Masulupwete
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 2,366
- 2,435
Nikiwa katika pilikapilika zangu za kipindi cha pasaka nilikutana na kituko kimoja kilichonishangaza na naona ni vema nikashea hapa. Nikiwa eneo la ilala bungoni DSM nilishuhudia trafiki akisimamisha gari aina Toyota coaster iliyokuwa ikitokea buguruni kuelekea mjini kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Katika hali ya mshangao mara baada ya gari kusimama kundi la abiria ambao wengi ni vijana wadogo pengine hawajazidi hata miaka 20 waliruka kupitia madirishani na kutokomea mitaa ya jirani. Trafiki alikagua gari na kukuta silaha za hatari zikiwemo mapanga, rungu, sime na vitu vingine vyenye ncha kali.
Kulikuwa na mazungumzo kuwa vijana hao ni kawaida yao kukodi gari wakidai wanaenda beach kuogelea lakini pindi wakifika huko hutumia hizo silaha kupora watu wanaowakuta huko. Vijana hawa wamejiunda kwenye makundi yao maarufu kama camps.
Kwa wapenzi wa picha mtanisamehe sikufanikiwa kupata picha mchina wangu aliisha chaji ningewawekea muone tunakoelekea