Tahadhari wadada.. Tahadhari!

Tahadhari wadada.. Tahadhari!

adakiss23

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
4,946
Reaction score
5,382
Amani iwe juu yenu wana jamvi!

Jana usiku mida ya saa 4 usiku nilikuwa maeneo fulani katikati ya jiji, eneo ambalo kwa tukio lililotokea hakuna anayeweza kuamini. Kulikuwa na mdada m1 akitembea pembezoni mwa barabara. Mara ikatokea bodaboda kukiwa na jamaa wawili wakapunguza mwendo then yule wa nyuma akawa kama anamsalimia yule dada hivi. Bi dada akawa anaendelea na safari yake. Ghalfa yule bi dada akaanza kupiga kelele ya mwizi.

Jamaa wamekwapua mkoba wa mdada wakala kona mtaa wa pili ambao kuna kiza kiasi flani. Jamaa mmoja akawasha gari fasta kuwakimbiza lakini hakufanikiwa kuwakamata. So dada zangu kuweni makini na mikoba yenu.
Siku njema!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
wanalizwa sana dada zetu kuna watoto wa kiarabu wana pikipiki baja wanatembelea hasa mitaa ya obay na masaki tunawalia timing tu,wameliza dadazetu sana
 
Hapa shuleni kwetu, kuna mwanafunzi mmoja alikuwa akivuta bangi kwa siri siri, sasa baada ya mda kidogo kama wahenga wasemavyo, kikohozi hakifichiki jamaa kichwa kikachanganya jamaa c akaanza kuokota makopo.

Jamani vijana tubadilike,bangi zanini?
 
Da! Sijui dunia ya baadae itakuwaje, maana hakuna kuaminiana. Sasa kila tufanyalo tujihadhari wizi/utapeli, tia shaka kila jambo linalohusu msaada, au kutoa pesa upate pesa. Na chunga mawasiliano yako cm mfano: anakupigia mtu usiemjua usikubari kusikiliza, maelezo/maelekezo yake. Alafu akikupa maagizo usiyatekeleze ogopa wizi kimtandao.
 
Back
Top Bottom