Omari R Nundu
R I P
- Nov 11, 2007
- 10
- 74
TAHADHARI MTANZANIA
1.1 Tafakari ni muhimu, kwa mja mwenye busara,
1.2 Kuwaza ya kuhukumu, hoja na mawazo bora,
1.3 Hadi zijiri takwimu, kuziepuka hasara,
1.4 Tumwombe sana Karimu, atwepushe na idhara.
2.1 Umoja si jambo gumu, si kikiri na kakara,
2.2 Kuwaza kwa kinidhamu, itikadi na fikira,
2.3 Yawe mema ya kudumu, tuinadi takibira,
2.4 Na kuchapa kazi ngumu, ibakiayo subira.
3.1 Tekeleza majukumu, wenye shida wana hera!
3.2 Tenda mambo kwa awamu, usifanye kwa papara,
3.3 Anza na ya kujikwimu, ufahari sio sera,
3.4 Hata wakikulaumu, usijitoe kafara.
4.1 Matendo mema hudumu, duniani na akhera.
4.2 Watendee binadamu, usingoje mshahara,
4.3 Kila mja na msimu, dunia ni mduara,
4.4 Chungu leo kesho tamu, wala haya si nadra.
5.1 Waja wema wana hamu, 'upae kama tiara',
5.2 Kila jema uhitimu, sifazo ziwe toara,
5.3 Lisiwepo jambo gumu, la kukutia harara,
5.4 Usiwe wa kukahimu, bali uwe barabara,
6.1 Siku hizi kuna simu, piga ukigaragara,
6.2 Huitaji baragumu, kuisambaza dhamira,
6.3 Kila mji na sehemu, imeenea minara,
6.4 Si ruhusu mahasimu, uwezo wakakupora,
7.1 Wapelekee salamu, wanasiasa chokora,
7.2 Kila wakimwaga sumu, iwageuke kafara,
7.3 Wakome kukuhujumu, hata bila ya bakora,
7.4 Katu usijilaumu, watapogeuzwa sura.
8.1 Wategemea mizimu, hawaijuwi kudra?
8.2 Hata waliosilimu, hawafanzi mas'hara,
8.3 Sembuse wao walimu, vilemba vilivyofura,
8.4 Hawaswabih ismu, Rabbika wao ni kura?
9.1 Natowa hii elimu, siambe nawacharura,
9.2 Kukosa kwao nidhamu, hakunitii hasira,
9.3 Bali ijuwe kaumu, weusi na machotara,
9.4 Kwamba hawa madhalimu, SI HAKI YAO KUPORA!!
Eur Ing. Omari Rashid Nundu
Iringa, Tanzania
28 Oktoba 2014