Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,557
- 19,107
Saa kama tatu hivi zilizopita nilikua Kariakoo kwenye jengo moja la ghorofa saba ambalo hutumika kama makazi ya watu na ofisi pia. Ofisi niliyokua naenda ipo ghorofa hiyo ya saba ambapo ilinilazimu nipande lift
Nilipobonyeza kitufe cha namba ya floor ninayoenda akawa amekuja dada ambaye kwa mavazi yake nikahisi alikua ametoka au anakwenda kwenye mazoezi (nadhani kwenye jengo lile ipo gym) hivyo ikanilazimu nibonyeze kitufe cha kumsubiria akapanda tukaondoka
Sekunde chache tu baada ya kuondoka tukiwa tunapita floor ya tatu taa zikazimika ndani ya ile lift, ikatoa mlio kama imegonga kitu halafu ikawa kama inarudi chini kisha ikasimama kabisaa! Yule dada akapiga yowe la ku panik. Nilipomwambia asiwe na wasiwasi tutatoka akanisogelea na kunikumbatia huku anaendelea kupiga kelele
Changamoto kubwa ni ile milango ya lift yenyewe ilivyokua mizito mpaka unahisi kabisa hata hizo kelele hazifiki popote. Nilinyoosha mkono na kubonyeza kitufe cha emergency bila kuondoa mkono(continuously) lakini hatukuweza kupata msaada kwa haraka
Hali ilikua ya taharuki kubwa maana kile kichumba cha lift ni kdogo, milango ni minene sana na joto lilikua linaongezeka. Tulikaa mle kama dakika saba au nane ambazo zilikua kama mwaka ndipo zikasikika sauti za watu kwa nje wakiwa wanashughulika kutufungulia mlango na muda walipofanikiwa kutufungulia yule dada niliyekua nae alikua amelala chini kwenye sakafu ya lift na akawa kama anaeelekea kupoteza fahamu!!!
Namshukuru Mungu tulitoka salama ingawa yule dada ilibidi apelekwe hospitali kwa hali aliyokua nayo maana hata mambo yake mengine ya kiuanamke (tafsida imezingatiwa) yalimuharibikia na ukizingatia mavazi aliyokua amevaa hakutarajia pengine mambo yamtokee wakati huo!
Wito wangu kwa watengeneza elevators, watengeneze lifts za milango transparent ili mtu aweze kuona nje angalau pressure inapungua kuliko hizi lift zenye milango utadhani gereza au kaburi aisee! Mtu unapokua unawaona watu nje unajua muda wowote unatoka. Amakweli kifo kwa binadamu ni sekunde tu!