Tahadhari: Mafuriko makubwa kutokea Tanzania

Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,581
6,675
Kuna taarifa imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa watu wawe na tahadhari kwani kuna uwezekano wa kunyesha mvua kubwa sana kama ilivyotokea hv majuzi.

Mvua hizo zitaathiri mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, Unguja, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Rukwa, Tabora na Kigoma.

Kwa wale wanaoishi Dar watakubaliana na hili hasa ukiangalia upande wa Magharibi kuna wingu kubwa limetanda.

Source: Clouds FM
 
Nilikatiza kigogo luhanga na kuona athari manake watu wanafanya usafi wa kuondoa tope na kufua. Kama ile ni trailor basi picha yenyewe itakuwa hatari sana.
Kiukweli serikali na jamii kwa ujumla haiwezi kuwafidia waathirika wa mafuriko ni wengi sana na damage ni kubwa mno na tahadhari hazionekani zikichukuliwa.

Msiba mwingine huo
 
Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imetoa tahadhali kutokea mvua kubwa kuanzia kesho na kuelekea mwaka mpya.Mikoa inayotarajiwa kuathirika zaidi ni Dar,Pwani,Dodoma,Singida,Tabora,Iringa,Mbeya na Kigoma.Wananchi wanaoishi mabondeni wametahadharishwa kutokurejea maeneo hayo. Source:TBC1.
 
Wana JF.
Mamlaka ya hali ya hewa nchini yatoa tahadhali kutokea kwa mvua kubwa kuanzia hapo kesho.

Kuelekea mwaka mpya wa 2012 mvua hizo zitaathiri mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, Unguja, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma.

Wakazi waishio mabondeni wanatahadhalishwa waondoke mapema.

SOURCE: TBC HABARI MPASUKO
 
Wana JF.
Mamlaka ya hali ya hewa nchini yatoa tahadhali kutokea kwa mvua kubwa kuanzia hapo kesho.

Kuelekea mwaka mpya wa 2012 mvua hizo zitaathiri mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, Unguja, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida,

Wakazi waishio mabondeni wanatahadhalishwa waondoke mapema.

SOURCE: TBC HABARI MPASUKO

Ongeza: Rukwa, Tabora na Kigoma.
 
Kuna taarifa ambayo TBC1 wameitoa kama habari mpasuko usiku huu nafikiri inahusu mvua maana nimekuta inaishilia. Maneno ya mwisho niliyoyasikia ni kuwa watu wa mabondeni wachukue tahadhari. Kuna yeyote aliyeisikia taarifa kamili atujuze?
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, imetoa taarifa kua kuanzia kesho mpaka Mwaka mpya kunatarajia kuanza kunyesha mvua kubwa kuliko maelezo! Mikoa itakayokubwa na kadhia hyo ni Dar km kawa, Kgm, Singda, Ddma, Iringa, Mtwara, Pwani, Tanga, Mbeya, Morgr. Wakazi wa mabondeni hasa wale wabishi wanatakiwa kuyaaga makazi yao mara moja kabla ya kukutwa na hiyo noma!
Nawasilisha. (Source; TBC1)
 
nasikia washarudi ktk makazi yao
tatizo la sisi watanzania ni wabishi hadi tuone maji yakijaa ndio tuanze kulaumu.
serikali nayo ifanye fasta kuwapa viwanja na uwezo wa kujenga makazi mapya
 
Ni taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa inayosema kuwa kuanzia kesho kutakuwa na mvua kubwa katika mikoa ya dar, dodoma, pwani, mtwara, lindi, unguja, mbeya, rukwa, singida, tabora, iringa na kigoma. Wakazi wa mabondeni wanatahadharishwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tumekwisha...!! na hii miundombinu yetu, na kuwaachia watu wanajenga kwenye mkondo wa maji...!! sasa watu wanakufa hakuna wa kusema tunabakia maneno tuuuu...!!
 
sometimes tma wasanii tu wale wenzangu wa mabondeni angalieni juu mpaka muone wingu jeusi
 
Kama hiyo tahadhari imetolewa na mamlaka ya hali ya hewa ya nchi hii, hata haina haja ya kuhofia kwani wanaweza wakasema mvua itanyesha badala yake bonge la jua linatandika.

Dharau dharau hizo ndugu? Ni bora ukachuku tahadhari hata kwa taarifa za kichaa, kuliko, kuzipuuza then zikawa kweli.
 
Back
Top Bottom