Tahadhari Vibanda vya M-Pesa, Kuweni makini na huu Utapeli

Mafunzo yapo makubwa sana mimi pia nimtoa mafunzo hayo na nawapa sana kwenye semina ila tatizo unayempa semina nimwenye huduma ya m-pesa au tigo pesa ila yeye hua hafanyi anaweka mfanyakazi ambaye hajui chochote mkuu
Wekeni masharti kwa kuwasaidie mtoa huduma lazima awe na cheti toka Voda au Tigo ikiwemo kitambulisho na picha yake.
 
1)moja ya kosa ni kumpa mtu simu yako yenye salio aingize namba,kuwa smart weka kitabu na kalamu aandike namba mweyewe
2)kuna tabia nyingine mtu anakuja na pesa umtumie anakukabidhi unahesabu anakuchanganya kidogo anatoka kabla hujatuma anarudi anakuambia naomba ile pesa kwanza ninaetaka kumtumia simpati,unamrudishia atazuga kama anaongea na simu ukishampa hiyo pesa,hapo ndipo atakapokuchanganya atakutolea pesa nyingine kama hizo ila ndani utakuta zimepungua.kama mwanzo ulihesabu laki tano za elfu kumi ,juu atapanga elfu kumi ndani elfu mbili.hapo wanakuwepo wenzake wanajifanya kutoa na kuweka pesa panakuwa busy,wewe ukimuona mteja wako unjua kaleta mzigo kamili kumbe ndani kapunguza
 
Huyo jamaa yako ni mwehu, ikitokezea ishu kama hiyo sio wewe wakala unaeirejesha hiyo hela kwa muhusika, ni tigo wenyewe ndo hua wanairehesha, so alikua awaambie hakuna utaratibu huo, asubirie tigo wenyewe ndo wangemrejeshea
 
Matapeli wa siku hizi wanatumia akili kidogo halafu ushirikina mwingi. Unaweza kutapeliwa mpaka mwenyewe ukashangaa imekuwaje ukatapeliwa kirahisi namna hii. Ukweli 'mijamaa' inatumia sana ushirikina.
 
Mjinga huyo, acha aibiwe, boss wake hakumpa semina kabla ya kumpa kazi? (cheap labour). Atajifunza next time.
 
Muhudumu yeye hakuangalia salio lake kabla ya kutii maagizo ya tapeli? Kwa sababu angeangalia salio kwanza lingebaki vilevile 890,000 na wala sio 1,690,000
 
Matapeli wa siku hizi wanatumia akili kidogo halafu ushirikina mwingi. Unaweza kutapeliwa mpaka mwenyewe ukashangaa imekuwaje ukatapeliwa kirahisi namna hii. Ukweli 'mijamaa' inatumia sana ushirikina.

Wekeni masharti kwa kuwasaidie mtoa huduma lazima awe na cheti toka Voda au Tigo ikiwemo kitambulisho na picha yake.
Mashart nimakubwa zaidi ya hayo usemayo maana ili uwe wakala voda au tigo masherti ni leseni ya biashara TIN namba ya T.R.A na paspot size barua ya serikali na vyote viptie mahakamani kwa mwanasheria apge mihuri hapo ndo unatengenezewa laini ya uwakala. Ila wakati mwingine watu hununua hizi laini hivyo kua wakala asiyejua mambo hayo
 
Muhudumu yeye hakuangalia salio lake kabla ya kutii maagizo ya tapeli? Kwa sababu angeangalia salio kwanza lingebaki vilevile 890,000 na wala sio 1,690,000
Ye alikua makini asitapeliwe pale aliposimama na mteja, na alijua sababu mwisho wa siku atakaeweka amount na password ni yeye mwenyewe Wakala basi hakuona shida yoyote,
Wala lilipokuja tukio la pili la kuambiwa kua kapokea hela kimakosa hakuweza kuhusianisha na tukio la kwanza kabisa. Hata wakati anahojiwa na Boss wake yeye mwenyewe hakujua kua tapeli wake alikua nae muda mchache uliopita. Ila baada ya kuambiwa aelezee matukio yote ndio ikagundulika jinsi mchezo mzima ulivyochezwa
 
Huyu aliyeachwa dukani ameshirikiana nao hao wezi, umeambiwa hela imeingia kwako kimakosa sawa, hauangalii balance yako kabla ya yote?
 
Back
Top Bottom