Tahadhari: Ufisadi katika awamu ya tano utaweka historia kuliko tawala zote!

Hata ufisadi wakati wa Nyerere ulikuwa mkubwa mno
but ulifunikwa na 'wana Taasisi' hadi wakamtangaza 'mtakatifu'
iwapo John atafariki leo naweza kutabiri bila shida mchakato wa kumtangaza
'mtakatifu' utaanza mapema sana...

Kawaida ufisadi wa 'waswahili' hutangazwa sana..lakini ufisadi
wa wana 'taasisi' utashangaa ukifunikwa..

usisahau kulikuwa na ufisadi wizara aliyoiongoza mkubwa tu na ulifunikwa

Mkuu sina uhakika na hili lakini wengi wenye akili tunajua aliyoayafanya akiwa wizara hiyo ni ya kutisha na CAG kila mwaka aliyaanika waziwazi.
 
tutanyanyasika sana kwa maamuzi mengine lakini hakuna mbabe mbele ya mauti.....ipo siku.....!
 
Ilikuwaje zabuni ilipewa kampuni bobevu na ya bei rahisi ghafla mchakato ukatwaliwa na Ikulu na kisha kupewa tenda kampuni nyingine isiyo na sifa tena kwa bei ya juu?
Nimewahi kushiriki ktk michakato hiyo na moja ya kigezo wanachohangaika kukisimamia watu wa manunuzi ni bei ya chini. Mara zote utawakuta wanasema hivyo. Kwa kiwango kikubwa ni collusion, trick na leakage ya information ili wagawane pesa. Tunayajua haya.

Muhimu ktk hayo, siyo bei ya chini tu. Kuna kitu muhimu, after-sale service. Mambo ya kusema wamebobea, nani nchi hii anajiganmba kubobea? Ni ubabaishaji tu.
 
PPRA ni sheria ambayo imeridhiwa na watanzania wote kupitia bunge, kama sheria haifai aidha irudishwe bungeni ifanyiwe marekebisho au ifutwe kabisa.

ni afadhali mchakato wa manunuzi kwa sheria ya PPRA unaweza kuwa na rushwa za ndani lakini bei ikawa the lowest na akapatikana lowest bidder kuliko huu utatibu wa tenda za ikulu, ambao bei wanaamua watu wachache
Hata sheria ya Takrima si ilipita Bungeni? Hata upuuzi hupita Bungeni. Bei ya chini siyo kigezo cha maana sana ktk manunuzi. Take care of after-sale service! Underline that!
 
Akili ni kubadili hizo sheria tunazoona mbovu na siokutokufuata sheria kabisa.

Kinyago tumekichonga wenyewe sasa unalaumu kinatisha
Suala siyo sheria mbovu, tuna watekelezaji wabovu. wanakwenda kutafuta njia ya kupata rushwa badala ya kufuata sheria inasemaje. Hata kwa vitu vya kipuuzi kabisa! Unanunua karatasi kwa sh. 15000 badala ya 7000. Unanunua Toyota kwa mil 200 badala ya 150! eti mchakato umefuatwa! RUBBISH!
 
Suala siyo sheria mbovu, tuna watekelezaji wabovu. wanakwenda kutafuta njia ya kupata rushwa badala ya kufuata sheria inasemaje. Hata kwa vitu vya kipuuzi kabisa! Unanunua karatasi kwa sh. 15000 badala ya 7000. Unanunua Toyota kwa mil 200 badala ya 150! eti mchakato umefuatwa! RUBBISH!
Umeshindwa jibu hoja!! Why kampuni ya bei rahisi ya kuchapa passport ilitupwa ikachukuliwa ya gharama za juu sana?
 
Kama ni kwel hayo yabafanyika basi tuvute subra, siku awamu ya 5 ikimaliza muda wake tuttajua ukwel.
Hivi wakati tunasubiri, si maisha yetu ndio yanakuwa rehani sababu muda unakwenda kwa kasi.....maana hadi anamaliza mkulu ni miaka 10 itakuwa imekatika......huo muda si unakwenda.....?!
 
Umeshindwa jibu hoja!! Why kampuni ya bei rahisi ya kuchapa passport ilitupwa ikachukuliwa ya gharama za juu sana?
Siyo kila swali lina jibu? Kuna maswali ya kipuuzi, nami silingani na upuuzi unaotaka nijibu.
 
Back
Top Bottom