G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,592
- 36,008
Kwanini naliona giza nene?
Mradi wa bomba la mafuta kutoka kaskazini mwa Uganda hadi Tanga kwenye bandari sasa ni dhahiri na kampuni ya TOTAL itausimamia mradi huu.
Kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya Kenya na Tanzania kuhusu kuishawishi TOTAL iteuwe nchi moja ya kupitisha bomba hili huku Uganda ikiviangalia vita hivi vya panzi!
Baada ya Kenya kuhisi ingeshindwa kwenye vita hii ilianza mpambano kivingine, ikatuma majasusi ambao hatujui walitoka na data zipi pale Tanga, pia rais wa Kenya akaanza jitihada nyingi mno kuvuta mradi huu.
Sasa Kenya wamekuja kivingine! Tayari wameamua kujenga bomba kutoka kaskazini mwa Uganda hadi bandari ya LAMU kwa gharama ya fedha zao za ndani.
1) Gharama ya mradi kwa Kenya ni nusu ya gharama ya mradi kwa Tanzania.
2) Kenya imefanya uwekezaji mkubwa kwenye bandari ya LAMU ambapo ndipo bomba litaishia ambayo itakuwa na uwezo mkubwa sana wa kubeba mameli makubwa hasa yale ya mafuta (wameamua kuachana na bandari ya Mombasa ambayo nayo ni bora kuliko ya Dar)
3) Muda wa kukamilika mradi kwa Kenya ni mfupi kuliko Tanzania.
Kwenye mradi kuna "return on investment" Pia kuna pay back period. Nionavyo mimi TOTAL ni lazima arejeshe investmen cost na hii ni lazima iwe kwenye tozo mbalimbali za kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi bandarini. Tukija kwenye pay back period; kama kiasi tulichokubaliana kurejesha kwa mwaka kikafeli kutokana na ushindani wa kibiashara kuwa mkubwa itabidi kuwe na mbadala ambapo serikali itatafuta fedha kwingine. Kenya wao watasimama kama serikali kwani wametumia fedha za ndani. Sisi ni lazima serikali iingize na TOTAL nae aingize ili arejeshe gharama zake.
Sisi wakati tumepeleka bomba Tanga kwenye bandari ndogo sana ya meli ndogo na mitumbwi, tumeenda kuboresha bandari ya Bagamoyo ambapo nayo mradi wake haueleweki.(Hapa Lowassa kama alijua) Hapa tunajiandaa kwa ushindani kweli?
Wakati ambao tutakuwa tunajiuliza hayo Uganda yeye atakuwa anafanya biashara! Akiwahi Kenya atapata akiwahi Tanzania atapata! Yeye hana haja na shida zenu!
Wakati sisi tukiwa hatujang'amua ni vipi tutarejesha fedha ya muwekezaji TOTAL yeye Kenya ataweza kuwa ameshachanja mbuga kuelekea Sudani Kusini! Tumejipangaje?
Ikumbukwe kuwa Kenya alishatuma majasusi na hatujui walifanikiwa kupata nini wakakitumia kama fimbo.
Tumejipangaje? Hapa sasa tutakuwa tunafanya ushindani wa kibiashara na Kenya! Uganda yeye amefurahi zaidi kwani atauza kwa wawili badala ya mmoja! Tumejipangaje na miundombinu na tozo? Tunaelekea?