TAHADHARI! Usiuze mwaka wako 2011!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAHADHARI! Usiuze mwaka wako 2011!!!!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kionambele, Dec 31, 2010.

 1. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo ni tarehe 31 Desemba 2010. Wengi hudhani hii ni tarehe tu kama zingine lakini siku hazifanani jamani. Kila tarehe zina maana yake na sababu zake katika kila mwaka.

  Kwa kifupi mambo yafuatayo yatakusaidia sana maishani mwako.

  1. Sura ya mwaka wako mzima wa 2011 itaamuliwa na mwaka huu utakukuta wapi ukiwa unafanya nini. Je utakuwa kwenye nyumba ya ibada? basi Mungu utakayekuwa ukimuabudu hapo ndiye atakuwa mmiliki wa mwaka wako wote.

  Je utakuwa kifuani pa mume wa mtu wakati huo? Basi mwaka wako utakuwa mikononi mwa Pepo la Uzinzi na kwa hakika unaweza usiuvuke.

  Je mwaka utakukuta umelewa chakari? Basi ulevi umekabidhiwa mwaka wako.

  Je mwaka utakukuta ukijiandaa kwenda kudhuru wengine? mwaka wako utakuwa mikononi mwa shetani.


  2. Kwa baadhi ya koo ambazo hutoa kafara kila mwisho wa mwaka, huu ndio wakati wa kujua kama umetolewa au umevuka mwaka. Lakini kwa waliojikabidhi mikononi mwa Bwana Yesu hawana haja ya kuogopa kitu, wao wanalindwa na Yesu na hakuna la kuwapata.

  3. Leo ndiyo siku ya kumshukuru Mungu kwa mwaka mzima 2010 na kumkabidhi 2011 mipango yako yote na ndipo utakuwa umejihakikishia mwaka mwema wenye heri na mafanikio makubwa.

  4. Kuna watu watatumika kukualika kwenye sherehe za kishetani lengo likiwa waiteke nyota yako ya mwaka mzima 2011, hivyo usiwe mjinga hakikisha mwaka unakukuta ukiwa unamshukuru na kumwomba Mwenyezi Mungu. Usikubali kuwa katika dhambi wakati mwaka ukiwa unaingia.

  Mungu awabariki na kuwalinda wanaJF wote!! Heri ya mwaka mpya 2011!!!!
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  asante...
   
 3. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Amina!
   
 4. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amina na ubarikiwe kwa utumishi huu, hakika maneno yako yataokoa roho zilizotaka kufanya mambo ya kishetani mwaka mpya!!!!!!!!!!!
   
Loading...