kerubi afunikaye
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 1,183
- 1,061
Ninayeongea nanyi ni shuhuda mara mbili wa wizi husika.Kumetokea aina mpya ya wizi hapa jijini Dar ambapo mwizi hutumia aina fulani ya maji ambayo ukinyunyiziwa unabaki umeduwaa au unazimia.
Wiki tatu zilizopita jirani yangu mwenye biashara ya tigo pesa aliibiwa sh milioni 9 baada ya wezi hao kufika eneo lake la biashara na baada ya kumshika usoni mfanyakazi wake aliduwaa na wezi hao kubeba pesa zote.Hata hivyo wiki iliyopita wezi hao walikamatwa baada ya uchunguzi wa askari na kesi inaendelea.
Leo hii muda wa jioni nilipigiwa simu na staff mwenzangu akilia kwamba amerudi nyumbani na kukuta housegirl wake akiwa hoi huku tv,music system pamoja na fedha vikiwa vimeibiwa.
Nilikwenda huko na tukafuatilia na kugundua kuwa msichana huyo alikuwa akisumbuliwa kwa kutongozwa mara kwa mara na mtu asiyejuana naye vizuri kiasi cha kuzoeana hadi kumwelekeza nyumbani na alikuwa akija kumtembelea jamaa anapokuwa kenda kazini yeye na mkewe na watoto wakiwa shule.
Baada ya kupata nafuu,msichana huyu ametueleza hayo na kusema kuwa leo hii jamaa alikuja na wenzie wawili akiwa na kichupa kidogo chenye maji mkononi na kumwagia usoni,akaanguka na kupoteza fahamu hadi alipostuka mbele yetu jioni hii.
Tumekuta nyumba imepekuliwa sana kama watu waliokuwa na muda wa kutosha kutafuta vitu na nadhani walikuwa wakitafuta pesa nyingi ingawa walikuta tu laki 8 kabatini.
Kilichonifanya niandike hapa ni taarifa tulizozikuta polisi kuwa matukio ya aina hii yameanza kushamiri sana hivi sasa na wamepokea malalamiko mengi ya aina hii na baadhi ya watu kukamatwa wakiwamo akina mama wawili wa kiarabu wanaodaiwa kumuuzia maji hayo mmojawapo wa watuhumiwa.Nawatahadharisha wakazi wenzangu wa Dar kuwa waangalifu.
Inasemekana wezi hummwagia mtu maji usoni au hujipaka mikononi ambapo wakimshika tu kwa mikono hiyo anapoteza fahamu.Sijafahamu kwamba maji haya ni kemikali zenye athari hiyo au ni ushirikina.
Naomba vyombo vya dola vifuatilie kwa undani na kukomesha wizi huu kama ilivyokuwa ule wa kuspray vioo vya magari.Mwenyezi Mungu mwenye haki atawakomesha wale wote wenye kuwaza uovu juu ya wenzao.Tafakari,chunguza,chukua hatua.