Tahadhari za kuchukua kukabiliana na kimbunga cha JOBO

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Kaa karibu na nyumbani kuepuka hatari. Usisafiri wakati wa mvua au upepo kwa kuwa barabara huwa na hatari zaidi

Ingiza vitu hatarishi ndani, kwa kuwa ni hatari ikiwa upepo mkali ukivuma. Hakikisha una chakula cha kutosha ndani ya nyumba yako

Weka mafuta ya kutosha kwenye gari yako. Hakikisha simu yako na vifaa vingine vya umeme vina chaji ya kutosha muda wote

Andaa begi lenye vitu vyako muhimu ili uhame kirahisi itakapolazimika. Kimbunga cha JOBO kimetabiriwa kuikumba Tanzania April 26.
 
Sisi ni wabongo bana, hata huwa hatujali hayo mambo

Mwaka 2004 ilitokea tsunami huko Indonesia na pwani ya EA ikapata partial waves na kina cha maji kuongezeka zaidi, lakini sisi ndio kwanza tukaenda zetu huko ma beach kuona hiyo tsunami ndio ikoje ikoje
 
Tumuombe Mungu aiepushie mbali maana hii taarifa walibe pembezoni mwa bahari hindi wala hawana habari....
 
Kimbunga kinaonekana kitakuwa kimevurugwa maana kilitaka kufanana jina lake na yule mwenye faili lake milembe...
🚶🚶🚶
20210404016.jpg
 
Back
Top Bottom