Tahadhari: Ugonjwa wa ebola umeingia Uganda

MR TOXIC

Member
Jun 4, 2019
72
125
Mtoto wa miaka mitano nchini Uganda apatikana kuwa na Ebola, shirika la afya duniani (WHO) limethibitisha.

Hiki ni kisa cha kwanza kuthibitishwa katika nchi hiyo wakati kukishuhudiwa mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo .

Zaidi ya visa 2,000 vimenakiliwa huko katika muda wa miezi 10 iliyopita - wengi wa waathirika wakifariki.

Inaarifiwa kuwa mtoto huyo wa kivulana alisafiri na familia yake na kuvuka mpaka kutoka Congo siku ya Jumapili.

Baada ya hapo alipelekwa katika hospitali moja nchini Uganda baada ya kuonyesha dalili ikiwemo kutapika damu, maafisa wamesema.

Uthibitisho kwamba ni ugonjwa wa Ebola ulitolewa na taasisi ya kupambana na virusi nchini Uganda Virus Institute (UVRI) jana Jumanne kal aya kutangazwa rasmi na maafisa jana usiku.

Waziri wa afya Uganda Jane Ruth Aceng amewaambia wanaandishi habari kwamba familia ya mtoto huyo wanaangaliwa, wakiwemo wawili walionyesha kuwa na dalili za kama za ugonjwa wa Ebola.

Baada ya hapo alituma ujumbe kwenye Twitter akieleza kwamba nchi hiyo imeingia katika 'hali ya muitikio'kufuatia kisa hicho.

Kwa Taarifa zaidi pitia taarifa hapa chini


Confirmation of case of ebola virus disease in Uganda

Kampala, 11 June 2019 - The Ministry of Health and the World Health Organization (WHO) have confirmed a case of Ebola Virus Disease in Uganda. Although there have been numerous previous alerts, this is the first confirmed case in Uganda during the Ebola outbreak on-going in neighbouring Democratic Republic of the Congo.

The confirmed case is a 5-year-old child from the Democratic Republic of the Congo who travelled with his family on 9th June 2019. The child and his family entered the country through Bwera Border post and sought medical care at Kagando hospital where health workers identified Ebola as a possible cause of illness. The child was transferred to Bwera Ebola Treatment Unit for management. The confirmation was made today by the Uganda Virus Institute (UVRI). The child is under care and receiving supportive treatment at Bwera ETU, and contacts are being monitored.

The Ministry of Health and WHO have dispatched a Rapid Response Team to Kasese to identify other people who may be at risk, and ensure they are monitored and provided with care if they also become ill. Uganda has previous experience managing Ebola outbreaks. In preparation for a possible imported case during the current outbreak in DRC, Uganda has vaccinated nearly 4700 health workers in 165 health facilities (including in the facility where the child is being cared for); disease monitoring has been intensified; and health workers trained on recognizing symptoms of the disease. Ebola Treatment Units are in place.

In response to this case, the Ministry is intensifying community education, psychosocial support and will undertake vaccination for those who have come into contact with the patient and at-risk health workers who were not previously vaccinated.

Ebola virus disease is a severe illness that is spread through contact with the body fluids of a person sick with the disease (fluids such as vomit, feces or blood). First symptoms are similar to other diseases and thus require vigilant health and community workers, especially in areas where there is Ebola transmission, to help make diagnosis. Symptoms can be sudden and include:

Fever

Fatigue

Muscle pain

Headache

Sore throat

People who have been in contact with someone with the disease are offered vaccine and asked to monitor their health for 21 days to ensure they do not become ill as well.

The investigational vaccine being used in DRC and by health and frontline workers in Uganda has so far been effective in protecting people from developing the disease, and has helped those who do develop the disease to have a better chance of survival. The Ministry strongly urges those who are identified as contacts to take this protective measure.

Investigational therapeutics and advanced supportive care, along with patients seeking care early once they have symptoms, increase chances of survival.

The Ministry of Health has taken the following actions to contain spread of the disease in the country:

The District administration and local councils in the affected area have been directed to ensure that any person with Ebola signs and symptoms in the community is reported to the health workers immediately and provided with advice and testing.

The Ministry of Health is setting up units in the affected district and at referral hospitals to handle cases if they occur.

Social mobilization activities are being intensified and education materials are being disseminated.

There are no confirmed cases in any other parts of the country.

The Ministry is working with international partners coordinated by the World Health Organization.

The Ministry of Health appeals to the general public and health workers to work together closely, to be vigilant and support each other in helping anyone with symptoms to receive care quickly. The Ministry will continue to update the general public on progress and new developments.


BBC
 

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,607
2,000
1126414


WaTanzania wameombwa "wasiwe na hofu" kuhusu kusambaa kwa Ebola, waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kufuatia taarifa za Ebola kuingia Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mpaka wa Tanzania unashikana na wa Congo, ambako virusi vya ugonjwa huo vimesababisha vifo vya takriban watu 1, 400.

Kauli hii inatolewa wakati Uganda imethibitisha kwamba kuna visa visaba vya watu wanaoshukiwa kuugua ugonjwa huo nchini.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, Bi Mwalimu amesema Tanzania "imekuwa ikichukua hatua za utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu"


Tumepokea kwa Tahadhari kubwa uwepo wa ugonjwa wa #Ebola nchini Uganda.Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikichukua hatua za utayari (preparedness) wa kukabiliana na ugonjwa huu. Wananchi wasiwe na hofu. Tutatoa Taarifa zaidi kwa umma ktk siku chache zijazo.


Hapo jana Tanzania, pamoja na Kenya, zilizindua mpango wa ukaguzi wa watu wanapovuka mipaka kuingia katika nchi hizo. Mpango huo utawasaidia maafisa kusambaza kwa haraka taarifa kuhusu iwapo kumegunduliwa visa vyovyote vya Ebola, waziri huyo ameeleza.

Wizara ya afya nchini Kenya kwa upande wake imetoa taarifa ikisema imetoa tahadhari kwa maafisa wote wa afya na umma kushinikiza hatua za uangalizi.Wizara hiyo imeeleza kwamba inaendelea kuufuatilia mlipuko huo wa muda mrefu katika jamhuri ya Kideokrasi ya Congo ulioanza mnamo Agosi mwaka jana, kwa lengo la kuimarisha utayari na muitikio wa wa Kenya katika kukabiliana na visa vya ugonjwa huo.

KUUTAMBUA UGONJWA WA EBOLA

  • Ni ugonjwa unao sambaa haraka na hupelekea vifo vya asilimia 50 ya waathirika
  • Dalili za awali ni homa ya ghafla, uchovu kupita kiasi, maumivu ya mishipa na koo.
  • Dalili za hatari ni kutapika, kuharisha, na kwa kesi zingine ni kutoka damu ndani na nje ya mwili.
  • Ebola huwapata binadamu wanapo gusana na wanyama walio athirika wakiwemo sokwe mtu, popo na paa.
  • Watu wanaambukiza endapo damu zao na maye vimebeba vijidudu, na hii inaweza fika mpaka wiki saba tangu mtu alipopona.
UGANDA IMEKABILIANA VIPI NA EBOLA SIKU ZA NYUMA?

Serikali ya Uganda imeidhinisha matayarisho makubwa kwa hali inayoshuhudiwa sasa:

1. Ni muhimu kukubuka kwamba serikali imeidhinisha mifumo na utaalamu kukabiliana na Ebola kwa usaidizi wa taasisi za udhibiti wa magonjwa za Marekani na shirika la afya duniani. Madakatri wa Uganda wamewahi kutumwa kwenda kusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo ulipozuka Congo na mataifa ya Afrika magharibi.

2. Ukaguzi na uthibitisho wa visa: majaribio yote hufanyika nchini Uganda katika maabara ya serikali. Iwapo serikali imeshindwa kuthibitisha sampuli nchini, basi zinasafirishwa katika makao makuu ya udhibiti wa magonjwa Atlanta Marekani.

3. Serikali ndio huthibitisha mlipuko, visa, au vinavyoshukiwa.

4. Kilichoisaidia Uganda kukabiliana na ugonjwa huu ni mamlaka ilio nayo kuhusu suala hili na kupeuka uvumi, na uzushi jambo linalochangia imani kutoka kwa umma.
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
982
1,000
Akhsante kwa taarifa mkuu;

Tanzania imejiandaaje jinsi ya kukabili ugonjwa huu hatari, if Uganda epidemic elapses means parts of Tanzania are also tremendously affected. kuna kakituo kamoja tuu pale Temeke Hospitali kako kama darasa la chekechea, eti kwa nchi nzima na hakina Madaktari wala manesi wenye moyo wa kujitolea, ,

akitokea mgonjwa mahali popote dar slaam, utasukumwa Temeke, na Madaktari sasa wa temeke ni kichekesho wakiona mgonjwa ana mp ya kawaida tu hasa kipindi hiki, wanamkimbia, wanogopa kufa, japo vifaa na madawa vipo, hapo waziri wa afya hajafanya la maana kabisa, apitie huko atafute mbinu juu ya kukabiliana na hali hii. mtakufa woote kama kuku ukiingia huu ugonjwa. na nchi yetu kwa sasa kidplomasia siyo nzuri sana. Mnene hajulikani kimataifa kiviiile, hata japo kupeana mawazo tu na wenzake hapo kusini tu, miaka mitano sasa imepita. jamani, hajaenda rasmi kusalimia, zaidi ya hivi juzijuzi tu alivyoalikwa kwa mbinde, anaangalia kwake tuuu eti ili asipinduliwe na kupewa changamoto kwa kuwabana wananchi wasipumue, ili aishi vizuri, Baba wa mji unatakiwa utoke wakujue upige domo weee watoto wale, ni shida sana, si muliona hata Ramaphosa siku ya kuapishwa kwake alipita faster wakati wa kusalimiana, ila kwa Kikwete alitulia kidogo tena wakapiga na picha, sura ya kimataifa ile, kifupi tutegemee poor respond from neighbouring countries. wakati wa majanga kama hili
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
982
1,000
Angekuwa Kikwete mngeona sasa hivi mavifaa ya kufa mtu yangeshushwa na midege ya USA,WHO, na posho za kutia moyo kwa madaktari, yaani wanaona kweli wanathaminiwa,

kupewa financial support na jirani au rafiki siyo utumwa. una socialise,

si mmnena kwenye methali zenu kuwa '' mtu pweke ni uvundo''

''Watu ni mali'' - mtu ni watu! kidole kimoja hakinanii.......

siyo nyinyi waswhili mloandika hivo?. eti mnajidanganya Tanzania tajiri, tajiri bila akili?
haya chukua hiyo dhahabu sijui uranium yakohiyo chimba ikutibu Ebolla,

maskini hata hamjui hizo minerals zinaendaga wapi

hata hako kajumba kalijengwa enzi za Kikwete bure na wafadhili.bado kako vilevile kama alivo kaacha, na gonjwa ndo hilo raja kwa kasi. awache mfe kwanzaaa ndo mjue umuhimu wa Rais mzalendo ni nini, tena anaweza acha maksudi tu ili mpunguze kilimi limi. yeye si anataka amani binafsi?
 
Top Bottom