TAHARIRI: Hili la kuchimba dawa Mh. Mwakyembe hajajipanga

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliliambia Bunge kuwa kuanzia Septemba mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kwa mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi kusimama vichakani ili abiria wao wajisaidie haja kubwa na ndogo maarufu kama ‘kuchimba dawa’.
Mwakyembe alitoa agizo hilo mwezi uliopita wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara yake na kueleza madhara yanayotokana na vitendo hivyo vya kuchimba dawa vichakani.
Kwanza, Dk. Mwakyembe alisema ni kitendo cha udhalilishaji kisaikolojia, hasa kwa wanawake, kuvua nguo hadharani mbele za watu wakiwamo watoto wao ili kujisaidia.
Pili, akafafanua kwamba mbali na kadhia hiyo, pia ni hatari kwa usalama wa abiria hao kwani huko wanakopelekwa kujisaidia si sehumu salama, wanaweza kukumbana na wanyama wakali wakiwamo nyoka hivyo kudhurika.
Tatu na kubwa, Waziri Mwakyembe alisema vitendo hivyo vinaharibu mazingira, hivyo kuhatarisha usalama wa afya za wakazi wanaoishi jirani na maeneo husika, na kwamba serikali haiwezi kuvumilia kuendelea kukaa kimya.
Tunampongeza Waziri Mwakyembe kwa kuliona hilo pamoja na nia njema ya kutaka kulipatia ufumbuzi, lakini tunadhani amri yake imewahi sana kabla ya kujipanga kuweka mazingira rafiki ya kufawanya abiria wasijisaidie vichakani.
Tunadhani ipo haja ya wizara yake kushirikiana na wenye mabasi yaendayo mikoani, kuhakikisha vinajengwa vyoo vya umma katika maeneo mbalimbali kutegemeana na urefu wa njia ambavyo vitawekewa usimamizi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kufanyiwa usafi.
Vyoo hivi vinaweza kujengwa jirani na vituo vya kuuzia mafuta vilivyopo jirani na barabara au karibu na makazi ya watu halafu vikakabidhiwa kwenye usimamizi wa uongozi wa eneo hilo na wenye magari pamoja na serikali wakawa wanachangia gharama za matunzo na usafi.
Baada ya hatua hizo kufanyika ni rahisi sana agizo la Waziri Mwakyembe kutekelezeka kwani kutakuwa na mbadala wa vichaka, abiria nao hawawezi kukubali tena kupelekwa huko wakati wanajua vipo vyoo mahala fulani.
Jambo hili linapaswa kufanyika upesi kwani tumechelewa kuondokana na aibu hii ya kujisaidia vichakani wakati huu wa sanyansi na teknolojia ambapo dunia inakazana kutokomeza magonjwa yanayotokana na uchafu, sisi ndiyo kwanza tunahamasishana kuchafua mazingira.
Hivyo basi tupo sambamba na Waziri Mwakyembe, tunakubaliana naye kuwa ana nia njema na lengo zuri kwa manufaa ya nchi, lakini kamwe asije akarudi nyuma na kubakiza agizo lake kuwa kama matamko mengine ya mawaziri yasiyofanyiwa kazi.
Ni wazi kuwa mwanzoni vikwazo vitakuwa vingi lakini kamwe asikubali kuvunjika moyo, wenye magari ndio wadau wakubwa katika hilo, hivyo awashirikishe kwa asilimia kubwa.

CHANZO: Tanzania Daima
 
tatizo kuna watu wanapenda kula mno njiani bila kujua hata usafi wa anachokula,mf mtu anatoka moshi -dar kila basi likisimama anashuka kwenda kula ataacha kuchimba dawa kila kichaka, kukaa kutwa nzima bila kula utakufa? kwa mantiki hiyo vyoo vijengwe basi, kama mabasi yangeweka vyoo vya ndani kama ninayoyafaham ni vizuri sana maana haja ndogo unaji - help palepale tatizo kuchimba mzizi mkuu duh,,,,hapatakalika
 
Ni wazo na agizo zuri lakini maandalizi yanahitajika.
Jana nilipita kwa bus katika barabara ya Chalinze Moshi na pale mbele ya Msata kuna mizani na pamejengwa choo.
Choo kina matundu mawili upande wa wanaume (kwa wanwawake sina uhakika) lakini Mabasi mawili tu yalifanya watu wajisaidie nje.Pia mabomba ya maji ni mabovu na huwezi hata kunawa mikono.
 
Back
Top Bottom