shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Nchi yoyote duniani huongozwa na sheria na taratibu zake,hata hapa kwetu Tanzania naamini sheria hizo na taratibu zipo.Lakini kuwa na taratibu na sheria ni jambo moja,ila kutekeleza ni jambo linngine.
Kuna huu uvunjaji wa sheria tena wa wazi kabisa unaofanywa na baadhi ya madereva hasa wa magari ya abiria kuingia na abiria kwenye vituo vya kuweka mafuta(petrol station).Hivi tushawahi kujiuliza endapo inatokea ajali ya moto na abiria wapo hapo kwenye gari,nini kitatokea?Au tumezoea maafa yanapotokea ndipo tuanze kuunda tume ya uchunguzi?
Kuna mambo ya kuchezea lakini si usalama na maisha ya watu.Haitasaidia vifo vimetokea halafu Rais aanze kutoa salamu za pole kwa "familia zilizopoteza ndugu zao".Tuna nafasi ya kuzuia majanga mengine kwa kuzisimamia sheria na taratibu zilizowekwa.Na hata sisi abiria tuwe na kauli moja tunapoona madereva wanatuingiza kwenye vituo vya mafuta kwani kwa kufanya hivyo tutaweza kuepusha madhara makubwa.
Pamoja tunaijenga nchi yetu!