TAHADHARI: Uwasilishaji Ripoti ya Pili Jumatatu ni mbinu ya kuteka mjadala wa Bajeti

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,035
144,386
Wadau,kwa mtazamo wangu,Ripoti ya Pili kuhusu mchanga wa dhahabu kuwasilishwa jumatatu siku ambayo mjadala wa Bajeti inaweza ikawa ni mbinu tu ya ku-divert attention ya watu wakiwemo wabunge ili mjadala wa Bajeti upite kiulaini.

Tundu Lissu na wapinzani kwa ujumla muipe kisogo taarifa hiyo mpaka kwanza mmalize mjadala wa Bajeti ndio kisha mjikite kuichambua hiyo ripoti.

Wapinzani ni wachache na hamuwezi zui hiyo Bajeti kupita ila logic hapa ni mapungufu ya hii Bajeti umma uweze kuyaelewa kupitia kwenu ili huko baadae ije ieleweke nani alikuwa chanzo cha matatizo.

Ni mtazamo wangu huu.
 
Wabunge waegemee kwenye mjadala wa bajeti ripoti ya makinikia watuachie
 
na mara zote iko hivyo
rejea matokeo dsm vs madawa ya kulevya mwisho wa siku trick ikamuumbua mtu
"shimo wamechimbia mimi watatumbukia wenyewe" jennifer mgendi
 
Unawapangia cha kufanya au?? Wamepokea riport hutak isomwe kwa manufaa ya nan? Siasa ni mchezo na wanaoongoza wanajua kuupanga vzr. Bajet itapita hakuna wa kuzuia,itajadiliwa mkitaka mtoke nje kama mwaka jana na mambo yatakwenda mpende msipende.
 
Ripoti inawasilishwa siku moja mijadala ya bunge Ya Bajeti inajadiliwa siku kibao kuanzia jumatatu unaongea utafikiri mjadala wa bajeti ni siku moja.
 
Mkuu kwa kupenda font fed tu hajambo, angetuwacha kwanza tukakokotolewa bajet
 
Sasa mtoa hoja unataka suala moja liachwe na mengine yasimame kama mdomo unapokunywa maji?? wabunge wafanye kazi yao ya kujadili bajeti na rais afanye kazi yake ya kupokea majibu ya tume aliyounda. Sasa kama wabunge wataacha kazi yao waliochaguliwa kuifanya na kushadadia report ya tume basi hawajui majukumu yao.
 
Bajeti ilishapita kabla ya kujadiliwa! Kilichobaki tusubiri tu maumivu Julai mosi.
 
Acha uongo ww
 
. Bajet itapita hakuna wa kuzuia,itajadiliwa mkitaka mtoke nje kama mwaka jana na mambo yatakwenda mpende msipende.
Ndiyo itapita tu, kwani wingi wa CCM ndiyo kutawezesha hilo. Lakini, katika nafsi yako, unafikiri kuna manufaa yoyote ya bajeti kupita kama hadi sasa bajeti ya mwaka jana imetekelezwa kwa 34% tu? What's the point of having budgetary parliament?
 
Bajeti imepita. CCM watapitisha tu, tuangali hili litakalo chomoza J3 ni jema au la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…