hata Dk 30?
 
it seems u know alot big bosssssssss
 
logical question..But nadhani huwezi kukosa specimen kwa ajili ya DNA
Hiyo Sawa sidhani kama Polisi wamezika bila kuchukua specimen kwa ajiri ya DNA ili kufikia hoja ya wahamiaji haramu, kumbuka kila Mara wanakufa hawa watu ilikua kwenye container sasa kwenye maji.
Biashara hii ya Trafficking ni kubwa na inalipa sana.
 
The minister was not supposed to give such statements

Angesema tu uchunguzi wa kina unafanyika ingeeleweka

Uhai wa mtu ni kitu cha muhimu kuliko yote
 
Tahariri hii imetoka gazeti la Zama Mpya

BEN-SAANANE-e1481561687834.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya ahadi za TANU ilikuwa ni ile iliyosema “Binadamu wote ni sawa” na pia “kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”. Ahadi hizi baadaye ziliingizwa pia kwenye Katiba yetu kama sehemu ya Haki za Msingi (Bill of Rights).

Kimsingi, kanuni hizi zinatuambia kuwa tunaweza kuwa na tofauti nyingi sana baina yetu, kuanzia zile za kidini, kisiasa, rangi, lugha, asili ya kitaifa n.k. Lakini mwisho wa yote sisi sote kama binadamu ni “sawa”. Usawa huu hauko katika masuala ya kisheria, hali, hadhi, ujiko, ukwasi n.k bali ni usawa unaotokana na ubinadamu wetu. Kwamba sisi sote kama binadamu tumeumbwa sawa na utu wetu wote ni sawa. Hakuna mwenye utu zaidi ya mwingine!

Taarifa za kupatikana miili ya watu saba ambao inadaiwa walikuwa wamefungwa kwenye viroba wakiwa na dalili za kuwa wameteswa au kuumizwa ni taarifa ambazo zinapasa kumshtua kila mtu anayejiona yeye ni binadamu. Katika usawa wetu wa kibinadamu tunajikuta tunaitwa siyo tu kuhoji lakini pia kupaza sauti kwa niaba ya binadamu wenzetu hao ili kutaka haki juu yao itendeke.

Bahati mbaya taarifa hizi pia zimehusishwa na kutoweka kwa miongoni mwa vijana wanaharakati Bw. Ben Saanane ambaye hajaonekana kwa muda sasa. Ninasema ni bahati mbaya kwa sababu Ben Saanane amekuwa akijihusisha na masuala ya kisiasa na hata ukosoaji wa viongozi walioko madarakani. Kutoonekana kwake katika kipindi kile kile ambacho miili hii imepatikana na kuzikwa kwa kile ambacho watu wanaona kama ni ‘haraka haraka’ kunawafanya watu wahisi labda kijana huyu ni miongoni mwa watu hao.

Binafsi naamini kwanza kabisa hata kama Ben Saanane angekuwa hajakosekana kama hivi na kama angekuwa anaendelea na shughuli zake bado kupatikana kwa miili hiyo kungetusukuma kutaka kujua ni nini kinaendelea, kwanini na na ni nani anahusika.

Kuna mambo kadhaa ambayo ni kweli. Kwamba, hao watu hawakujifunga wenyewe kwenye viroba lakini pia ni vigumu kuamini kama walijitumbukiza wenyewe wakiwa kwenye viroba kwenye mto Ruvu. Hili kimantiki haliwezekani. Ni wazi kuna binadamu wengine walihusika katika kufanya hili – la kuwafunga kwenye viroba na kuwatumbukiza mtoni. Na kama ni kweli watu hao walikuwa wameuawa kabla ya kufungwa au kutupwa mtoni basi ni wazi pia kuwa kuna watu walihusika na mauaji hayo.

Ni kwa sababu hiyo naweza kusema kuwa ni ukosefu mkubwa wa hekima na weledi kwa chombo chochote cha umma kutokufuata taratibu za msingi za kiutu za kushughulikia watu hao. Baada ya miili kukutwa ikielea jambo kubwa na la msingi kufanyika – kwa taratibu za kisheria na kawaida kabisa – ni kutaka kujua kwanza hao ni kina nani, walikufa vipi, na kwanini wapatikane eneo moja, na ni nani anahusika.

Maelezo ambayo yametolewa yenye kuashiria kuwa hawa ni “wahamiaji haramu” yanazua maswali mengi zaidi kuliko yanayojibu. Kama Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Mwigulu Nchemba anajua kuwa hawa ni wahamaiji haramu basi ni muhimu kwenda mbele zaidi na kujibu maswali zaidi badala ya kuyaacha yaning’inie hewani kama mzoga uliooza. Yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani bila ya shaka atakuwa na majibu ya maswali yote haya. Hawa ni wahamiaji kutoka nchi gani na walijuaje? Je, ni kwanini waliuawa? Je, majina yao ni kina nani? Je, ni nani walihusika na ama mauaji yao au kuwatumbukiza mtoni?

Kama nilivyosema awali hawa ni binadamu; utu wao haujadiliki kwani binadamu wote ni ‘sawa’ na wote wana utu sawa. Hata adui bado ni binadamu. Hata mtu unayemchukia bado ni binadamu. Kanuni hii ya msingi iliyoliunda taifa letu haipaswi kupotezwa au kudharauliwa na yeyote.

Lakini swali la msingi na muhimu ni je Serikali iko tayari kuacha vyombo huru kufanya uchunguzi wa miili hiyo ili kujiridhisha kuwa hawa siyo Watanzania na raia wa Tanzania ambao wanalindwa na sheria mbalimbali za nchi yetu?

Binafsi naamini ili kuondoa hisia kuwa serikali ama inahusika – moja kwa moja au kwa namna moja – na tukio hili ni vizuri kwanza kabisa miili yote ifukuliwe, ifanyiwe uchunguzi wenye kushirikisha watu huru, na hatimaye taarifa itolewe (post mortem) ili kutoa wasiwasi wowote ambao unaweza kuonekana umeingia kwa wananchi.

Lakini pia, ni jukumu la vyombo vyote vya serikali ikiwemo TISS, Polisi na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha kijana Ben Saanane anapatikana kwani kutokupatikana kwake kunaleta ubaridi katika harakati za kisiasa nchini. Hii ni kwa sababu kama miili ya watu hao ni kazi ya kundi la kihalifu nchini na kutokujulikana au kupatikana kwa kundi hilo kunaweza kutumiwa kisiasa kuonesha kuwa serikali inaanza au taasisi zake zinaanza kufanya kile ambacho kimeshuhudiwa huko Burundi na Rwanda na kwenye baadhi ya nchi ambazo siasa zake hazijali sana haki za raia au zile haki za kibinadamu. Ni kwa maslahi ya serikali kumpata Ben Saanane.

Ni matumaini yangu, kuwa serikali yetu itafanya yote yanayopaswa ili kuondoa wingu la hofu ambalo linaweza kufanya watu wahofie serikali yao. Kupatikana kwa Ben Saanane na kufanyiwa uchunguzi kwa miili iliyopatikana Ruvu ndio njia pekee ya kuzidi kuonesha kuwa serikali ya Awamu ya Tano inajali wanyonge na wale wasio na watetezi hata kama watu hao ni wahamiaji au wanasiasa wa upinzani au wale ambao wanawakera au wanaoweza kuwaona kuwa ni maadui wao.

Nje ya hapo maswali yanayoulizwa sasa hayatakoma na yatapaswa kuulizwa na kutakiwa kujibiwa siku moja. Hata kama siku hiyo itachelewa. Na majibu yake yatakapopatikana wahusika wote bila kujali vyeo vyao vya sasa, hadhi zao za sasa, au kile wanachoweza kuamini kuwa ni kinga za sasa siku moja wataitwa kujibu mbele ya Watanzania, na mbele ya Mungu.
Salaam,Mzee Mwanakijiji.Naona sasa umerejeshewa ID na password yako.
 
Naomba isiwe ni viongozi wa kisiasa ama wa upinzani au tawala kutafuta stori mpya ya kuichafua serikali,

Nimekaa na haya mawazo yangu nikajukuta kama nakabwa koo vile
Kwa hili embu ngoja niyatoe yakinikost potelea mbali,

Naanza hivi:-
Inawezekana kama kweli saa nane kapotea ni pande mbili ndio zitahusika ambazo ni wahasimu kisiasa.
1. Uongozi kwa maana ya serikali
Vigezo vyangu
a) haiwezekani watu saba wapatikane halafu haraka haraka wazikwe kama wanyama kana kwamba ni wagonjwa wa ebora au ugonjwa wowote hatari,
b) tamko la mh. Waziri kuwa walozikwa ni wahamiaji haramu kwa maana ya wakimbizi, hiii haiharalishi kuwaondoa uhai wao hasa kwa kitendo cha kinyama, na sidhani kama kuna tamko lolote la kutafutwa kwa waliofanya hilo tukio
c) kuwanyima haki malehem hata kwa kutangazwa sura zao au hata kusubiri matangazo kutoka kwa barozi zilizoko nchini naamini wapewa taarifa picha zikawekwa wazi tukawatambua au wakatambulika na ndugu zao kokote waliko duniani

Mf:- hivi karibuni kuna mtanzania aliokolewa kutoka uarabuni kupitia video iliyozunguka kutafuta ndugu zake, hatimaye taarifa zikavuka mipaka mpaka tz akaokolewa kutoka kwenye mateso makali, kwa nini sisi tukute bin adam mwenzetu kafa hafu tunachukulia kirahisi hivi??
Mawazo ya wengi tunaweza sema hata saa nane yaweza akawa alikua miongoni mwao,

Ni kwa nini tuituhumu serikali??

Huyu ndie mtu alieweza kukosoa popote na wakati wowote pasipo na kupepesa macho, iwe kweli au si kweli yeye alisimamia kile anachokijua
Ikaonekana akipotea wengi watazima midomo walokuwa wanamfuata saa nane kwa mienendo yake.

2. VYAMA VYA UPINZANI ( UKAWA)
Vigezo vyangu
a)kutafuta tukio la kuwarudisha juu
Ikumbukwe kuwa toka uongozi huu uingie madarakani ni dhahili ukawa umepoteza dira hasa kwa kukosa pakuongelea,
Tumekua tukisikia hoja zao sio zile za kujisimamia wamebaki ni kusubiri matukio kama waandishi wa habari ili wasikike katika vyombo vya habari na pengine wasisahaurike kama wapo
Cha ajabu watu wamekua wakijipa moyo kuwa serikali itayamaliza, mf; bila kupepesa macho kwenye sakata la kiwanda cha dangote cha theruji tuliona walivolishangilia baada ya kiwanda kufungwa, kwenye tetemeko la kagera tuliona walivoyatafuta madhaifu ya serikali dhidi ya majanga.
Kwa hili inaonekana wazi kuwa wapinzani wamekuwa wakiliombea taifa majanga na pengine kuyatengeneza ili kuikosoa serikali.

b) kafara
Kutokana na hali mbaya kisiasa hasa za upinzani kwa mwendo kasi wa mh. Raisi inaonekana wazi uponzani unayumba hivyo inaweza kuamuliwa mtu atolewe kafara ili kupata pakuongelea kama waote tunavyoshuhudia japo ni kitendo cha kinyama na katika haya mambo yaweza kuwa kweli au si kweli.

c) kujitengenezea historia ya kishujaa, vyama pinzani vinatabia ya kutafuta historia ya kweli na ambayo kila anaeisoma imguse kweli kweli, mtu kama huyu akitolewa kama mfano katika chama hukuza jina na historia yake na ya chama pia, japo hua inapendeza ikitokea pale napofanya kwa masirahi ya taifa na watu wake kwa nia njema,
d) kuchafua serikali
Baada ya kugundua kua viongozi walioko madarakani kwa sasa na hata mawaziri waliowengi kujenga hoja ni kazi hasa za kwenye tuhuma kama hizi wengi hupendelea vitendo zaidi ili vilete tija kwa taifa zima, wao wanaitumia hii nafasi kuwamulika kwa wanainchi tuliojikuta tunawekeza mawazo yetu na fikra zetu kwa wanasiasa.

Baada ya kuongea yote hayo sasa najihisi huru na nimawazo yangu tu hakuna chanzo chocho wala mtu yeyote nyuma yangu nazungumza kulingana na mtazamo wangu katika hili swala gumu na zito katika taifa letu

Kama nikokinyume na matakwa ya watu natumia neno samahani
Mkuu wewe ulitaka maiti iliyooza kwa kukaa majini ikae siku ngapi mortuary, hebu tupe uzoefu wako.
Tatizo lako ni kuhusisha tukio na serikali, as if walikuwepo wakati hao jamaa walipouwawa/kufa na kushonewa sanda ya kiroba.
Huna evidence yoyote kutu convince hivyo.

Inawezekana kabisa Saanane ni ndugu yako, lakini hii isiwe sababu ya kupata mihemuko isiyo na maana kulaumu wengine kwa kupotyyea huyu jamaa.
Mbaya Zaidi mawazo yako yameelekea kujenga hoja zisizo na mashiko ,kwamba hiyo miili mmoja ni wa Saanane.
Kama hivyo ni kweli upande wako, huzuiwi kupata amri ya mahakama kufukua miili na kuifanyia postmortem.
Ndo jukumu lako kama ndugu.
 
Tanzania HAIJAWAHI WALA HAITAWAHI KUA NA SIASA ZA AINA HII! Nawaombeni kuwa na subira na kuacha kutengeneza mazingira ya Taharuki kwa jamii! Tafadhali sana!
KASSIM HANGA NA OTHMAN SHARIF si walikuwa waajiriwa wa serikali ya jamhuri ya muungano walipotezwa hivi hivi
 
Mkuu wewe ulitaka maiti iliyooza kwa kukaa majini ikae siku ngapi mortuary, hebu tupe uzoefu wako.
Tatizo lako ni kuhusisha tukio na serikali, as if walikuwepo wakati hao jamaa walipouwawa/kufa na kushonewa sanda ya kiroba.
Huna evidence yoyote kutu convince hivyo.

Inawezekana kabisa Saanane ni ndugu yako, lakini hii isiwe sababu ya kupata mihemuko isiyo na maana kulaumu wengine kwa kupotyyea huyu jamaa.
Mbaya Zaidi mawazo yako yameelekea kujenga hoja zisizo na mashiko ,kwamba hiyo miili mmoja ni wa Saanane.
Kama hivyo ni kweli upande wako, huzuiwi kupata amri ya mahakama kufukua miili na kuifanyia postmortem.
Ndo jukumu lako kama ndugu.

Maskini pengine hujui hata wajibu & kazi za serikali (dola)!

Aidha sijui hata kama umemsoma mleta mada pamoja na huyu ndugu uliyekwoti andiko lake kwa pamoja ukawaelewa

Hebu rudia tena kusoma pengine ukawaelewa.

Na labda ngoja nikusaidie kidogo;

Suppose, yeyote akapata court order ya mahakama kwamba marehemu hao wakafukuliwe huko walikozikwa ili kufanya uchunguzi na pengine kuweza kutambuliwa kwa hao marehemu, ni nani atakuwa ameumbuka hapo?

Jibu la moja kwa moja ni serikali kupitia kitengo cha jeshi la polisi na kwa lugha nyingine ni kwamba tutarudi kwenye hoja ya msingi ya mleta mada.....wajibu wa dola kwa raia wake....kwamba pamoja na mengine ni kulinda usalama (uhai) wa watu wake na yeyote aliyeko katika nchi husika wakiwemo wahamiaji haramu!!

Siyo lazima kamwe hiyo miili mmoja uwe wa Ben Saanane. Muhimu ni serikali kupitia vyombo kutambua wajibu wake!!

Na pia si kosa watu kujenga assumptions za namna hiyo, kwamba, labda ktk hao waliozikwa kinyama baada ya kuwawa kinyama mmoja wao ni Ben Saanane huyu anayesemekana amepotea mpaka sasa!!

Yes, si serikali yenyewe imejenga ama kutengeneza mazingira ya watu kufikiria hivyo? Au wewe huoni hilo?

Na mwisho nikuulize hivi, ni kipi bora na muhimu kwa serikali ingepaswa kufanya?

Kui - treat miili iliyooza na kuitunza hata ijiridhishe kuwa kweli haina wenyewe na kisha kuizika au kupitia songombingo hili ikalazimishwe kuifukua tena toka kaburini ili kufanya uchunguzi?
 
Haaaah bado kabisa haijaniingia kama Ben kafa.............

I will never accept that situation until this will be confirmed.....

Kama hii itakuwa imetokea kweli Tanzania tutakuwa tumeingia kwenye historia ya hovyohovyo tokea Uhuru.......
Kila Binadamu ana haki ya kuishi.Ipo siku ukweli utajulikana hata kama ni baada ya karne nzima.
 
Back
Top Bottom